Posts

Showing posts from July, 2009

Taifa la Kesho

Image
Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Picha hii inatueleza mengi kuhusu malezi ya watoto katika jamii yetu. Ni kawaida kwa watoto katika Tanzania kuonekana kwenye baa, na kwenye miziki, hata usiku wa manane. Humo mitaani wanashuhudia mambo ya ajabu mengi, kuanzia ulevi, matusi, na hata watu kuumizwa au kuuawa kwa tuhuma za wizi. Kuwapiga au kuwaua wezi imeshakuwa kivutio kikubwa mitaani, kama vile burudani. Haya ndio malezi ya watoto wa leo. Watakapokuwa watu wazima, itakuwaje? Picha hapo juu niliiona kwenye blogu fulani, ila nimesahau. Nitapenda kutafuta chanzo ili niweke taarifa kikamilifu.

Picha kutoka Tamasha la Utalii (KTTF) 2009

Image
Tarehe 5-7 Juni, kulifanyika tamasha la utalii Arusha, Tanzania. Tamasha hili hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi Juni. Wahusika wa Programu ya Utalii Mto wa Mbu walishiriki tamasha hilo. Leo wameniletea picha za kumbukumbu.

Mafanikio ya Mradi wa Utalii: Mto wa Mbu

Nimesoma taarifa ya kufurahisha katika Arusha Times kuwa mradi wa utalii Mto wa Mbu, umeteuliwa kuwa mfano wa kuigwa nchini Tanzania. Ni heshima kubwa, nami natoa pongezi kwa vijana wanaoendesha mradi huu. Nimewafahamu vijana hao kwa miaka kadhaa, tukizungumzia masuala mbali mbali muhimu. Katika kupita kwangu Mto wa Mbu na wanafunzi wa kiMarekani, vijana hao wamekuwa wenyeji wetu wa kutueleza masuala ya tamaduni za mji ule. Nimeandika habari zao kwenye blogu yangu . Nao katika blogu yao wameandika habari ya ushirikiano wetu . Ni jambo la kufurahisha kuwaona vijana wakijituma katika shughuli za maendeleo namna hii, na nawatakia mafanikio makubwa zaidi siku za usoni.

Lugha za asili ni muhimu sana zisiachwe zikatoweka

Image
(Picha: Mkurugenzi wa Mradi wa Lugha za Tanzania (LOT) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Josephat Rugemalira) Wadau mbalimbali wa lugha walikutana katika warsha iliyoandaliwa na Mradi wa Lugha Tanzania(LOT) na kujadiliana kuhusu lugha za asili Tanzania. Makala hii ya Mwandishi Wetu, aliyehudhuria warsha hiyo yaeleza. Lugha za asili zimebeba maarifa mengi yaliyolimbikizwa na jamii ambapo kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa sasa kuzidumisha,kuzififisha na kuzibeza zitakufa taratibu katika kipindi cha miaka 20 ijayo. Mkurugenzi wa Mradi wa Lugha za Tanzania (LOT) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Josephat Rugemalira anasema, iwapo raia wamenyang'anywa fursa ya kutumia lugha yao kujadili sera ziletwazo kwao au kuhoji sheria zinazotungwa ili kuwadhibiti, raia hawa ni kama wanyama waliohasiwa wasiweze kujiamulia mambo yahusuyo maisha yao wala kurithisha raslimali zao kwa watoto na wajukuu. “Lugha hizi , lazima zifunguliwe milango katika sekta