Posts

Showing posts from August, 2013

Zawadi Baada ya Mhadhara Finland

Image
Bado nina mengi ya kusema kuhusu safari  yangu ya wiki iliyopita nchini Finland, kwenye mkutano. Nina kumbukumbu nyingi, na kama nilivyowahi kusema zamani, blogu yangu ni mahali ninapojiwekea mambo yangu binafsi. Kama nilivyotamka , nilialikwa kutoa mhadhara maalum, ambao hapa Marekani huitwa "keynote address." Mada yangu ilikuwa "The Epic as a Discourse on National Identity." Baada ya kutoa mhadhara, mtoa mhadhara alikuwa anakabidhiwa ua. Ua hilo ni shukrani ya waandaaji wa mkutano. Hapa kushoto anaonekana Profesa Pekka Hakamies, mwenyekiti wa kamati ya maandilizi, ambaye aliniletea mwaliko. Tulioalikwa kutoa hiyo mihadhara maalum tulikuwa watano, kila mtu akatoa mhadhara wake kwa wakati tofauti. Mhadhara wa aina hiyo hutolewa mbele ya washiriki wote wa mkutano, na unategemewa kuweka msingi au changamoto za kujadiliwa na washiriki katika vikao mbali mbali ambamo mada mbali mbali hutolewa. Katika kuhudhuria hivyo vikao vya baadaye, nilifurahi kuw

Ziara Yangu Finland Imefanikiwa Sana

Image
Tarehe 19 hadi 24 nilikuwa kwenye Chuo Kikuu cha Turku, Finland, kwenye mkutano wa kitaaluma. Nilialikwa nikatoe mmoja ya mihadhara maalum, "keynote address." Mhadhara wangu ulikuwa "The Epic as a Discourse on National Identity." Utafiti, ufundishaji na uandishi wangu kuanzia kwenye mwaka 1977 umekuwa zaidi kuhusu masimulizi kama yale ya Iliad, Odyssey, Dede Korkut, Sundiata, Liongo Fumo, Kilenzi, Beowulf, Gassire, Ibonia, na Kalevala. Anayeonekana pichani kulia, ni Profesa Pekka Hakamies, mwenyekiti wa jopo la maandalizi, aliyenialika. Washiriki walikuja kutoka pande mbali mbali za dunia. Hapa kushoto niko mbele ya kanisa moja, mjini Turku. Sikupata muda wa kuingia ndani, bali nilikuwa napita hapo nje kila nikiwa njiani baina ya hoteli nilyofikia na sehemu ya mkutano, mwendo wa dakika kama 15 kwa mguu. Jioni ya tarehe 23 nilialikwa Helsinki, kwa chakula cha jioni. Hapo nilikutana na wa-Tanzania kadhaa waliokuja kujumuika nami. Ukarimu wao

Nangojea Kukaguliwa "Eapoti"

Image
Wadau, wiki ijayo ninasafiri kwenda Finland, kwenye mkutano, nikitokea uwanja wa ndege wa Minneapolis. Sasa kuna haka kasuala ka waBongo kukaguliwa sana kwenye hivyo viwanja vya ndege. Nasubiri zamu yangu. Hii mijitu iliyotufikisha hapa imetuhujumu sana waBongo. Nasikia mingine ni mijitu mikubwa serikalini, na mingine eti ni mifanyabiashara. Biashara gani hii kama si uroho wa fisi, ujambazi, na uuaji? Hii mijitu imechangia kuathirika kwa afya na maisha ya wengi nchini, na kinachoudhi ni kuwa inaachwa iendelee kutanua na kufanya hujuma hizo. Haya ni baadhi ya matunda ya kuwa na CCM madarakani. Nchi hii iko mikononi mwa CCM. Nawapongeza wana-CCM na vikofia vyao, na magwanda yao ya kijani, kwa kutufikisha hapa tulipo. Miaka yote iliyopita, nilikuwa najivunia kuwa m-Tanzania, kutokana na kazi kubwa aliyofanya Mwalimu Nyerere. Ilikuwa ni heshima kuwaambia watu popote duniani kuwa mimi ni m-Tanzania. Miaka hii ya leo najisikia aibu kuwa m-Tanzania.

Afrifest 2013 Ilifana Minnesota

Image
Jana, mjini Brooklyn Park hapa Minnesota, yalifanyika maonesho ya Afrifest. Afrifest ni tamasha linalofanyika mara moja kwa mwaka, likiwajumuisha watu wenye Asili ya Afrika na wengine wowote wale, kwa lengo la kufahamiana, kujielimisha, na kujipatia burdani mbali mbali. Watu wa kila aina walishiriki, wazee, vijana, na watoto. Hapa kushoto tunawaona watoto wakiwa na mpiga ngoma maarufu hapa Minnesota. Aliwaonyesha namna ya kupiga ngoma, na pia aliwaelezea maana na matumizi ya ngoma katika tamaduni za Afrika. Watu walikuwa wameambiwa kuwa tamasha lilipangiwa kuanza saa sita mchana. Kuanzia hapo watu walikuwa wanafika, kwa wakati wao. Vijana kutoka benki ya Wells Fargo walifanya kazi nzuri ya kujitolea, kuwahudumia waliohudhuria. Walikuwa wamevalia tisheti nyekundu. Hapa ni banda ambapo watu walikuwa wanajipatia chakule. Wahusika wanajua sana kuandaa vyakula, kama vile wali na kuku. Siku nzima, kulikuwa na muziki kuto

Afrifest 2013, Minnesota

Image
Kesho, Agosti 10, ndio ile siku ya tamasha la Afrifest hapa Minnesota. Ni tamasha linalofanyika mara moja kwa mwaka, kwa lengo la kuwakutanisha watu wenye asili ya Afrika na wengine pia. Afrifest ni fursa ya kufahamiana, kuelimishana, na kuburudika na maonesho mbali mbali ya michezo na tamaduni. Kwa taarifa zaidi kuhusu tamasha la kesho, angalia tangazo nililobandika hapa. Pia soma nilivyoandika katika blogu yangu ya ki-Ingereza . Kama una watoto, na unakaa maeneo haya ya Twin Cities, jiulize watoto hao wana fursa zipi za kupanua mawazo ili wawe raia wa dunia ya utandawazi wa leo. Unawaandaa vipi waweza kuwa na uzoefu wa kufanya kazi na kushirikiana na watu wa mataifa na tamaduni mbali mbali. Ni wazi kuna vitu vikubwa ambavyo mzazi unaweza kufanya kwa lengo hilo. Lakini vile vile, kuna vitu kama haya matamasha ambayo yanachangia. Mimi kama mtafiti, mwalimu na mwandishi nahudhuria Afrifest kila mwaka. Napata fursa ya kufahamiana na watu, kukutana na wale ambao tunafahamiana, kuo

Mapendekezo ya Mwigulu Nchemba Kuhusu Ajira kwa Vijana

Image
Jana, kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mwigulu Nchemba ametoa mapendekezo kuhusu ajira, ambayo anasema atayawasilisha Bungeni kama hoja binafsi : Habari vijana wenzangu, Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA. HINTS, 1) Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi. Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI; (A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI (B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja (C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA H

Tundu Lissu: Pigeni Kelele Kuokoa Watanzania

Image
Lissu: Pigeni kelele kuokoa Watanzania Penulis : mtandao-net on Saturday, August 3, 2013 | 10:09 PM CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeutaka umoja wa vijana wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IYDU) kupiga kelele kote duniani ili kuwanusuru Watanzania wanaouawa hovyo kwa sababu za tofauti za siasa hapa nchini. Akizungumza na uongozi wa umoja huo (IYDU) jijini Dar es Salaam wiki hii, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu alisema ni wakati wa vijana kuwaokoa wenzao wa Tanzania ambao kujiunga kwao na siasa kumesababisha wachukiwe na watawala. “Watu wanauawa hadharani na hakuna hatua zinazochukuliwa…nendeni katika nchi zenu katika mabunge yenu mkapige kelele katika haya yanayotokea Tanzania; inaweza kusaidia na mkawa mmewasaidia Watanzania,” alisema Lissu. Tundu Lissu alisema viongozi wengi wamekamatwa na kufunguliwa kesi nyingi mahakamani, na hivyo kuifanya CHADEMA kuwa katika wakati mgumu kuliko mwingine wowote katika uendeshaji wa siasa za vyama vingi