Posts

Showing posts from August, 2012

Kumbukumbu ya Johannesburg: Mwanamuziki Moeketsi

Image
Nilikuwa Johannesburg, Juni 14 hadi 18 mwaka huu, kama nilivyoandika hapa . Tarehe 17 nilikuwa katika ziara ya sehemu kadhaa za mji wa Johanneburg. Sehemu moja tuliyotembelea inaitwa Newton, na hapo ndipo nilipopiga picha inayoonekana hapa. Nimekaa pembeni ya sanamu ya Kippie Moeketsi, mpiga saksofoni maarufu, aliyezaliwa mwaka 1925 na kufariki mwaka 1983. Mwenyeji wetu aliyekuwa anatuongoza katika ziara hii alisema kuwa Kippie aliamua kubaki nchini Afrika Kusini pamoja na matatizo yote ya utawala wa makaburu. Leo nimeangalia taarifa za mwanamuziki huyu mtandaoni, nikagundua kuwa huenda nilishasikia na kupendezwa sana na muziki wake. Hebu msikilize:

Uzinduzi wa Mzunguko wa Tano wa Mashindano ya Uandishi

Image
UZINDUZI WA MZUNGUKO WA TANO WA MASHINDANO YA UANDISHI WA RIWAYA ZA KIINGEREZA KWA AJILI YA VIJANA   Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania (CBP), Abdullah Saiwaad (kushoto), akimkabidhi Mkama Mwijarubi, hundi ya dola za kimarekani 2000 Dar es Salaam jana, baada ya kitabu chake alichoandika cha Kiss Kiddo: The birthday party kuchaguliwa kuwa moja ya kitabu bora ambacho kitaingia katika mzunguko wa nne wa mashindano ya uandishi wa riwaya za kiingereza kwa ajili ya vijana. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Mradi huo Pilli Dumea. Katibu Mtendaji wa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania (CBP), Pilli Dumea (katikati), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam jana, moja ya vitabu vilivyo ingizwa katika muhutasari wa vitabu bora vilivyoandikwa kwa lugha ya kiingereza chini ya mradi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya (CBP), Abdullah Saiwaad na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Tuzo ya Burt Adam Shaffi. -- Na Mwandishi Wetu Tuzo ya Burt ya Fas

Rais Mkapa na Vitabu

Image
Nimeiona picha hii kwenye blogu ya Michuzi . Inamwonyesha karani wa sensa akiwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa. Wako katika shughuli ya sensa. Kitu kilichonifanya niandike ujumbe huu ni vitabu vinavyoonekana hapo pichani. Daima nimekuwa nikijiuliza je, mawaziri, wabunge, wakurugenzi, na wengine wote ambao tunawaita viongozi, wana vitabu majumbani mwao, na je, wanavisoma? Ni faraja na heshima kuwa na viongozi wanaosoma vitabu. Ingekuwa jambo jema iwapo watu wanapogombea ubunge au nafasi nyingine ya uongozi, tungewauliza kama wana vitabu, kama wanasoma vitabu, na kwa muda huu wanapogombea wanasoma vitabu vipi. Hapo tungeweza kuwabaini watu makini na mavuvuzela pia. Lakini tatizo ni kuwa utamaduni wa kusoma vitabu haupo Tanzania. Kwa hivyo, mavuvuzela nao wanaingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wakiwa na uhakika kuwa hakuna atakayewauliza kuhusu masuala ya vitabu.

Mwanaanga Neil Armstrong Amefariki

Image
Mwanaanga Neil Armstrong alikuwa binadamu wa kwanza kutua na kutembea mwezini, Julai 20, 1969. Dunia nzima ilisisimka kutokana na tukio hilo. Wakati ule nilikuwa shuleni, kidato cha tatu. Tulifuatilia kwa makini habari nzima za shirika la NASA hadi kufikia hatua ile ya kihistoria. Hayo nayakumbuka vizuri sana. Nakumbuka pia kuwa sheikh moja wa Tanzania alitoa tamko kuwa haiwezekani binadamu kwenda mwezini, kwani Quran haiafiki. Kwetu sisi, Neil Armstrong alikuwa shujaa, pamoja na wenzake Edwin Aldrin na Michael Collins waliosafiri naye kwenye chombo chao, Apollo 11. Nakumbuka kuwa katika Tanzania, kuna watu waliviita vyombo vyao vya usafiri, kama vile magari, Apolo 11. Neil Armstrong amefariki, akiwa na umri wa miaka 82. Mungu amweke mahali pema Peponi. Amina.

"The Satanic Verses:" Kitabu Kigumu Kukielewa

Image
The Satanic Verses , kitabu cha Salman Rushdie,  ni kitabu ambacho nimekiona kigumu kukielewa. Nilinunua nakala miaka mingi kidogo iliyopita, nikaanza kusoma, lakini sikufika mbali. Mtindo aliotumia Rushdie katika kuandika kitabu hiki unahitaji msomaji awe amesoma sana vitabu vingine. Inatakiwa msomaji awe anajua mambo mengi, kuanzia yale ya falsafa hadi ya hadithi na dini. Vinginevyo, ni rahisi kutoka kapa unapojaribu kusoma The Satanic Verses . Mwandishi maarufu Nadine Gordimer wa Afrika Kusini, ambaye alipata tuzo ya Nobel mwaka 1991, amegusia suala hili alipoandika kwamba "anyone who actually has read, and been sufficiently literate fully to understand, this highly complex, brilliant novel knows that dominant among its luxuriant themes is that of displacement." Hayo ameyaandika katika insha yake, "Censorship--the Final Solution, the Case of Salman Rushdie," Telling Times, Writing and Living, 1954-2008 , uk. 448. Mimi ni profesa wa masomo ya ki-Ingereza

Utamaduni wa Kusoma Vitabu

Image
Picha hii nimeiona kwenye mtandao wa VOA NEWS . Ilipigwa ufukweni Ziwa Nyasa, upande wa Malawi. Nimevutiwa na huyu mtalii anayejisomea kitabu. Ninafahamu manufaa ya kusoma vitabu; navisoma kila siku. Nafahamu faida ya kuwa na vitabu, kwani ninavyo zaidi ya 3000. Kama ninavyoandika mara kwa mara katika blogu hii na sehemu zingine, utamaduni wa kusoma vitabu uko sana miongoni mwa wa-Marekani. Ni kawaida kwa wa-Marekani kuwanunulia wenzao vitabu kama zawadi, kwa mfano kwenye nyakati muhimu kama Krismasi. Wa-Marekani wanapokwenda nchi yoyote kama watalii, ni kawaida kwao kutafuta vitabu kuhusu nchi ile, wavisome kabla ya kusafiri, wakishafika kwenye nchi ile, au wakisharudi kwao. Ndio maana watalii hao hupenda sehemu zenye maduka ya vitabu. Wa-Tanzania wangekuwa makini wangetambua na kuitumia fursa hiyo, kama nilivyoelezea katika kitabu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Lakini lazima nikubali kuwa kuweka mawazo na mawaidha katika kitabu haiisaidii jamii ambayo haina utamaduni wa kus

Kufungiwa kwa Gazeti la MwanaHalisi

Watetezi wa haki za binadamu, asasi za kijamii na wadau wakuu wa habari nchini, leo wameipa serikali siku saba kufungulia gazeti la MwanaHALISI, vinginevyo wataitisha maandamano ya kupinga hatua ya serikali kufungia gazeti hilo kwa muda usiojulikana, kuminya uhuru wa habari, haki za binadamu na utesaji wa wanaharakati.  Tamko la asasi hizo ni kama ifuatavyo hapa chini: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 22 Agosti 2012 YAH: KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANAHALISI   KWA mara nyingine tena, tumewaiteni hapa kuwaomba mtufikishie ujumbe wetu huu kwa watawala. Ujumbe wenyewe unahusu kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda aliyoitoa bungeni, Alhamisi tarehe 16 Agosti 2012. Kama mnakumbuka vema, wakati akijibu swali bungeni siku hiyo, Waziri Mkuu Pinda alisema, “Serikali imechukua wajibu wake kulifungia gazeti hilo, na kwamba kama wahusika hawakuridhika na hatua iliyochukuliwa na serikali wana haki ya kukata rufaa kwa mamlak

Ziarani Israel

Image
Mwishoni mwa Desemba, mwaka 1992, nilikwenda Israel kuhudhuria mkutano wa Israeli Folklore Society, ambao ulifanyika mjini Nazareth. Tulihudhuria watafiti kutoka nchi mbali mbali. Tulipata pia fursa ya kutembelea sehemu mbali mbali, kama vile Jericho, Jerusalem na Bethlehem. Hapa pichani naonekana nikiwa Jerusalem. Ilikuwa tarehe 29 Desemba. Huyu mzee aliye kushoto alikuwa akijaribu kuniuzia hilo vazi nililovishwa kichwani. Wachuuzi wa Jerusalem ni mahiri sana, wenye ushawishi mkubwa. Kwa ushawishi wao, na ucheshi, mtu unaweza kujikuta unanunua bidhaa ambazo hukutegemea.

Kususia Sensa ni Kujihujumu

Image
Sensa ni muhimu kwa nchi yoyote kwa maana kwamba ni sherti serikali ijue idadi ya watu wake na mahali wanapoishi. Takwimu na taarifa hizo ndio msingi wa upangaji wa mipango yoyote ya huduma na maendeleo. Kwa akili yangu finyu, huu ni ukweli usiopingika. Kama kuna sehemu ambapo watu hawajahesabiwa, sehemu hiyo itaonekana iko wazi; haina watu. Kwa maana hiyo, hakutakuwa na msingi wowote wa kuiingiza sehemu hiyo katika mpango wa huduma au maendeleo. Sehemu itakayoonekana haina watu itawekwa kando katika mipango hiyo ya huduma na maendeleo. Sasa basi, endapo kulikuwa na watu sehemu hiyo, ambao walisusia sensa, wasije wakajitokeza baadaye na kulalamika kuwa wanaonewa.

Salamu za Idd Mubarak

Image
Kwa siku hii tukufu ya Idd Mubarak, napenda kutoa salam kwa ndugu zetu wa-Islam waliotimiza majukumu ya Mwezi Mtukufu hadi kumaliza vizuri. Naamini kuwa baraka za Muumba zitokanazo na ibada hizi zinatuneemesha sote. Pia naomba Muumba atusaidie kujenga mshikamano na undugu miongoni mwetu wanadamu wote, kwani hili ni fundisho la msingi la dini zetu. Fundisho hili nimeliona katika picha hii ninayoibandika hapa, ambayo nimeikuta Facebook.

Leo Ninatimiza Miaka 61

Leo ninatimiza miaka 61 ya maisha yangu. Pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuniweka hai hadi leo, ni lazima nijiulize: nimetumiaje fursa hii aliyonijalia Mungu ya kuwepo duniani miaka yote hiyo? Mungu ametuweka hapa duniani kwa sababu gani? Maisha yetu yana faida gani kwa wanadamu wenzetu? Tuna malengo gani yenye manufaa kwa wanadamu wengine siku hadi siku, mwezi hadi mwezi, mwaka hadi mwaka? Miaka hii ninamwazia na kumsoma sana Ernest Hemingway. Alifariki akiwa na umri unaofanana na huu niliofikia leo. Tangu akiwa kijana, na miaka yote ya maisha yake, alitoa mchango mkubwa kwa walimwengu kwa uandishi wake. Alipokuwa na miaka 53, alitunukiwa tuzo ya Nobel katika fasihi. Je, nikijifananisha na watu kama Hemingway, mimi nimeshafanya nini? Masuali haya ni magumu. Siku ya leo, pamoja na kumshukuru Mungu, pamoja na kujiuliza kuhusu wajibu wangu hapa duniani, nawajibika kuwakumbuka wenzetu wengi ambao hawakupata fursa ya kuishi miaka niliyoishi. Wengi wamefariki wakiwa wachanga, wengine v

Matukio Afrifest 2012

Image
Kama ilivyo katika matamasha mbali mbali ninayohudhuria, katika tamasha la Afrifest lililofanyika siku chache zilizopita, kulikuwa na matukio mengi ya kukumbukwa, na nilipata bahati ya kukutana na watu wengi. Napenda kuongelea tukio moja. Alikuja kwenye meza yangu mama mmoja. Katika maongezi nilitambua kuwa ni m-Marekani mweusi. Tuliongelea kuhusu shughuli zangu za ufundishaji, na pia alipenda kujua mada za vitabu vyangu, nami nikamwelezea. Alichukua vitabu vifuatavyo: Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , Africans in the World, na Matengo Folktales . Kisha, alipoona kitabu cha ki-Swahili, CHANGAMOTO: Insha za Jamii , alikichukua. Nilishangaa kidogo kuona anachukua kitabu cha ki-Swahili, wakati haijui lugha hiyo. Aliniambia kuwa mume wake ni m-Somali kutoka Kenya, ambaye anajua ki-Swahili. Akaendelea kunieleza kuwa anamnunulia hicho kitabu. Kisha akaniomba nikisaini, nami nilifanya hivyo, nikaandika na salaam kwa ki-Swahili. Niliwahi kuandika katika blogu h

Afrifest Twin Cities 2012

Image
Kwa mara nyingine tena, tamasha la Afrifest limefanyika hapa Minnesota. Tamasha hili hufanyika mara moja kwa mwaka, na huu ni mwaka wa sita. Kulikuwa na shughuli mbali mbali, kuanzia tarehe 10, hadi 12. Hapa naleta picha chache za shughuli ya jana, yaani tarehe 12. Kama kawaida, wauza bidhaa mbali mbali walikuwepo. Hili banda lilikuwa na kaseti za hotuba za wanamapinduzi mbali mbali waliojihusisha na harakati za wa-Marekani Weusi. Kulikuwa pia na t-shirts na vitu vingine, vyenye picha za watu maarufu kama Marcus Garvey, Bob Marley, na Malcolm X. Hapa nilinunua t-shirt yenye picha ya Bob Marley. Hao jamaa, wenye asili ya Jamaica, walikuwa wanauza chakula. Tamasha la Afrifest ni fursa ya wafanya biashara kuleta bidhaa au huduma zao. Hapa kushoto kabisa ni banda la benki ya Wells Fargo. Tamasha kama hili kwa vile ni fursa ya kuwapata wateja wapya. Hapa ni wachezaji wa soka wakiingia. Shughuli za Afrifest ni kwa ajili ya watu wa kila rika. Watoto nao hushiriki.

Maprofesa Wanakipenda Kitabu Hiki

Image
Siku chache zilizopita, nimeona makala ya Elizabeth M. Cannon na Carmen Heider ambao ni maprofesa wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Oshkosh. Wameelezea jinsi kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kilivyowasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi waliowaleta Tanzania kimasomo. Makala yenyewe ni " A Study Abroad Program in Tanzania: The Evolution of Social Justice Action Work," Humboldt Journal of Social Relations , 34 (2012), 61-84 Maprofesa hao waliwaleta wanafunzi Tanzania mwaka 2008, 2010 na 2012. Pamoja na mambo mengine, wameelezea matatizo waliyoyapata katika kuwahamasisha wanafunzi kwenye vipengele kadhaa vya masomo yao. Hatimaye walitafuta njia ya kukitumia kitabu cha Africans and Americans katika mijadala darasani, kwa kuwapangia wanafunzi sehemu za kusoma ili waongoze majadiliano darasani. Mkakati huu ulileta mafanikio mazuri, kama wanavyoeleza hapa: We also thought carefully about how to design our on-site class sessions to reflect

Tamasha la "Afrifest 2012" Minnesota

Wikiendi hii kutafanyika tamasha jingine la Afrifest hapa Minnesota. Tamasha hili hufanyika kila mwaka, na huu ni mwaka wa tano. Lengo ni kuwakutanisha wa-Afrika, watu wenye asili ya ki-Afrika, na wengine wote, kwa ajili ya kujionea na kuelimishana kuhusu mambo mengi ambayo watu weusi wamefanya katika historia, katika nyanja mbali mbali. Ni fursa ya kusherehekea mafanikio yao katika fani mbali mbali, na pia kubadilishana mawazo kuhusu changamoto zilizopo, kwa lengo la kujipanga kwa mshikamano na maendeleo siku za usoni. Nafurahi kuwa nimekuwa mshirika katika shughuli za Afrifest tangu mwanzo, kama mwanabodi wa Afrifest na sasa mwenyekiti wa bodi. Kesho, tarehe 10 jioni, tutafanya ufunguzi wa tamasha. Nitaongea machache kuhusu Afrifest na kisha watu watapata fursa ya kujumuika na kufahamiana. Keshokutwa, Jumamosi, na hadi Jumapili, tutakuwa na maonesho ya aina aina. Nami nitakuwa na meza yangu, nikiwa na vitabu na machapisho mengine. Kwenye shughuli hizi napata fursa ya kuongea na w

Kwenye Baa Hakuna Udini

Katika wiki sita zilizopita, nimepata fursa ya kuichunguza nchi yangu kwa karibu. Kitu kimoja kilichonigusa, ingawa sio kigeni, ni kwamba kwenye baa hakuna udini. Niliamua niandike makala hii kuhusu jambo hilo, kwani naona linasisimua. Nimezunguka Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Songea, na kwa vile baada ya shughuli zangu za mchana napenda jioni kuvinjari baa, nimejikuta nikijumuika na wa-Islam na wa-Kristu katika baa kwenye miji hiyo. Kilichobadili hali hiyo ni ujio wa Mwezi Mtukufu. Lakini kabla ya hapo wa-Islam na wa-Kristu tulikuwa tunajumuika vizuri kabisa huko baa. Hatubaguani bali tunakaribishana. Tunaongea; tunapiga soga; tunajenga mahusiano mema. Kwenye baa moja Tanga, nilipata fursa ya kuongea na meneja, ambaye ni mu-Islam. Mada yetu ilikuwa ulabu. Nilianza mimi, kwa kusema kuwa katika dini yetu, hatukatazwi kunywa pombe. Tunakatazwa kulewa. Meneja naye akaionyesha kidole bia yangu na kuniambia kuwa kwa mu-Islam, ile bia yangu ni haram. Muislam haruhusiwi kuinywa hata