Jana, kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mwigulu Nchemba ametoa mapendekezo kuhusu ajira, ambayo anasema atayawasilisha Bungeni kama hoja binafsi:
Habari vijana wenzangu, Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA. 
 
 HINTS,
 1) Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara,
 mikoa, halmashauri-  serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. 
Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi. 
Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI;
 
 (A) KILA OFISI 
ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA 
UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI
 (B) KUNA WATU
 WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA 
ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA  UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO 
HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja 
 (C) KUNA WATU wanapewa ajira za 
mikataba na  WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA HAKUNA MTU ANAYEWEZA 
KUZIBA NAFASI HIYO au hakuna mwenye uzoefu.
 
 KWA UPANDE WA PILI SASA WA WAHITIMU;
 
 (1) KILA MTAA KUNA KIJANA AU VIJANA WAHITIMU WANA MIAKA 2 HADI 5 HAWANA
 KAZI WANAZUNGUKA NA BAHASHA MPAKA SOLI ZA VIATU ZINAKWENDA UPANDE
 
(2) KILA MTAA VIJANA WAPO WAKIOMBA KAZI WANAAMBIWA HAWANA UZOEFU wa 2 or
 3 yrs, Au anayetakiwa awe na 4yrs experience hata katika ngazi za ofisa
 wa ngazi za kuanzia ilihali hakuna chuo kinafundisha uzoefu
 (3) 
Vijana wapo na diploma hawajulikani walipo kwa Serikali na wamekaa miaka
 2 hadi 5 na diploma zao wanasubiri kazi. kipindi ambacho angewezeshwa 
kwenda shule angeshavuka diploma na degree angekuwa hata na master.
 
 Kufuatia hali hii 
 (i) vijana wanaitwa bomu ili hali VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA
 (ii)  Vijana wana stress, wamekata tamaa hawaoni future na wengine wanahasira sana
 (iii) Vijana wahitimu wanatunzwa na wazee ambao hawakwenda shule hivyo kuwa mzigo kwa wazazi.
 
 Lengo ni kuitaka serikali ikishajua idadi ya wahitimu na ikama yake cos
 ofisi ziko wazi mlioko ofisini mkisema ukweli msiogope mabosi wenu 
mtakiri hili
 
 (1) Serikali ifanye re allocation ya vijana kwenye nafasi za kazi kufuatana na ujuzi wao,
 (2) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu 
maofisini na hata kuwalipa half a saraly of a full employed officer ili 
kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu kwa kijana aombapo kazi.
  (3) Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata half a saraly ili wapate uzoefu
 (4) Uwezo wa kazi na marks za kwenye vyeti ni vitu viwili tofauti, 
serikali ikiwa attach ofisini vijana itajua uwezo wao itaacha kuongezea 
wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi 
hiyo
 (5) Serikali ibane matumizi yake ili itenge fedha ya kuendeleza
 wahitimu. Mtu mwenye diploma kusubiri kazi miaka 5 ni kipindi angeweza 
kuwa na degree na masters yake.
  Baadhi sehemu za kukata matumizi ya
 serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye magari na mafuta ya 
magari. Unakuta bosi anakaa bunju halafu dreva gongolamboto halafu ofisi
 posta, au bosi kiluvya dreva mbagala ofisi posta kila siku trip hizo, 
pia training nje ya nchi kwa mtu mwenye 59yrs nakutumia milions and 
milions zisitishwe ili tuandae generetion ya kupokea majukumu.
 Pia 
serikali ikishajua waliopo pia iandae projection ya tunakoelekea in 
three to five yrs hali itakuwaje na serikali inampango gani. Cos maisha 
bora yanaletwa na KAZI.
 SERIKALI IKISHAJUA IWEKE BAJETI AMA YA 
GUARANTEE AU YA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYO  LABOUR INTENSIVE ili 
kuchukua vijana wahitimu na wa mtaani. SENSA HII SIO GHARAMA NI 
KUWATANGAZIA TU WAHITIMU WAKAJIANDIKISHE KTK OFC ILIOKARIBU AU KUPELEKA 
CV kwa DC the cv zinachambuliwa.
 
  This is a rough idear. You can add or improve. 
 
 VIjanaaaaaaaa, itikieni NGUVU KAZI YA TAIFA
********************************************************************
Nami nimemjibu katika ukurasa huo huo wa Facebook kama ifuatavyo:
Kwanza
 kabisa, andika ki-Swahili ipasavyo, sio kuchanganya na maneno ya 
ki-Ingereza, kama ufanyavyo. Tunapaswa kuonyesha kuwa tunaiheshimu lugha
 yetu. Kiswahili kinajitosheleza, sawa na lugha zingine. Lugha ni kioo 
cha nafsi na upekee wa jamii au taifa. Kuiheshimu lugha ni dalili ya kujiheshimu.
Hasa
 kwa mtu anayehesabiwa kuwa ni kiongozi, sherti kuonyesha mfano katika 
hili. Kama kiongozi unashindwa kuonyesha heshima kwa lugha yetu, 
unashindwa kuonyesha heshima wa utambulisho huu wa Taifa letu, ni 
kiongozi gani, na unawafundisha nini watoto wetu?
Ujumbe
 wako kuhusu ajira unapwaya sana. Hujaweka suala hili katika mkabala 
wowote, wala hujalifanyia utangulizi unaoonyesha kuwa unaelewa historia 
na upana wa suala hili. Hata dhana yenyewe ya ajira unayotumia ni finyu.
 Papo hapo unadai kuwa umefanya utafiti. Ni ajabu.
Hujazingatia
 tulikotoka, kwa Mwalimu Nyerere, ambaye aliongelea masuala haya ya 
ajira. Aliongelea masuala ya elimu kwa vijana, akisisitiza kuwa tuwape 
elimu ya kujitegemea. Inaonekana hujasoma lolote kuhusu mawazo ya 
Mwalimu Nyerere juu ya suala hili la elimu ya kujitegemea. 
Ungefanya
 utafiti kuhusu kinchoendelea duniani, angalau ungegundua kuwa katika 
dunia ya leo, watu huongelea umuhimu wa kutoa elimu kwa vijana kwa lengo
 la kuwawezesha kujiajiri, kujitengenezea ajira.
Hilo
 hujataja, na haionekani unalifahamu. Wewe unaongelea ajira serikalini. 
Dhana hiyo, ingawa ilikuwa na mantiki kubwa miaka ya zamani, inapitwa na
 wakati. Na wewe kama kiongozi, ulipaswa utambue hilo, ili uweze kutoa 
ushauri mwafaka kwa hao vijana.
Unajiita
 kijana, lakini mawazo yako ni yale yaliyokuwa yanakubalika karne 
iliyopita, sio mawazo ya karne ya 21. Katika karne ya 21 kuwajengea 
vijana dhana kuwa waelekeze nguvu katika kutafuta ajira serikalini ni 
upotoshaji. Hii dhana kwamba Tanzania inahitaji viongozi vijana ni 
upuuzi, kama vijana wenyewe ni akina Mwigulu Nchemba. Hawafai kuongoza, 
kwa sababu hawajui dunia ikoje na inakwenda wapi.
Ingekuwa
 Mwigulu Nchemba unajua dunia ya leo ikoje na inakwenda wapi, kuhusu 
hili suala la ajira, ungefahamu kuwa sekta inayokuwa kwa kasi kuliko 
zote hapa duniani ni utalii. Hujataja jambo hilo, ambalo liko wazi 
miongoni mwa wote wanaofuatilia maendeleo ya uchumi na ajira katika 
karne hii. 
Sekta
 ya utalii ndio inayokua kwa kasi kuliko zote, na ndio inayoleta 
matumaini ya kutoa ajira nyingi kuliko hiyo serikali ambayo ndio msingi 
wa mapendekezo yako. 
Kama
 mtu unataka kutoa mchango katika suala la ajira kwa vijana, ni muhimu 
sana kuwafungua macho kuhusu sekta hii ya utalii, na jinsi ya wao 
kujiandaana kujipanga kunufaika na sekta hii.
Sisemi
 kuwa suala la ajira serikalini lisahauliwe. Lakini ninachosema ni kuwa 
tuwe na upeo mpana, upeo wa kuelewa hali halisi ya dunia ya leo. Tuwe 
pia watu ambao tumesoma yale aliyosema Mwalimu Nyerere kuhusu elimu ya 
kujitegemea.
Mwigulu
 ukiwa ni katibu mwenezi, nilitegemea unaeneza mawazo thabiti ya 
kuliendeleza Taifa. Lakini naona unaeneza mawazo rejareja, baadhi yakiwa
 yamepitwa na wakati. Mtu kama wewe hufai kuwa kiongozi. Wala usije 
ukadhani mimi ni CHADEMA. Mimi ni raia ambaye si mwanachama wa chama 
chochote cha siasa, ila nawashuhudia CCM mnavyojikanyaga. 
Ninapenda
 kusema neno moja zaidi kuhusu Nyerere. CCM mmemsaliti Mwalimu Nyerere. 
Yeyote anayesoma "Azimio la Arusha" na maandishi mengine ataliona hilo. 
CCM ni chama kinachohujumu mapinduzi aliyoyawazia Mwalimu Nyerere.
Ungemsoma
 Mwalimu Nyerere, ungefahamu kuwa alikuwa anakazana sana kuleta 
mapinduzi vijinini, ili kuwe na fursa za kiuchumi na ajira, na hivi 
kupunguza ndoto ya vijana kuhamia mijini. Wewe andiko lako lote kuhusu 
ajira unawaelekeza vijana waende katika ajira za serikali. Ni kuwavutia 
waende mijini. Hujasema lolote kuhusu kuboresha maisha ya vijijini, 
uchumi wa vijijini, na ajira huko huko vijijini.
Kwa
 kumalizia, ningependa kujua iwapo Mwigulu Nchemba unasoma vitabu 
vyovyote. Ningependa kujua kama una vitabu nyumbani kwako. Ningependa 
kujua iwapo tangu mwaka huu uanze hadi leo, umesoma vitabu vingapi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
- 
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
 - 
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
 - 
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
 

1 comment:
Prof, umesema ukweli japo anaweza kuna na nia na wazo zuri. Ni afadhali ameamua kuiainisha mapema hii hoja ili akiweza aiboreshe. Hoja hii inaonesha uanika uwezo mdogo wa uwelewa Mwingulu. Sasa tunapata majibu ya michango yake bungeni.
Hili ni janga.
Post a Comment