Nimesifiwa kwa Kutumia Lugha Vizuri
Jana jioni nilikuwa kwenye baa moja karibu na Lion Hotel, Sinza, ambapo nilikutana na daktari mmoja rafiki yangu wa miaka mingi. Alikuwa na kaka yake, ambaye naye ni msomi. Kisha akaja rafiki yao mmoja, ambaye ni mfanyabiashara. Baada ya takriban saa moja ya maongezi yetu, huyu mfanyabiashara alisema ameguswa na namna ninavyoongea ki-Swahili vizuri, ingawa nimekaa Marekani miaka mingi. Alisema ameguswa na jinsi ninavyoongea bila kutumia maneno ya ki-Ingereza. Daktari akachangia mada hii kwa kusema kuwa hata ninapoongea ki-Ingereza, huwa siigi namna wanavyoongea wa-Marekani. Hapo waheshimiwa hao wakalalamika kuhusu watu ambao hata wakienda Marekani kwa miezi sita tu, wanakuja hapa na kujifanya hawawezi kuongea kama wa-Tanzania. Daktari aliigiza mikogo ya watu hao, tukawa tunacheka. Nilifurahi kusifiwa hivyo. Nilichukua fursa hii kuwaeleza kuwa hata ninapokuwa kijijini kwangu watu wanashangaa jinsi ninavyoongea ki-Matengo vizuri kabisa, ingawa nimekaa Marekani miaka mingi. Tena nin