Posts

Showing posts from January, 2011

TAMKO LA JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAM JIJINI MWANZA

Nimeona tamko hili nikaamua kuliweka katika blogu yangu, kwa vile ninaheshimu uhuru na haki ya watu kujieleza. Mimi ni m-Katoliki, na ingawa sikubaliani na kila kilichomo katika tamko hili, nimeona lina mengi ya kufikirisha, kwa manufaa ya Taifa letu. Hatuwezi kukwepa ukweli kwamba ni Taifa la watu wa imani mbali mbali na mitazamo mbali mbali, na kwa hivi, pamoja na tofauti zetu, lazima tutafute namna ya kuishi pamoja kwa maelewano. Hatua moja ni kusikiliza maoni ya kila mtu, kwa utulivu na kuheshimiana. Ndio maana nachangia kueneza tamko hili. --------------------------------------------------------------------------------------- TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU JIJINI MWANZA KUHUSU HALI YA KISIASA, KAULI ZA MAASKOFU, NA MUSTAKBALI WA NCHI LILILOTOLEWA JUMAPILI TAREHE 23 JANUARI, 2011 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MBUGANI (MUSLIM SCHOOL), JIJINI MWANZA UTANGUZI: Mwaka 2010 ulikuwa mwaka wa Uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali wakiwemo madiwani, wabunge, wawakilishi

Mikataba Bomu Itaendelea Kutumaliza

Wa-Tanzania wanalalamika sana kuhusu mikataba bomu ambayo inalisababishia Taifa hasara kubwa. Tafsiri yao, kwa ujumla, ni kwamba tunaingizwa katika janga hili na mafisadi ambao wanasaini kwa makusudi mikataba hii, kwamba hao ni wa-Tanzania wenye ubinafsi na uroho, na hawana uchungu na nchi, bali wanatafuta namna ya kunufaika wao. Mafisadi wetu hao wanashirikiana na mafisadi wa nje kuitafuna nchi yetu. Kwa ujumla, nami nina hisia hizo. Kwanza kuna ukweli usiopingika kuwa maadili katika nchi yetu yanazidi kuporomoka. Vile vile nazingatia usemi wa wahenga kuwa lisemwalo lipo, na kama halipo laja. Pia tunaona taarifa kutoka sehemu mbali mbali za dunia kuhusu uozo wa rushwa katika masuala ya mikataba, zabuni, na kadhalika. Lakini msimamo wangu hauishii hapa. Naamini kuwa hata kama tukiondoa kabisa rushwa na ufisadi, tukawa na watu wanaojali maslahi ya nchi na hao ndio wakawa wanaosaini mikataba yetu, bado tutaendelea kulizwa na mikataba bomu. Kitakachosababisha janga hili ni kuanguka kwa

Kitimoto

Image
Neno kitimoto ni maarufu Tanzania. Kitimoto ni nyama ya nguruwe; inapendwa sana katika mabaa na sehemu zingine. Ubora wa kitimoto ni kivutio kwa wateja na neema kubwa kibiashara kwa wenye baa. Hapa kushoto ni sahani ya kitimoto ambayo niliinunua kwenye baa moja Sinza, hatua chache kutoka Lion Hotel. Ninapokuwa katika miji kama Dar es Salaam, napatikana mitaa ya u-Swazi, kama inavyoonekana katika picha hii, iliyopigwa Sinza, bondeni ukifuata barabara inayopita mbele ya Lion Hotel. Kwa wale wasiojua, neno u-Swazi linamaanisha sehemu wanazoishi wananchi wa kawaida. Hapo kushoto kuna baa na sehemu ya kitimoto ambapo nimeshakuwa mteja mara kadhaa. Picha hii inaonyesha jinsi mwenye kitimoto anayotangaza biashara yake. Tofauti na zamani, anaweza kuagiza nyama kutoka bucha kwa kutumia simu, na anaweza kuchukua oda za wateja kwa simu pia. Pamoja na umaarufu wake, kuna hisia tofauti, michapo, na utani kuhusu kitimoto, mambo ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti kama sehemu muhimu ya utamaduni w

Kwa wa-Tanzania, Dini Imekuwa Bangi

Katika hali ya kawaida, dini ni kitu cha manufaa kwa wanadamu, kwa maana kwamba inatufundisha kumtambua na kumcha Mungu, na kwa wale wanaoamini miungu wengi, ni hivyo hivyo. Dini inatufundisha maadili ya kumtendea binadamu mwingine kama tunavyopenda kutendewa. Kwa ufafanuzi zaidi maadili hayo ni kama kupendana, kusikilizana, kuheshimiana, kusameheana, na kutakiana mema. Kwangu mimi m-Katoliki, maadili hayo yalielezwa kwa uwazi na Yesu katika mafundisho yake mengi, hasa pale aliposema kuwa amri kubwa kuliko zote ni kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote, nguvu yetu yote na akili yetu yote, na kumpenda jirani kama tunavyojipenda wenyewe na pia kuwapenda adui zetu. Kwa lugha rahisi ni kuwa tunapowachokoza wengine au kuumiza hisia zao kwa makusudi, au tunapokosa uvumilivu na badala yake tunatunisha misuli na kujibu mapigo, tunaasi dini na kuwa makafiri. Kwa kuzingatia hayo, niliandika makala kuwa penye dini hapana magomvi, na kwamba kuwepo kwa magomvi ni ushahidi wa kukosekana kwa dini. Dhana

Tamko Kuhusu Matamko ya Wa-Tanzania

Tanzania sasa imekuwa nchi ya matamko. Kila kukicha linatolewa tamko kutoka kikundi au jumuia fulani. Katika siku za karibuni, kwa mfano, tumeshasikia matamko kutoka vyama vya siasa, jumuia za kidini, na taasisi mbali mbali, za serikali na zisizo za serikali. Matamko ya wa-Tanzania yanahusu zaidi masuala tata ya jamii, au migogoro. Yanahusu mambo kama sera za serikali au vitendo vya watendaji mbali mbali, kama vile polisi, au taasisi zingine. Mara kwa mara, matamko yanakuwa na hisia za kulalamika, kuonya, au kutangaza msimamo. Kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Binafsi, naliona ni jambo zuri, kwa maana kwamba watu wanatumia uhuru wao wa kuelezea hisia, mawazo na mitazamo yao. Kwa hivi, sishangai kuyasikia matamko hayo. Kila mtu ana haki ya kutoa tamko lake, ili mradi havunji sheria au kuingilia uhuru wa wengine wa kutoa matamko. Utamaduni wa matamko ni mzuri. Ni bora kuliko tunayoyaona au kuyasikia yakitokea katika jamii za wenzetu, ambao migogoro yao inawapele

Andika ki-Swahili; ki-Ingereza Hatuelewi

Kuna tabia katika jamii ya wa-Tanzania ya kulalamika pale mtu anapoandika ki-Ingereza. Malalamiko haya yanaonekana mara kwa mara katika blogu ya Michuzi , kwa mfano, ambayo inasomwa sana na wa-Tanzania, pale inapotokea makala iliyoandikwa kwa ki-Ingereza. Walalamikaaji wanakumbushia kuwa wa-Tanzania wengi hawajui ki-Ingereza, na kwa hivi wanataka mwandishi awafikirie hao kwa kuandika kwa ki-Swahili, lugha wanayoifahamu. Ujumbe unaojitokeza katika malalamiko hayo ni kwamba ni jambo la uzalendo kwa mwandishi kuwafikiria hao wa-Tanzania walio wengi, ili nao wapate kufaidika na yale yanayoandikwa. Sijawahi kuona malalamiko hayo yakipingwa. Inaonekana kuwa hoja inayotolewa katika malalamiko hayo inakubalika miongoni mwa wa-Tanzania. Katika kulitafakari suala hili, naona kuna haja ya kuwakosoa hao walalamikaji. Ingawa ni kweli kuwa mtu akiandika kwa ki-Swahili anawafikia wananchi wasiojua ki-Ingereza, kuna pia tatizo la uvivu katika jamii yetu. Malalamiko hayo ni sehemu ya tatizo hili

Nimejiunga na Bodi ya Operation Bootstrap Africa

Nimerejea jioni hii kutoka Minneapolis, kuhudhuria mkutano wa bodi ya Operation Bootstrap Africa (OBA). Mimi ni mwanabodi wapya. Niliteuliwa mwishoni mwa mwaka jana, na mkutano wa leo ulikuwa ni wa kwanza kwangu. Nilifahamu habari za OBA tangu nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, 1980-86, kwamba ilikuwa inajishughulisha sana na masuala ya elimu Tanzania. Mwaka jana, nilipopendekezwa kuwa mwanabodi, nilifanya juhudi za kuifahamu zaidi OBA . OBA , imefanya mengi ya manufaa kwa nchi ya Tanzania, kwa kuhamasisha michango miongoni mwa wa-Marekani. Yeyote anayewafahamu vizuri wa-Marekani, anatambua jinsi wanavyojituma katika shughuli za kujitolea. Ni jambo ambalo wanafundishwa tangu utotoni, na linasisitizwa mashuleni, kuanzia madarasa ya mwanzo kabisa hadi chuo kikuu. Nilikaa katika mkutano wa leo nikisikiliza taarifa za michango inayotolewa na watu mbali mbali kwa manufaa ya Tanzania, watu wenye hela nyingi na wasio na hela nyingi, nikawa najiuliza kwa nini sisi wenyewe

Wauza Vitabu wa Mitaani Dar es Salaam

Image
Kitu kimojawapo kinachonivutia ninapokuwa Dar es Salaam ni wauza vitabu wa mitaani. Wako wa aina mbili. Wako wenye sehemu maalum ya kuuzia vitabu, iwe ni meza tu au kibanda. Hao wanaonekana sehemu mbali mbali za mjini Dar es Salaam, kuanzia katikati ya mji, kama vile barabara ya Samora, hadi sehemu za pembeni, kama vile Mwenge na Ubungo. Picha iliyoko hapa kushoto niliipiga Ubungo, mwaka jana, karibu na kituo kikuu cha mabasi. Pembeni ya mwuza vitabu kuna kibanda cha muuza machungwa. Wako wauza vitabu wengine ambao hutembeza vitabu mitaani, sawa na wale vijana ambao wanatembeza bidhaa mbali mbali, ambao tunawaita machinga. Hapo kushoto kuna picha niliyopiga Sinza Kijiweni, mwaka jana, kwenye hoteli ya Deluxe. Nilikuwa hapo, na hao vijana wawili wakaja, mmoja akiuza vitabu na mwingine peni za kuandikia. Nilivutiwa, nikaanza kuongea nao. Nilimwuliza huyu muuza vitabu kuhusu wateja, na kama wa-Tanzania wananunua vitabu, akanielezea uzoefu wake. Nilinunua vitabu viwili. Kimoja ni tafs

Mwongozo wa "Things Fall Apart"

Image
Nimefundisha riwaya ya Things Fall Apart ya Chinua Achebe tangu yapata mwaka 1976, sehemu kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Chuo Kikuu cha Burundi, na vyuo vya Colorado na St. Olaf . Kutokana na uzoefu huu, na mengi niliyojifunza, na kwa lengo la kuweka kimaandishi mawazo yangu juu ya riwaya hii, niliandika mwongozo. Nimeshaongelea kidogo kuhusu mwongozo huu katika blogu hii , lakini napenda kueleza zaidi habari zake. Aliyenisukuma kuandika mwongozo huu kwa wakati niliofanya hivyo ni rafiki yangu A.S. Muwanga, aliyekuwa katika Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye na mimi tulikubaliana kuwa niandike pia mwongozo kuhusu kitabu cha The African Child , kilichoandikwa na Camara Laye. Muwanga alifanya mpango na kitabu kilichapishwa mwaka 1988 na Nyanza Publications Agency kama inavyoonekana katika picha hapo juu. Lengo mahsusi lilikuwa ni hasa kuwasaidia wanafunzi wa sekondari waliokuwa wanasoma riwaya hizo. Miaka hiyo, 1976 hadi 1991, nilikuwa mha