Nimefika Chuoni Augustana
Jana nilifika chuoni Augustana, Illinois, kutoa mihadhara. Jana jioni niliongea na walimu wachache kuhusu masuala ya utamaduni na utandawazi katika dunia ya leo na umuhimu wa kuwaandaa wanafunzi wetu ipasavyo. Leo nimepata fursa ya kuongea na wanafunzi wapatao 40, ambao wanaenda Ghana na Senegal kwa masomo. Nimekuja hapa chuoni Augustana kusaidia kukuza mpango wa masomo kuhusu Afrika . Profesa John Tawiah Boateng, kutoka Ghana, aliyesimama nami hapa juu, kulia, ni mmoja wa wahusika wa mpango huu, chini ya mratibu wa masomo yahusuyo nchi za nje katika chuo cha Augustana, Dr. Kim Tunicliff. Hapa chini wanaonekana wote wawili, Dr. Tawiah Boateng akiwa katika kunitambulisha kwa waliohudhuria. Dr Tunicliff tulifahamiana miaka iliyopita, alipokuwa makamu rais wa jumuia ya vyuo vinavyoshirikiana katika eneo la Marekani ya Kati, Associated Colleges of the Midwest (ACM). Nilikuwa mwanabodi katika bodi ya uongozi wa jumuia ya vyuo hivi, nikiwa mshauri wa mipango ihusuyo ushirikiano kati ya vyu