Posts

Showing posts from December, 2019

Kofia ya CCM Nchini China

Image
Naleta picha ya ujumbe wa CCM kwenye kikao na wenyeji wao mjini Shanghai, China, mwaka 2018. Hapo mezani upande wa kushoto kuna kofia ya CCM. Yawezekana walikwenda ziarani na magwanda yao na vikofia. Je, kuna sababu gani mimi kuandika ujumbe kuhusu kofia? Sina jambo la maana zaidi la kuongelea? Kwa nini nisiongelee madhumuni ya ziara na mafanikio yake? Ninaandika ujumb e huu kama mtafiti, mwandishi, na mtoa ushauri juu ya masuala ya utamaduni na utandawazi. Nimekuwa nikifanya shughuli hizo hapa Marekani na Tanzania pia, ambako nimeendesha warsha mara kadhaa kuanzia mwaka 2008 katika miji ya Arusha, Tanga, na Dar es Salaam. Ninajaribu kuwaelewesha watu kuwa tofauti za tamaduni zina athari kubwa, hasa katika dunia ya utandawazi wa leo. Tunapokutana na watu wa tamaduni tofauti na wetu, tuwe makini. Tunaweza tukaelewana vibaya, au tunaweza tusielewane. Ni muhimu tujielimishe kuhusu tofauti hizo kabla hayajatupata hayo. Kofia ya CCM ni sehemu ya vazi rasmi la wana CCM. Ni utambulisho w

Maongezi Kuhusu Fasihi Simulizi ya Africa

Image
Jana jioni, kwa mwaliko wa chama cha wanafunzi kiitwacho Karibu, nilitoa mhadhara hapa chuoni St. Olaf  kuhusu fasihi simulizi ya Afrika. Tuna wanafunzi wachache kutoka Afrika, lakini wanajitahidi kuitangaza Afrika kwa namna mbali mbali, kama vile mihadhara, filamu, ngoma, muziki, michezo ya kuigiza, na maonesho ya mavazi. Mara kwa mara wananialika kuelezea utamaduni wa Afrika, hasa unavyojitokeza katika fasihi simulizi. Nami hupenda kufanya hivyo. Ninauenzi mchango wa Afrika duniani. Afrika ni chimbuko la binadamu. Ni chimbuko la tekinolojia, sayansi, lugha, fasihi, falsafa, na kadhalika. Hiyo jana nilelezea hayo, nikaleta methali kadhaa kuthibitisha uzito wa falsafa ya wahenga wetu kuhusu masuala ya maisha na maadili. Tulitafakari methali hizo, na mwishoni nilisimulia hadithi iitwayo "The Donkey Who Sinned," iliyomo katika kitabu cha Harold C. Courlander kiitwacho A Treasury of African Folklore. Nayo tuliitafakari, kwa jinsi inavyoonyesha athari za ubabe kwa wale wasi