Posts

Showing posts from June, 2021

Hitimisho la Trade with Africa Business Summit 2021

Image
Video hii ni ya hitimisho la mkutano uliofanyika tangu Mei 31 hadi Juni 4, uitwao "Trade With Africa Business Summit." Nimeshautajataja mkutano huu hapa. Kila mtu alishukuru kwa kuhudhiria kutokana na elimu kubwa na pana iliyopatikana katika mihadhara na mijadala. Mwaandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri, alikuwa amenialika nikaongelee kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Kitabu kilitajwatajwa kwenye mkutano, hata katika video hii ya dakika za mwisho za mkutano. Mtoa mada Vera Moore, mmiliki wa kampuni ya Vera More Cosmetics, anaonekana mwishoni kabisa akiwa ameshika kitabu. Tulishangaa amekipataje upesi namna ile. Namshukuru Toyin kwa mwaliko wake. Ameniarifu kuwa ataendelea kunibebesha majukumu, nami niko tayari. Video zote za mkutano zinapatikana mtandaoni. Nikizingatia thamani ya elimu iliyomo, kulipia gharama iliyotajwa ni sawa na uwekezaji makini. Zinapatikana hapa: https://www.nazaru.trade/courses/5248326/content

Nina Wasomaji Butiama kwa Mwalimu Nyerere

Image
Sijawahi kufika Mwitongo, Butiama, lakini kitabu changu, ambacho ni kama nafsi yangu, kimefika. Pichani anaonekana mjukuu wa Mwalimu Nyerere akiwa anasoma kitabu hiki. Picha hii aliiweka mitandaoni akiwa ameambatisha ujumbe. Ninanukuu baadhi ya aliyosema. "My Dad gave me this book to read this morning, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences by Joseph Mbele. I just finished it. One lesson I learned is to respect, understand, and see the value in both cultures. I would highly recommend this book." .................. "My Dad gave me this book, he felt that it could be helpful for me, I’ve lived in the US since I was 7, I’ve made the decision to move back this year. There are many things which I still question. It will be a long learning process, this book has given me hope." .................. "Thank you for writing this book Professor Mbele. I’ve learned quite a lot from reading it but I’ve also grasped a better understanding of many things which

Ms. Vera Moore - Mdau Mpya wa Kitabu Changu

Image
Wiki hii nzima, nimekuwa nikihudhuria mkutano mkuu uitwao Trade With Africa Business Summit. Mkutano umejumlisha wafanya biashara, wanadiplomasia, na wajasiriamali, na wengine kutoka nchi mbali mbali. Mwandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri kutoka Nigeria, mjasiriamali na mhamasishaji wa biashara baina ya Afrika na Marekani, alikuwa amenialika kuongelea kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Alikipigia debe mkutanoni, na kilitajwa mara kwa mara. Mjumbe mmoja, Vera Moore, mfanyabiashara maarufu wa vipodozi, alitusisimua alipokuwa akiongea, kwa kutuonyesha nakala ya kitabu akisema ameshanunua. Nilishangaa alivyokinunua haraka namna ile. Nafurahi kuwa na mdau maarufu huyu. Wengine wanakuja.