Posts

Showing posts from July, 2021

Utamaduni wa waCheki

Image
Tarehe 10 Julai, katika tamasha liitwalo International Festival Faribault, nilipata fursa ya kutembelea banda la jumuia iitwayo Czech Heritage Club, yaani klabu ya urithi wa waCheki, yaani watu wenye asili ya Czechoslovakia. Tuliongea, wakaniambia kuwa kuna maonesho ("exhibition") ya utamaduni wa waCheki mjini Montgomery. Wakanipa jina la makumbusho ambako maonesho yamewekwa, na kwamba yatakuwepo hadi Septemba mwanzoni. Niliwaambia kuwa mimi ni mtafiti katika "folklore" na utamaduni kwa ujumla, na kwamba lazima nitaenda kuangalia maonesho. Jana, tarehe 17, nilienda Montgomery, nikapata fursa ya kuangalia hifadhi. Ina mambo mengi sana ya historia na utamaduni. Nilipiga nyingi. Hapa naleta baadhi.

Tamasha la Kimataifa Faribault, Minnesota

Image
Tarehe 10 Julai, 2021, nilishitiki International Festival Faribault , tamasha linaloandaliwa na Faribault Diversity Coalition  mara moja kwa mwaka. Safari hii, nilimwalika Bukola Oriola, mwenye asili ya Nigeria, na mwanae Samuel Jacobs kuwa nami kwenye meza yangu na vitabu vyao. Niliwahi kuwa mwanabodi wa Faribault Diversity Coalition  na nimeshiriki tamasha mara nyingi. Wanakuwepo watu kutoka mataifa mbali mbali. Bendera za nchi zao zinapepea hapa uwanjani siku nzima. Katika ratiba ya tamasha, kunakuwepo muda wa watu kuandamana wakiwa na bendera zao kuelekea jukwaa kuu, na hapo kila mmoja hupata fursa ya kuelezea kifupi  bendera na nchi husika.  

Jirani Yangu, Msomaji Wangu

Image
Pichani katikati ni mama Merrilyn McElderry , na kushoto ni mjukuu wake. Nilijipiga picha hii nao juzi, tarehe 3 Juni, mjini Edina, jimbo la Minnesota. Merrilyn ni mwalimu mstaafu, msomaji makini wa maandishi yangu. Anayapenda na anafuatilia kwa karibu shughuli zangu kuhusiana na hadithi na mihadhara. Aliposoma kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , aliandika dondoo za kusisimua akifananisha utamaduni wa waAfrika na ule wa Wahindi Wekundu. Aliweza kufanya hivyo kirahisi kwa kuwa alishafanya kazi miaka 15 katika eneo wanamoishi waChippewa. Baraka iliyoje kwangu kuwa na wadau wa aina yake.