Posts

Showing posts from July, 2010

Ninasoma "Siku ya Watenzi Wote"

Image
Kwa siku kadhaa sasa nimekuwa nikisomaa Siku ya Watenzi Wote , kitabu cha Shaaban Robert, ambacho nilikinunua tarehe 8 Julai pale Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu Dar es Salaam, kwa bei ya shilingi 5,000 tu. Ninapenda kusoma vitabu muhimu kama hivi vya Shaaban Robert, kama nilivyoandika katika blogu hii na katika kitabu cha CHANGAMOTO . Nimeamua kujielimisha ili niweze kuandika kwa ki-Swahili vizuri iwezekanavyo. Ni jitihada binafsi ya kujikomboa kutokana na kasumba na fikra potofu tulizo nazo wengi, hasa wasomi, kuhusu lugha ya ki-Swahili. Ninataka kuonyesha heshima kwa lugha hii kwa kuiandika kwa usahihi. Mambo mengi yaliyomo katika Siku ya Watenzi Wote yanatokea Dar es Salaam. Tunawaona wahusika wakiwa katika mitaa kama Kichwele, Ilala, Mnazi Moja, Kariakoo, na Msasani. Hii inafurahisha, kwani mwandishi anauenzi mji huu kwa kuuweka kitabuni namna hii. Inanikumbusha hadithi za mwandishi Moyez Vassanji, kama vile Uhuru Street , ambaye naye aliandika sana kuhusu Dar