Posts

Showing posts from 2020

UNAWAFAHAMU WAMAREKANI?

Image

Hata Balozi wa Japani Kalalamikia Uchaguzi wa Tanzania

Image
Ule unaoitwa uchaguzi ambao ulifanyika Tanzania tarehe 28 mwezi Oktoba umelalamikiwa sana ndani na nje ya nchi. Kilichonishtua zaidi ni kuwa hata Balozi wa Japani nchini Tanzania amelalamika, kwa tamko hili: I am troubled by the information of widespread irregularities and wrongdoings during the recent election process in this country. I am convinced that sound democracy based upon multiparty system works best to contribute to further development and prosperity of Tanzania. (GOTO Shinichi, Ambassador of Japan to Tanzania) Ziko nchi, kama vile Marekani, ambazo tamaduni zao hazina utata juu ya kukosoa, kulalamika, na hata kukemea. Lakini Japan haina jadi hiyo, kwa misingi ya utamaduni wao ambao umejengeka katika dhana kama "saving face." Ukilalamikiwa na Japani, lazima ujitafakari sana, na hapa ndipo mamlaka za Tanzania zimekwama. Niliwahi kutamka katika ukurasa wangu wa Facebook kuwa mimi kama mtafiti wa tofauti za tamaduni nililichukulia tamko la balozi wa Japani kwa uzito wa

Miji Alimoishi Shaaban Robert: Hazina ya Taifa

Image

Kitabu Kujadiliwa Chuoni St. Olaf

Image
Tarehe 8 Januari, kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitajadiliwa katika semina ya maprofesa wa chuo cha St. Olaf Nitaendesha hiyo semina ili kuleta mitazamo mipya juu ya migogoro ambayo waMarekani wana jadi ya kuijadili kama matokeo ya ubaguzi wa rangi. Suala la tofauti za tamaduni hawaliwazii. Semina yangu italenga kuleta dhana hiyo. Semina hii ni moja ya semina zinazoendeshwa kwa ufadhili wa Institute for Freedom and Community hapa chuoni. Kwa kawaida, semina hizi zinahusu mada za kitaaluma. Lakini hii semina yangu inahusu mahusiano ya watu ya kila siku, bila kupotelea kwenye mawingu ya nadharia. Profesa moja mstaafu, maarufu katika taaluma ya falsafa, baada ya kukisoma kitabu changu aliniambia kuwa tunahitaji kitabu cha aina hii. Hii ni fursa ya kukitaambulisha kitabu changu rasmi hapa chuoni, ingawa kuna watu ambao wamekuwa wakikisoma.

Alex Trebek wa "Jeopardy" Afariki

Image
Alex Trebek, mwendeshaji wa kipindi cha televisheni cha "Jeopardy" amefariki, akiwa na miaka 80.  Kwa hapa Marekani, "Jeopardy" ni kipindi maarufu sana, ila mimi sikuwa najua. Nilikuja kuzinduka tarehe 23 Novemba, 2017. Kumbe siku hiyo Trebek alikitaja kitabu changu Matengo Folktales  katika kipindi chake. Watu mbali mbali walioshuhudia walianza kupeana na taarifa na mimi nikazipata. Pongezi zilifika kwa wingi, na ndipo nami nikafahaamu maana ya kutajwa kwenye kipindi hicho.

SHAABAN ROBERT: MWALIMU WETU

Image

Tamasha la Kimataifa Faribault, Minnesota

Image
Jana, tarehe 10, nilishiriki tamasha la kimatafifa mjini Faribault, Minnesota. Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na Faribault Diversity Coalition. Miaka iliyopita, nilikuwa mjumbe wa bodi wa hiyo Coalition. Tamasha hujumuisha maonesho ya tamaduni za watu wa mataifa mbali mbali waishio Faribault na maeneo ya jirani. Nimeshiriki tamasha hili Miaka iliyopita, na daima, inakuwa ni fursa nzuri ya kukutana na watu na kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu mambo mbali mbali ya dunia yetu ya utandawazi wa leo. Ninashiriki kama mwandishi na mtoa ushauri katika masuala ya taamaduni. Ninaonesha vitabu vyangu. Hii jana nilionesha pia vitabu via Bukola Oriola na mtoto wake wa miaka kumi na tatu Samuel Jacobs.

Kitabu Chawasili Nairobi

Image
Nakala za kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , zimewasili Nairobi. Simu namba 722 250 644.

Tundu Lissu, Serikali ya CCM, na Ushoga

Kwa kuzingatia kuwa kuna upotoshaji mwingi kuhusu msimamo wa Tundu Lissu juu ya ushoga, napenda kusema kuwa msimamo wake unafanana na msimamo wa serikali ya CCM kuhusu ushoga. Katika mahojiano kwenye kipindi cha "Hard Talk," yaliyotumia lugha ya kiIngereza, ambacho waTanzania wengi hawakijui, Tundu Lissu aliulizwa msimamo atakaochukua kuhusu ushoga endapo atakuwa na mamlaka. Alijibu kuwa hatajishughulisha na kupekua nini kinaendelea vyumbani mwa watu. Alimaanisha ataheshimu haki ya "privacy." Ikumbukwe kuwa haki hiyo imo katika katiba ya Tanzania pia. Kwa upande wa serikali, baada ya kushambuliwa sana kutoka ndani na nje ya nchi kufuatia kauli za Makonda, wizara ya mambo ya nje ilitoa ufafanuzi kwamba kauli za Makonda si msimamo wa serikali ya Tanzania. Wizara ilisema kuwa Tanzania inaheshimu mikataba yote ya kimataifa iliyosaini juu ya haki za binadamu. Tamko hilo lilitosha kuzimisha mashambulizi. Nami nilitamka na bado ninatamka kuwa serikali ilifanya busara kutoa

Duka Jipya la Vitabu Vyangu

Image
Vitabu vyangu viwili, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences  na Matengo Folktales  sasa vinapatikana katika duka la taasisi iitwayo  Planting People Growing Justice . Mwanzilishi na mwendeshaji wa taasisi hiyo, Dr. Artika Tyner, ni profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha St. Thomas  hapa Minnesota. Aliniuliza iwapo nitaridhia vitabu vyangu kuuzwa na taasisi hiyo. Alianza kukifahamu kitabu changu mwaka juzi, baada ya kununua nakala kadhaa kwa ajili ya watu aliowapeleka Ghana katika safari ya kielimu akishirikiana na Monica Habia,  mwanazuoni mwenzake kutoka Ghana. Baada ya safari hiyo, Monica alinielezea jinsi kitabu kilivyowasaidia waMarekani kuyaelewa mambo waliyokutana nayo Ghana. Unaweza kutembelea tovuti ya Planting People Growing Justice . Vitabu hivi viwili vinapatikana Tanzania, katika maduka ya Soma Book Cafe  na  A Novel Idea .

Kitabu Muhimu kwa Wageni Marekani

Image
Tarehe 11 mwezi huu, nilipata ujumbe kutoka kwa jamaa aishiye eneo la kati la jimbo hili la Minnesota. Anasema kuwa wana jumuia yao ambayo inawakaribisha na kuwasaidia wahamiaji na wakimbizi kimaisha.  Anasema kuwa wanatumia kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , na wanakiona ni bora sana kwa malengo yao. Kauli kama hizi si ngeni kwangu. Nimezisikia tangu mwaka 2005 nilipochapisha kitabu. Sehemu ya ujumbe ni hii hapa: I  have been involved with a local organization in St. Joe that works to help refugees and immigrants adjust to and succeed in central Minnesota. Our group is called Cultural Bridges.  I have been sharing your book, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, with members of our group. Everyone who has read it has really enjoyed it and we see it as an excellent resource as we work to fulfill our mission as an organization.

Yatokanayo na Picha ya Msomaji Nami

Image
Picha hii ilipigwa tarehe 27 Julai, 2019, Soma Book Cafe, Dar es Salaam. Wadau wa vitabu, yaani waandishi, wachapishaji, wauzaji, na wasomaji wa vitabu, tulikusanyika kuongelea masuala yanayotuunganisha. Huyu ninayeonekana naye pichani ni Chiombola Joseph ambaye nilimfahamu siku hiyo. Nilikuwa nimetoa mhadhara kuhusu "Writing About Americans," naye akawa mmoja wa wale walionunua vitabu vyangu vilivyokuwa vikiuzwa na Soma Book Cafe. Napenda kusema neno juu ya hilo na mengine yatokanayo. Uamuzi wa kununua kitabu si wa kawaida na si rahisi katika jamii yetu waTanzania. Huyu ndugu alinunua viwili. Sikumbuki wanauzaje, lakini lazima nusu laki au zaidi ilimtoka. Zingatia kuwa vitabu vyangu si udaku na haviko katika orodha ya vitabu vinavyofundshwa mashuleni na vyuoni nchini. Anayeamua kununua vitabu vyangu Tanzania ninamwona kama mtu wa pekee. Najiuliza, ni nini kinachomtuma kufanya hivyo? Bila shaka ni hamu tu ya kutaka kujua mambo. Mimi mwenyewe niko hivyo. Sichoki kununua

Sasa Nimesoma "The Comedy of Errors" (Shakespeare)

Image
Jana nilimaliza kusoma "The Comedy of Errors," tamthilia mojawapo ya Shakespeare, ambaye alliandika tamthilia 37, na labda zaidi kidogo. Katika ulimwengu wa fasihi, Shakespeare ni kinara. Wanafasihi wanaweza kuhoji kwa nini ninatumia neno fasihi kuziongelea tamthilia. Malumbano huenda yasiishe. "The Comedy of Errors" ni tamthilia inayoelezea matatizo na mikanganyiko itokanayo na uwepo wa watu kadhaa katika jamii ambao wanafanana maumbile na sura kiasi kwamba ukikutana na mmoja, halafu baadaye ukakutane na mwingine, hutajua hata kidogo kuwa ni mwingine. Tamthilia hii inaonyesha migogoro, kutoelewana, na magomvi kwa sababu hiyo. Kusoma maandishi ya Shakespeare kunahitaji mwendo wa taratibu. KiIngereza chake ni cha zamani, miaka mia tano iliyopita, na utamaduni ni vile vile. Ni chemsha bongo kwa sisi watu wa leo, sawa na kusoma tungo za zamani za kiSwahili kama vile "Al Inkishafi" au "Utenzi wa Rasi 'lGhuli." Kwa mtazamo wangu, chemsha bongo

Tunasoma Fasihi ya Afrika

Image
Baada ya muhula wa masomo kwisha hapa chuoni St. Olaf, mwezi Mei, sasa ninafundisha kozi maalum ya fasihi ya Afrika. Kwa miaka, nimefundisha kozi hiyo. Ni fursa kwa watu kuufahamu mchango wa waAfrika katika kutafakari masuala ya maisha ya binadamu (kwa maana ya kifalsafa ya "the human experience" na "the human condition") kwa njia ya fasihi. Ninapofundisha fasihi ya Afrika, ninaanza kwa kuielezea Afrika kama chimbuko la binadamu, tekinolojia, lugha, fasihi, falsafa, na yengine yite ambayo binadamu anahusika nayo. Safari hii ninafundisha Changes: A Love Story , Maru , Season of Migration to the North , na Woman of the Ashes. Nimesoma baadhi ya vitabu vya waandishi wote wanne na caribou vyote nilivyovisoma nilivbsoma katika kufundisha. Naweza kusema ninafahamu zaidi kazi za Ama Ata Aidoo na Mia Couto. Hata hivyo, vitabu hivi ninavyofundisha sikuwahi kuvisoma. Kila mara ninapofundisha kozi hii, au nyingine yoyote ya fasihi, nina jadi hiyo ya kufundisha angalau baadhi y

Utalii Tata

Image

Utalii wa Utamaduni Wilayani Kwetu

Image
Kwa miaka na miaka nimekuwa nikiongelea masuala ya utamaduni na utandawazi pia utamaduni na utalii au utili wa utamaduni.  Nimewahi kuhusisha vitabu na utalii. Nimesema kuwa watalii wengi kutoka huku ughaibuni, kama vile Marekani, hupenda kusoma vitabu, na sisi tutahitaji kuwa na maduka ya vitabu. Napenda kujielekeza wilayani kwetu: wilaya ya Mbinga, lakini Nyasa pia. Tunatakiwa kuandika vitabu kuhusu historia, utamaduni, na mambo mengine ya kwetu. Watalii wakija, wakute maduka ya vitabu, vitabu kuhusu historia ya miji kama Mbambabay, Liuli, Lituhi, Mbinga, Kigonsera na kadhalika pia taasisi kama hospitali ya Litembo. Wakute vitabu kuhusu vivutio kama jiwe la Mbuji. Tuwe na hifadhi ya vitu mbali mbali vya kitamaduni, kama vile mitumbwi, nyavu za kuvulia samaki, ala za muziki, kama vile ngoma, "ngwaja," "sekatela," "mapenenga," na "nkwendakwenda." Katika jumba la hifadhi, ziwepo video za ngoma, na masimulizi ya hadithi. Ziwepo picha za vivuti

Utalii na Utamaduni

Image

Mhadhara Wangu wa Kwanza Kwa Zoom

Tarehe 28 mwezi huu, nilitoa mhadhara kwa wanachuo wa chuoni St. Olaf na wasikilizaji walikuwa Mankato. Mada ilikuwa Understanding Each Other: Brothers and Sisters From Two Continents . Nimeshahutubia wanachuo wa South Central College mara kadhaa, na ninafurahi kuwa wanaendelea kuwa na hamu ya kunisikiliza, kama inavyoelezwa hapa . Kivutio kimojawapo ni kitabu changu Hii tarehe 28 ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuhutubia kwa kutumia Zoom. Changamoto ya kuhutubia bila kuiona hadhira kiuhalisia haikosi kuathiri mhadhara. Lakini ripoti nilizopata kutoka kwa mratibu wa mhadhara ni kwamba watt waliufurahia mhadhara wangu, ambao ni huu hapa .

Ninaupenda Ualimu

Image
Ndoto yangu tangu ujana wangu ilikuwa ni kuwa mwalimu. Nilihitimu chuo kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1976, nikateuliwa kuanza kufundisha pale, katika idara ya "Literature." Ndoto yangu ikawa imetimia. Ninaipenda kazi yangu na ninawapenda wanafunzi wangu.  Tangu mwaka 1991, ninafundisha katika idara ya kiIngereza hapa katika chuo cha St. Olaf, jimbo la Minnesota. Naleta picha kutoka miaka michache iliyopita nikiwa na wanafunzi wangu wa somo la kuandika kiIn gereza. Hili ni moja kati ya masomo ninayofundisha. Inapendeza kuwasaidia wanafunzi kujifunza matumizi ya lugha rasmi kwa nidhamu na usahihi kabisa. Lugha ina mitego na changamoto nyingi. Tuchukulie mfano wa mwanafunzi wa kubuniwa ambaye jina lake ni Mark. Tuchukulie kuwa Mark ameandika, "The reason why I spoke that way was because I was not feeling well."  Hapa Marekani, jamii ambayo kiIngereza ni lugha mama yao, watu wengi huandika kwa kiwango hicho, na wengi hawafikii kiwango hicho, kwani hutumia ma

Vitabu Nilivyonunua Leo

Image
Ni muda mrefu umepita, nami sijaandika kuhusu vitabu nilivyonunua kama nilivyokuwa naandika miezi iliyopita. Leo nimeona nifanye hivyo. Nilienda Apple Valley kukutana na mkurugenzi wa African Travel Seminars ambaye tunafanya shughuli za kutangaza utalii Afrika. Baada ya kikao, nilienda katika duka la Half Price Books , ambalo nimelitembelea mara nyingi. Kama kawaida, nilikwenda kwanza kuona vitabu vya Hemingway. Nilichagua  Paris Without End: The True Story of Hemingwahy's First Wife na Ernest Hemingway: Artifacts From a Life . Nilichagua Paris Without End kwa sababu nilitaka kujua zaidi juu ya Hadley Richardson, mke wa kwanza wa Hemingway. Nimesoma habari zake hapa na pale, lakini si kwa undani. Ninafahamu jinsi anavyoelezwa na Hemingway katika riwaya ya A Moveable Feast .  Vile vile niliguswa sana na barua alizoandika Hemingway kwa mke wake huyo pale alipokuwa ameanzisha uhusiano na mwanamke mwingine, Pauline. Hemingway anaelezea namna alivyosongwa na mawazo kuhusu tatizo

Sherehe ya African Travel Seminars

Image
Juzi tarehe 22, Ilifanyika sherehe mjini Minneapolis ya kutimiza miaka 24 ya kampuni ya African Travel Seminars. Niliwahi kuandika taarifa katika blogu hii.  Waalikwa walikuwa watu waliowahi kusafiri na kampuni hii ya utalii ambayo hupeleka watu kwenye nchi kama vile Ghana, Senegal, Gambia, Morocco, Misri, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Afrika Kusini, Cuba na na Brazil. Walialikwa pia marafiki wa kampuni.  Nilipata fursa ya kusema machache, nikaongelea utalii kama nyenzo ya elimu na ujenzi wa mahusiano baina ya mataifa na tamaduni. Mmiliki na mkurugenzi wa African Travel Seminars, Georgina Lorencz, aliniagiza nipeleke nakala za kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , ambacho siku za karibuni ameanza kukipendekeza kwa wadau naowapeleka Afrika. Nilipeleka pia nakala za Matengo Folktales kuwa kuwa nilijua kuwa katika hotuba yangu ningetaja umuhimu wa kuelewa misingi ya utamaduni na falsafa ya wahenga wetu wa Afrika. Kulikuwa pia na vyakula vha kiAfrika.

Mwaliko wa African Travel Seminars

Image
Nimepata mwaliko kutoka African Travel Seminars wa kushiriki shughuli itakayofanyika tarehe 22 Februari. Mada siku hiyo itakuwa "Celebrating Black Culture Through Travel." Kutakuwa na chakula, maonesho na michezo mbali mbali kuhusu Afrika. Nimealikwa kuongelea kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , ambacho African Travel Seminars hutumia kwa watalii wanaoenda Afrika. African Travel Seminars inaelimisha na kujenga mahusiano baina ya watu kupitia utalii. Hivi karibuni, tumeamua kushirikiana. Malengo ya kampuni hiyo yanafanana kwa namna fulani na ya kampuni yangu ndogo ninayojaribu kuikuza iitwayo Africonexion: Cultural Consultants.

Utamaduni na Utandawazi

Image

Kitabu Kimeingia Kwenye Maktaba ya Peace Corps

Image
Kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kimeingia kwenye maktaba ya Peace Corps iliyoko Washington DC. Mkurugenzi ameniandikia, na sehemu ya ujumbe ni hii: We will add it to the Peace Corps library where our staff and visitors can enjoy it. I look forward to reading more of it as I find the topic to be very relevant and important to our work. I have already begun reading it, and it has reminded me of my own experiences in Togo, West Africa. As I was reading, I was struck by the section on eye contact. I really love the verses you included from the poem by Sufi poet Ibn ‘Arabi about the veiled woman and eye contact, and I got a good chuckle at your stories of misunderstandings—as I, as well surely all of us, have had many such experiences and misunderstandings. Kauli za mkurugenzi za kukumbuka aliyoona Afrika na kufananisha na yaliyomo kitabuni, zinafanana na kauli za waMarekani wengine waliosoma kitabu hiki baada ya kuishi Afrika. Afrika kwenyewe