Posts

Showing posts from February, 2010

Nimejiunga "twitter"

Napenda kuwafahamisha wasomaji wa blogu hii na maandishi yangu mbali mbali kuwa nimejiunga "twitter," mtandao wa mawasiliano ya haraka haraka. Bofya hapa . Shukrani kwa kuwa pamoja nami katika blogu hii. Nawakaribisha kujumuika nami "twitter" vile vile na kufuatilia shughuli zangu kwa karibu zaidi.

Maandalizi ya "Afrifest 2010"

Image
Leo nilienda Minneapolis kwenye mkutano wa maandalizi ya Afrifest , tamasha la utamaduni linalofanyika hapa Minnesota kila mwaka, kama kielelezo cha historia na mchango wa wa-Afrika katika ulimwengu. Tulikutana katika mgahawa uitwao 1st Cup Cafe. Ni sehemu ambapo wa-Afrika hupenda kukutana na shughuli nyingi hufanyika hapo, kama vile mihadhara, uzinduzi wa vitabu, na burudani. Mwanzilishi wa Afrifest ni Nathan White, ambaye anaonekana katika picha hapa juu, wa pili kutoka kulia. Mimi ninayeonekana kulia kabisa nimekuwa mwanachama wa kamati hii tangu mwanzo. Mchango wangu umekuwa zaidi katika kuelezea historia ya watu wenye asili ya Afrika, tangu chimbuko la binadamu katika Afrika hadi kuenea kwa wa-Afrika hao sehemu mbali mbali za dunia. Hilo ndilo somo ninalotoa siku ya tamasha, nikiwa na vielelezo kadha wa kadha vya kimaandishi. Shughuli zote tunazofanya kama wanakamati ni za kujitolea, lakini tunazifanya kwa moyo mmoja kwa vile tunaamini umuhimu wa kuwakutanisha watu wenye asili

Maongezi Mjini Faribault, Minnesota

Asubuhi leo nilikwenda mji wa Faribault, mwendo wa nusu saa. Nilikuwa nimealikwa na Mama Delane James, mkuu wa maktaba ya Faribault , kwenda kuongea na wafanyakazi wa maktaba kuhusu masuala ya utamaduni wa wa-Afrika. Mji wa Faribault unazidi kuwa na watu kutoka pande mbali mbali za dunia, wengine wakiwa wakimbizi au wahamiaji wa kawaida au watafuta ajira. Miji mingi hapa Marekani inajikuta katika hali hiyo. Matokeo yake ni kuwa wenyeji wa miji hiyo na hao wageni wanakumbana na masuala yatokanayo na tofauti za tamaduni. Wahudumu wa maktaba wanakumbana na masuala hayo pia, kwani wageni hao nao ni wateja wa maktaba, ambapo wanatafuta ujuzi wa aina mbali mbali, kama vile lugha, ili kuweza kuyafahamu mazingira na maisha katika nchi ya Marekani. Ingawa nilishafika katika maktaba ya Faribault mara kadhaa, sikutambua kuwa ina wafanykazi wengi kama niliowaona kwenye mkutano wa leo. Nilipata fursa ya kutoa mawaidha ya msingi kuhusu umuhimu wa kujifunza suala la tofauti za tamaduni, ili kuepush

Fursa za Kuwatoa Upepo wa-Tanzania

Pamoja na kuwa kazi yangu ya msingi huku Marekani ni kufundisha, ninajishughulisha pia na mipango ya uhusiano baina ya vyuo vya Marekani na Tanzania na nchi zingine za Afrika. Mipango hii ni ile ya kupeleka wanafunzi Afrika. Kwa upande wa Tanzania, napata pia fursa ya kufanya mahojiano (intavyuu) na wasomi wanaotafuta nafasi ya kuja Marekani kwa masomo zaidi au utafiti. Hizi ni kazi za kujitolea, lakini nazifanya kwa moyo moja, nikizingatia umuhimu wake kwa upande wa Marekani na nchi zetu, kwani, pamoja na kutoa fursa mbali mbali kwa wahusika, zinakuza maelewano duniani. Mtu unapokuwa na fursa au wadhifa kama wangu, wa-Tanzania wanasema umeula. Wanaamini unalipwa hela nyingi sana, tena dola, si madafu. Pili, wanategemea kuwa unatumia fursa hizi kujitajirisha sana kifedha kwa msingi wa "akili mkichwa." Zaidi ya yote, wa-Tanzania wanataka wakuone unaishi maisha ya hali ya juu, si uwe unakula pilau au chapati kwenye vihoteli vya Ubungo au Kinondoni. Siku moja, miaka ya tisin

Mwaliko wa Mhadhara: Kampuni ya RBC Wealth Management

Nimealikwa na kampuni ya RBC Wealth Management mjini Minneapolis, kwenda kutoa mhadhara tarehe 19 Februari. Kampuni hii ambayo shina lake ni nchini Canada, inafanya shughuli zake sehemu mbali mbali duniani, ikiwa na wafanyakazi wanaozidi 80,000. Kama ninavyosema mara kwa mara katika blogu zangu na maandishi mengine, dunia ya leo inavyozidi kuwa kijiji, na watu wa mataifa na tamaduni mbali mbali kujikuta wakifanya kazi pamoja maofisini, vyuoni, katika biashara, na kadhalika, ni muhimu kujielimisha na masuala ya tofauti za tamaduni. Kujielimisha huko ni msingi mojawapo wa mafanikio. Kampuni ya RBC Wealth Management imenialika makusudi ili kuongelea suala la mahusiano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali wanaofanya kazi katika kampuni hiyo, kwani wafanyakazi hao wanatoka sehemu mbali mbali za dunia. Kampuni hii ilishanialika miaka michache iliyopita, kuongea na viongozi na maofisa wa kampuni kuhusu masuala haya haya. Walitaka kupata mawaidha kuhusu namna ya kushughulika na wafanyakaz

Wamarekani Safarini Malawi

Image
Leo nilikwenda mjini Chippewa Falls, katika jimbo la Wisconsin, umbali wa maili 123 kutoka Northfield, ambapo naishi. Nilienda kuongea na kikundi cha wa-Marekani wanaojiandaa kwenda Malawi kwa shughuli za kujitolea. Nilialikwa na Mama Diane Kaufmann, ambaye anaonekana kushoto kwangu, katika picha hapa juu. Yeye ameenda Malawi mara kadhaa, katika wadhifa wake kama mratibu wa mpango wa ushirikiano baina ya dayosisi ya Kanisa la kiLuteri Kaskazini Magharibi ya Wisconsin na Malawi. Ana uzoefu wa kupeleka vikundi vya wanadayosisi Malawi katika mpango huo. Vile vile tumeshirikiana kwa miaka kadhaa katika kuendesha mafunzo kwenye kituo cha Luther Point . Kikundi nilichoenda kukutana nacho leo kinaenda Malawi kuwashughulikia watu wenye matatizo ya macho, na kuwagawia miwani. Wanatarajia kufanya shughuli hizo Karonga na Chitipa. Baadhi yao wameshaenda Malawi, na kwa wengine hii itakuwa ni mara yao ya kwanza. Mama Kaufmann aliniita niongee nao kuhusu masuala ninayoongelea katika kitabu changu c

Kioo cha Lugha: Jarida la Kiswahili la Isimu na Fasihi

Image
Leo nilienda posta nikakuta bahasha yenye vitabu ikiwa imetumwa Dar es Salaam. Sikujua ni vitabu gani. Nilipofungua nikakuta ni nakala za jarida la Kioo cha Lugha . Nimefurahi kupata hazina hii nikiwa huku ughaibuni ambako natumia ki-Ingereza karibu muda wote. Sasa, kwa kusoma makala maridhawa zilizoandikwa na watafiti na walimu mahiri wa Tanzania, Kenya, na kwingineko, nitajiongezea ujuzi wa kutumia ki-Swahili katika taaluma, hasa isimu na fasihi. Miaka ya karibuni nimepata msisimko wa kuandika kwa ki-Swahili, ili kujitoa katika giza la ujinga linalotukabili wasomi wengi. Ujinga huu ni pamoja na kutoelewa namna ya kutumia ki-Swahili ipasavyo, na pia kudhani kuwa ki-Swahili hakina uwezo sawa na lugha zingine katika kuelezea mambo, hasa taaluma. Ninajitahidi kujikomboa. Mwaka jana, kwa mfano, niliandika makala nyingi kwa ki-Swahili, hadi nikachapisha kitabu . Wakati wa kuandika nilisoma kazi kadhaa za Shaaban Robert ili kujijengea uwezo na kujiamini katika kutumia lugha ya ki-Swahili