Posts

Showing posts from March, 2013

Wa-Marekani Watua kwa Mama Lishe, Usa River

Image
Mwezi Januari mwaka huu, nilipokuwa Tanzania nikifundisha kozi ya Hemingway, niliandaa fursa mbali mbali za kuwawezesha wanafunzi, ambao ni wa-Marekani, kushiriki katika utamaduni wa wa-Tanzania, ili kujifunza. Tulikuwa tumefikia Colobus Mountain Lodge, iliyomo pembeni mwa Arusha National Park. Siku moja, mara tu baada ya wanafunzi hao kuwasili nchini niliwapeleka kwenye mji mdogo wa Usa River, ili wakazunguke na kujionea. Niliamua kuwasafirisha katika dala dala, tukiwa tumebanana. Usafiri ule ulikuwa kitu kipya kabisa kwao, lakini niliona ni muhimu kwao, wajifunze. Tulifika Usa River, tukazunguka mitaa kadhaa, na kisha tukasogea tena pembeni mwa barabara kuu. Hapo wanafunzi walimwona mama lishe akiwa kazini, wakapanga foleni kujipatia chipsi mayai. Kwao hili lilikuwa jambo jipya, ila walifurahia hicho chakula. Niliridhika sana kwamba wanafunzi walipata fursa hiyo ya kujionea na kufaidi huduma ya mama lishe, kwani ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Tanzania ya leo. W

Ufundishaji Wangu wa Maandishi ya Achebe

Image
Nimefundisha maandishi ya Chinua Achebe kuanzia miaka ya sabini na kitu. Kabla sijahitimu na shahada ya kwanza Chuo Kikuu Dar es Salaam, mwaka 1976, huenda nilifundisha Things Fall Apart katika shule za sekondari nilikopelekwa kufanya mazoezi ya kufundisha, yaani sekondari ya wasichana Iringa, 1974, na sekondari ya Kinondoni, 1975. Sina hakika. Lakini baada ya kuhitimu shahada ya kwanza, mwaka 1976, nilipata fursa za kufundisha Things Fall Apart , nikianzia na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo nilikuwa mhadhiri. Mwaka 1980, chini ya mkataba wa ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi, nilifundisha kwa wiki kadhaa katika Chuo Kikuu cha Burundi. Kitabu kimojawapo kilikuwa Things Fall Apart Uzoefu huu ulinifanya niandike mwongozo wa Things Fall Apart , ili kuelezea mambo ambayo waandishi wengine hawajayaweka wazi.  Ilikuwa ni fursa kwangu kuwaelezea wanafunzi na walimwengu namna ninavyoichukulia riwaya hii ya Things Fall Apart . Kwa maelezo zaidi ya historia hii, soma hapa . Sihit

Achebe wa Enzi za Ujana Wetu

Image
Sisi tuliosoma sekondari miaka ya sitini na kitu tunaikumbuka picha ya Chinua Achebe inayoonekena hapa kushoto. Ndio picha iliyokuwepo kwenye jalada, upande wa nyuma wa kitabu cha Things Fall Apart . Kwa bahati nzuri, ninayo nakala ya miaka ile ya Things Fall Apart. Niliipata miaka ya karibuni, nikaona niwe nayo, angalau kujikumbusha enzi za ujana wetu. Ninazo pia nakala za matoleo ya hivi karibuni, lakini ile ya zamani niliiona kama lulu. Kuanzia mwaka 1966 hadi 1970 nilikuwa mwanafunzi wa sekondari, seminari ya Likonde. Wakati huo riwaya ya Things Fall Apart ilikuwa maarufu. Tulivijua pia vitabu vya watoto ambavyo Achebe alikuwa ameandika. Navikumbuka viwili: The Sacrificial Egg and Other Short Stories na Chike and the River . Shule yetu ilikuwa na maktaba kubwa na nzuri sana. Nidhamu ya kusoma ilikuwa kali, chini ya usimamizi wa mapadri waliokuwa waalimu wetu. Miaka ile ile, Achebe alichapisha riwaya ya No Longer at Ease na Arrow of God na A Man of the People . Tulikuwa tu

Toleo Jipya la "Kioo cha Lugha"

Image
Siku chache ziilizopita, nilipata nakala ya jarida la Kioo cha Lugha , kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mimi ni mwanakamati katika kamati ya uhariri wa jarida hilo. Ni furaha kubwa kwangu kushirikiana na wanataaluma wenzangu katika mambo ninayoyapenda. Masuala ya la lugha, fasihi, utamaduni, na falsafa yana nafasi ya pekee katika maisha yangu. Toleo hili la Kioo cha Lugha lina makala nyingi, kama inavyoonesha katika picha hii hapa kushoto. Wanaodhani kuwa ki-Swahili kina mapungufu katika kuelezea taaluma mbali mbali, watafakari upya suala hilo, hasa kwa kusoma machapisho kama yale yatokayo katika Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, ambayo ni ya taaluma mbali mbali. Niliwahi kugusia suala hilo katika ujumbe huu hapa .

Buriani, Chinua Achebe

Image
Msiba mzito umetufika leo, wasomaji wa fasihi na walimwengu kwa ujumla. Chinua Achebe amefariki, akiwa na umri wa miaka 82. Maarufu kama muasisi wa fasihi ya ki-Ingereza katika Afrika, Chinua Achebe ametoa mchango mkubwa katika uandishi, mchango ambao uliiweka Afrika mahala pazuri katika ramani ya fasihi ya dunia. Tangu alipochapisha riwaya yake maarufu, Things Fall Apart , hadi kufariki kwake, Achebe ameandika riwaya, hadithi fupi, na insha kuhusu fasihi, uandishi, siasa na utamaduni. Amefanya mahojiano mengi, ambayo, kwa bahati nzuri yanapatikana mtandaoni au katika vitabu na majarida. Achebe aliamini kwa dhati kuwa jukumu la msanii ni kuwa mwalimu wa jamii. Yeye mwenyewe amezingati wajibu huo tangu ujana wake, alipochapisha Things Fall Apart , hadi kurariki kwake. Amewafundisha waAfrika mengi kuhusu jamii yao, udhaifu na uwezo wao, na amewafundisha walimwengu kuwaona wa-Afrika kwa mtazamo tofauti na ule wa wakoloni. Amewafundisha walimwengu maana ya ubinadamu, ambayo inavuka m

Tamko la CCM Mkoa wa Vyuo Vikuu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Mkoa maalum wa vyuo vikuu, kanda ya Dar es salaam, umefanya kikao cha kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha Mkoa huo na Chama kwa ujumla. Pamoja na Ajenda hiyo, pia kikao hicho:- · Kimelaani vikali matukio ya kuvamiwa, kudhuru mwili na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa Dini na wanahabari. Mkoa umesikitishwa sana na tukio la kushambuliwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda. · Lakini pia, kimevitaka vyombo vya Dola kuwakamata, kuwashikilia na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliothibitika kuhusika na matukio ya namna hiyo bila kuangalia Itikadi za Kivyama, Cheo ama Kundi. Na pia kuyataka makundi ya kijamii, wanaharakati na wanasiasa kuacha kuingilia/kuvuruga kwa namna yeyote taratibu za kisheria na kiusalama. · Pia, kuwataka wanausalama kumhoji kwa kina Dr Slaa juu ya tuhuma zake dhidi ya Kurugenzi ya Usalama wa Taifa (TISS) na kumtaka kuthibit

Dunia Bila U-Islam

Image
Wiki hii nimenunua vitabu kadhaa. Kimojawapo ni A World without Islam , kilichotungwa na Graham E. Fuller. Na hiki ndicho kitabu ninachotaka kukiongelea hapa. Nilipokiona kitabu hiki katika duka la vitabu la hapa chuoni St. Olaf, nilivutiwa na jina la kitabu, nikajiwa na duku duku ya kufahamu ni kitabu cha aina gani, na kinaongelea nini. Dhana ya dunia isiyokuwa na u-Islam ilikuwa ngeni kwangu, kwa kuzingatia jinsi dunia ya leo ilivyo na jinsi u-Islam ulivyo na nguvu duniani. Dunia bila u-Islam ingekuwaje? Ninahisi kuwa hadi hapo, wewe msomaji nawe tayari umeshapata mawazo au hisia fulani. Kama wewe ni mu-Islam, labda umeshaanza kuhisi kuwa kitabu hiki kimeandikwa na adui wa u-Islam. Labda unahisi kuwa kitabu hiki ni mwendelezo wa vita vya Msalaba ("Crusades"). Labda unahisi kuwa ni njama za makafiri dhidi ya u-Islam. Na kama wewe ni mmoja wa wale wanaoitwa wa-Islam wenye msimamo mkali, labda tayari unatamani yafanyike maandamano kulaani kitabu hiki, kama yalivyofanyika m

CHADEMA: Taarifa kwa Vyombo vya Habari, Machi 14, 2013

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14 MACHI, 2013 Ndugu waandishi wa habari, Tumewaita hapa leo, ili kupitia kwenu tuweze kutoa taarifa inayohusu kukamatwa kwa mmoja wa viongozi wa chama chetu, Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, aliyekamatwa jana tarehe 13 Machi 2013, ofisini kwake makao makuu ya CHADEMA. Jeshi la polisi linasema limemkamata Lwakatare likimtuhumu kuhusika na mashambulio ya watu mbalimbali kutokana na ushahidi uliopo kwenye walioita, viedo ambayo pia imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwanza, tunapenda kuwaambia umma wa watanzania na watu wote duniani kwamba, CHADEMA hakina nia yoyote ya kuzuia polisi kutenda kazi zake, iwapo watakuwa wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Bali, tunachoeleza hapa ni jinsi polisi na vyombo vingine vya dola vinavyoshiriki katika kutengeneza paropaganda chafu dhidi ya CHADEMA za kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na unyama unaoendelea nchini wa kutesa watu, kupiga, kung’oa

Mabucha, Mto wa Mbu

Image
Nilipiga picha hii hapa kushoto kwenye mtaa mmoja wa Mto wa Mbu. Nilivutiwa na mwonekano huu: safu ya mabucha na pia akina mama wakiwa wamejitokeza tu hapo mlangoni  na kuelekea walikokuwa wanaelekea. Nilitafakari suala la haya mabucha, ila sikupata fursa ya kuongea na yeyote kuhusu suala hilo. Sikuweza kujua kama wenye mabucha hayo ni akina nani. Miezi mingi iliyopita, kulikuwa na taarifa za mgogoro Mto wa Mbu baina ya wa-Kristo na wa-Islam. Sikufuatilia undani wa tatizo, isipokuwa haikuwa taarifa njema, kwani migogoro si jambo jema. Taarifa hii ilinigusa kwa namna ya pekee kwa sababu nilishafika Mto wa Mbu mara kadhaa na nafahamiana na baadhi ya watu wa pale. Mimi kama mgeni nilikuwa na hisia kuwa Mto wa Mbu ni mji uliotulia sana. Sikutegemea mgogoro wa aina ile. Hayo yote yalinijia kichwani wakati napiga picha hii.

Maktaba ya Karatu

Image
Wadau wa blogu yangu hii watakuwa wanajua jinsi ninavyoleta taarifa za maktaba mbali mbali, hasa zile ninazopata fursa ya kuzitembelea. Mfano ni taarifa hii hapa . Mwaka huu, tarehe 7 Januari, nilipata fursa ya kuiona maktaba ya Karatu. Nilikuwa njiani kuelekea kwenye uwanja wa mnada , lakini papo hapo nilitaka kuiona maktaba. Kuna kibao nilikiona wakati natembea, kikielekeza iliko maktaba. Nilipofika hapo nilipiga tu hii picha, nikaendelea na safari yangu ya mnadani. Maktaba iko juu kwenye sehemu ya mwinuko ambao nadhani ndio juu kabisa pale Karatu. Sikuingia ndani. Nikifika tena Karatu, nitaweka kipaumbele kuingia humo na kuona ilivyo. 

Matokeo Zaidi ya Mhadhara wa Faribault

Image
 Nimeshaandika kuhusu mhadhara niliotoa mjini Faribault hivi karibuni na jinsi ulivyowagusa waliohudhuri, kama Mhadhiri Becky Davis alivyoelezea hapa . Mhadhiri huyu ameandika ujumbe mwingine kwenye blogu yake , akigusia tena mhadhara ule: ------------------------------------------------------------ African Folk Tales When Joseph Mbele visited our class last week, one of the things he talked about is how folk tales can be so very valuable in learning about a culture. He said that's a way to understand what's important and what a culture sees as valuable and moral.  It made me very happy that I had already planned to make (force?) each student in my Humanities of South Africa class to present a South African Folk Tale to the rest of the class. Joseph Mbele has a book of folk tales himself, which I am purchasing as soon as I get my next paycheck: These folk tales are from Tanzania, and I can't wait to read this. Since we're studying South Africa, howeve

Utalii wa Kiutamaduni Unakuza Uchumi Haraka

Image
Hapa ni ndani ya kituo cha utamaduni cha jiji la Arusha   Na Albano Midelo UTALII wa kiutamaduni bado ni nadharia changa katika nchi za ulimwengu wa tatu ikiwemo Tanzania,kutokana na ukweli kuwa katika nchi hizo wamezoea kuona utalii wa asili wa kutembelea mbuga za wanyama. Utalii wa kiutamaduni ni nadharia mpya hapa nchini ambapo serikali imeanza kuutambua utalii wa kiutamaduni na kuupa nguvu kubwa aina hiyo ya utalii miaka ya hivi karibuni,zamani vivutio vya utalii wa kiutamduni kama majengo ya kale,maeneo ya kihistoria na makumbusho hayakupewa mtazamo wa kiuchumi zaidi. Maeneo hayo yalipewa mtazamo wa kielimu zaidi na kuundwa idara za mambo ya kale na idara ya makumbusho ambazo zote awali zilikuwa katika wizara ya elimu na utamaduni ambavyo viliwekwa kama vyanzo vya elimu zaidi kuliko vyanzo vya utalii kwa sababu wakati ule  watalaamu walifanya tafiti mbalimbali za mambo ya kale wakiwemo wakina Dk.Leakey Hata hivyo baadaye kulikuwa na mabadiliko katika u

Mafanikio ya Mhadhara Wangu Faribault

Image
Nilishaleta taarifa kuhusu mhadhara niliotoa katika chuo cha South Central, Faribault. Mhadhara ulihusu kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Mhadhiri aliyekuwa mwenyeji wangu, Rebecca Fjelland Davis, ameandika taarifa ifuatayo katika blogu yake , akaambatisha pia uchambuzi wa kitabu aliouandika kwenye mtandao wa Goodreads : Joseph Mbele's book AFRICANS AND AMERICANS Our class, "Culture and History of South Africa,"  read Africans and Americans: Embracing Cultural Differences last week. The author, Joseph Mbele came to visit us on Tuesday. It was unanimously considered a DELIGHT. The book is a fast read, and Joseph Mbele writes in a conversational, welcoming style that sucks you right in, keeps you laughing, and keeps you reading.  In person, Joseph proved to be one of the most brilliant, funny, warm, and gentle human beings I've ever met. My students loved him; the two hours with him flew past. Africans a

Wazazi Wamefurahia Kijana Wao Kwenda Tanzania

Siku kadhaa zilizopita, niliandika ujumbe wa shukrani kwa mafanikio ya kozi niliyofundisha Tanzania mwezi Januari juu ya mwandishi Ernest Hemingway. Nilikuwa na wanafunzi 29 wa chuo cha St. Olaf . Leo nimepata ujumbe kutoka kwa wazazi wa mwanafunzi mmojawapo, ambao ninauleta hapa. Nimebadili jina la mwanafunzi, na ninamwita Kijana: Dear Professor Mbele -- We want to thank you so very much for all you have done for our son, Kijana! He absolutely loved the recent trip to Tanzania. We thank you for giving him the opportunity to experience the rich culture of your home country. Kijana came back a different person--a better person--for all he was able to experience. You have given him a very valuable gift. He also truly enjoyed learning about Hemingway. thank you again for taking Kijana and the other students on the adventure of a life time. We hope to meet you sometime!  Sincerely,  Father and Mother of Kijana. --------------------------------------------------------------------

Kimahama Literature Centre, Arusha

Image
Kati ya maduka ya vitabu yaliyoko Tanzania, kuna moja mjini Arusha liitwalo Kimahama Literature Centre. Sikumbuki ni lini nilianza kusikia jina la duka hili, ila nakumbuka kuwa miaka zaidi ya kumi iliyopita, uongozi wa duka hili ulinunua kutoka kwangu nakala za kitabu changu cha Matengo Folktales . Kama nakumbuka vizuri, walinunua nakala 20. Baadaye nilipata taarifa kuwa zote zimeuzwa. Siku nyingine, miaka michache iliyopita, nilijikuta tena ndani ya Kimahama Literature Centre kama ilivyo kawaida yangu, kutembelea maduka ya vitabu. Meneja alikuwa mpya. Katika maongezi, nilipomwambia kuwa nimechapisha kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , alinunua nakala kadhaa kutoka kwangu. Mwaka huu, niliona kitabu hiki kinauzwa hapo, nikapiga picha hiyo hapa kushoto. Kuwepo kwa kitabu hiki katika duka hili kuliwahi kuelezwa na mwanablogu Bwaya katika blogu yake . Hizi ndizo baadhi ya kumbukumbu zangu za duka hili. Kitu kimojawapo kilichonigusa ni kuona

Yatokanayo na Mhadhara Wangu Mjini Faribault

Image
Sikupenda kuelezea kirefu mafanikio ya mhadhara niliotoa katika chuo cha South Central , mjini Faribault kwa wanafunzi na maprofesa wanaojiandaa kwa safari ya Afrika Kusini. Niligusia tu kuwa mhadhara ulikuwa mzuri. Undani wa kilichotokea ni habari ambayo nataka niwaachie waliohudhuria waelezee.  Kwenye ukurasa wa Facebook , Profesa Becky Davis aliweka picha ambayo nimeiazima hapa, na pia aliandika hivi: Joseph Mbele spoke with us this morning. What a generous spirit, and what a delightful and humorous speaker!  Kwa upande wangu, mihadhara ya aina hii ninaitoa mara kwa mara, kwenye vyuo, taasisi na jumuia mbali mbali hapa Marekani. Msingi wake ni yale niliyoandika katika kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Mialiko hii inatoka zaidi kwa waMarekani ambao wanapangia safari ya Afrika au wanashughulika kwa namna mmoja au nyingine na waAfrika, iwe ni barani Afrika au hapa hapa Marekani. Watu hao, ambao ni wengi sana, wakishasoma kitabu hiki wanapata h