Posts

Showing posts from 2009

CHANGAMOTO: Insha za Jamii

Leo nimechapisha kitabu kipya. Kinaitwa CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Ni mkusanyiko wa makala mbali mbali nilizoandika mwaka 2009, juu ya masuala ya uchumi, siasa, jamii, na utamaduni yanayoihusu Tanzania na dunia kwa ujumla. Hiki ni kitabu changu cha kwanza katika lugha ya ki-Swahili. Naamini kuwa uzoefu niliopata utanisaidia siku zijazo. Kwa kuanzia, kitabu hiki kinapatikana mtandaoni, pamoja na vitabu vyangu vingine. Bofya hapa .

KWA KINA NA PROF. JOSEPH MBELE

Ili kuwapa mwanga zaidi wasomaji wa blogu hii kuhusu fikra zangu, naleta tena mahojiano ambayo niliwahi kufanyiwa na blogu maarufu ya Bongo Celebrity . Bofya hapa .

Bia za Kuzindulia Kitabu

Miaka michache iliyopita, nilichapisha kijitabu kuhusu Things Fall Apart . Nilimtumia ujumbe rafiki yangu aliyekuwa anaishi Dar es Salaam, kuhusu kuwepo kwa kijitabu hicho, naye akaniandikia hima. Nanukuu sehemu ya ujumbe wake: Kuhusu habari ya kitabu nitajitahidi ili niweze kujulisha watu ila, naomba kitu kimoja ukija Tanzania tutafanya kitu kinachoitwa uzinduzi maana yake tutaalika waandishi wa habari jambo ambalo ni rahisi sana hapa kwetu ili mradi kinywaji kipatikane na tunaweza kualika kundi moja la mziki basi . Aliendelea kufafanua mkakati huo, ikiwa ni pamoja na kuwaalika wageni muhimu, kama vile waziri wa elimu au naibu wake. Wazo ambalo lilinata kichwani mwangu zaidi ni hili la kuandaa kinywaji. Kwa maneno mengine, nilitegemewa kununua bia nyingi. Bado sijafanya huu uzinduzi wa kufa mtu, nikinukuu usemi wa mitaani. Badala yake, najiuliza nchi yetu inakwenda wapi. Wazo la bia za kuzindulia vitabu linaelezea vizuri hali halisi ya jamii ya Tanzania. Tumefikia mahali ambapo

Wimbo wa Taifa (Tanzania)

Darasa Chini ya Mti

Image
Makala hii, inayotokana na picha inayoonekana hapa chini, ilichapishwa katika gazeti la KWANZA JAMII. Ni makala ya pili. Kusoma makala ya kwanza, bofya hapa . Darasa Chini ya Mti Na Profesa Joseph L. Mbele Nimeona picha kwenye blogu kadhaa ambayo inamwonyesha mwalimu na watoto wa darasa la kwanza, chini ya mbuyu. Ubao wa kuandikia umepigiliwa kwenye mbuyu. Kama inavyotegemewa, Watanzania wanalalamikia hali hiyo. Wanauliza kwa nini watoto wasome katika mazingira ya aina hii. Wengine, kama kawaida, wanaishutumu serikali. Napenda kuliangalia zaidi suala la darasa kufanyika chini ya mti. Je, ni balaa kama tunavyodai au kunaweza kukawa na mtazamo mwingine? Kuna vijiji na jumuia nyingi nchini mwetu ambazo hazina shule. Sababu moja ni kuwa idadi ya watu katika nchi yetu inaongezeka muda wote. Vijiji vinaenea sehemu za mbali ambazo zamani zilikuwa mapori au mashamba. Watoto wanatembea mwendo mrefu kwenda shuleni. Na kadiri watu wanavyoendelea kujenga mbali na shule, mwendo wa kutembea h

Elimu ya Kijijini

Makala hii ilichapishwa katika gazeti la KWANZA JAMII Profesa Joseph L. Mbele Mara kwa mara nakumbuka elimu niliyopata kijijini, kabla ya kuanza shule. Wengi wetu tulipitia njia hiyo. Ni elimu gani hiyo? Tangu utotoni, tulipata maelekezo kutoka kwa wazazi kuhusu mambo mbali mbali, kufuatana na umri, kuanzia namna ya kuvaa hadi namna ya kula kwa adabu na kuwasalimia watu. Baadaye wavulana tulijifunza kuchunga mbuzi na ng’ombe, na kutandika nyasi kwenye zizi la ng’ommbe, na kukamua maziwa. Wasichana walifundishwa kazi za jikoni na kulea watoto. Kama ilivyo kwa watoto wengine, baba na mama walikuwa wananituma kufanya shughuli hii au ile. Hata majirani walikuwa wanatutuma sisi watoto kuwasaidia shughuli mbali mbali. Yote hii ilikuwa ni sehemu ya elimu yetu. Nilipokua kidogo nilianza kushiriki katika kilimo. Nilijifunza kulima, kupanda, kupalilia, na kuvuna mazao. Nilijifunza kuchuma kahawa na kuishughulikia baada ya hapo. Shughuli hizi ziliniwezesha kufahamu zaidi habari za udongo, n

Utamaduni na Utandawazi

Makala hii ilichapishwa katika KWANZA JAMII . Profesa Joseph L. Mbele Tangu mwaka jana, nimekuwa naendesha warsha hapa Tanzania kuhusu utamaduni na utandawazi. Mwaka jana nilifanya hivyo Arusha, na mwaka huu nimeendesha warsha Tanga na Dar es Salaam. Warsha hizi zimehudhuriwa na watu kutoka Tanzania, Kenya, Cameroon, Uingereza, Sweden, na Marekani. Hao wa nchi za nje ni watu waliokuwepo Tanzania kwa shughuli mbali mbali. Niliamua kuanza kuendesha warsha hizi hapa Tanzania kutokana na kutambua kuwa ni muhimu katika dunia ya leo inayozidi kuwa kijiji. Watu wa tamaduni mbali mbali wanazidi kukutana kwa sababu mbali mbali, kama vile biashara, masomo, utalii, na uwekezaji. Watu wa tamaduni mbali mbali wanajikuta wakifanya kazi pamoja viwandani, maofisini, na kadhalika. Wanafunzi, watafiti, na walimu, wanajikuta wakishughulika na watu wa tamaduni mbali mbali. Hali hii inaweza kusababisha migogoro ya aina aina, kwani kila mtu ana namna yake ya kuongea, kufikiri, kufanya mambo, ambayo inat

Maprofesa Hatuvunji Msitu, ni Mwalimu wa Shule ya Msingi

Image
Picha hii ilichapishwa tarehe 15 Novemba katika blogu ya Haki Ngowi , pamoja na maelezo haya: Mwalimu, Albert Juakali wa shule ya msingi Iboma iliyopo kijiji cha Udinde Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya Mti wa Mbuyu kama alivyokutwa na Mpigapicha wetu. Picha na Brandy Nelson Nina mengi ya kusema kuhusu picha hii. Kwa leo napenda kumwongelea huyu mwalimu, kwa kuirejesha makala yangu iliyotokea katika gazeti la KWANZA JAMII . Maprofesa hatuvunji msitu, ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Na Profesa Joseph L. Mbele TUNAONGELEA sana mfumo wa elimu. Kitu kimoja ninachoona hatukizungumzii ipasavyo ni wadhifa wa mwalimu wa shule ya msingi. Jamii haimwoni mwalimu wa shule ya msingi kama mtu wa pekee sana. Lakini, akitokeza mwalimu wa chuo kikuu, kama mimi, jamii inafungua macho na kutega masikio. Jamii inamwona mwalimu wa chuo kikuu, profesa, kuwa mtu wa pekee sana, kumzidi mwalimu wa shule ya msingi. Kwa miaka kadhaa sasa, nimejjijengea mtazamo t

Ziara Katika Shule ya Sayansi ya Mazingira

Image
Kwa miaka yapata kumi, nimekuwa nikialikwa kila mwaka kwenda kwenye shule ya sayansi ya mazingira mjini Apple Valley, Minnesota, kutoa mhadhara kwenye somo la falsafa za jadi na mazingira. Mimi kama mtafiti wa masomo yahusuyo masimulizi na falsafa za jadi na utamaduni kwa ujumla, nimetumia fursa hii kuwaeleza wanafunzi namna binadamu, tangu mwanzo wake hapa duniani, alivyoweza kuyatafakari, kuyatathmini na kuyaelezea mazingira. Tangu enzi za mwanzo binadamu aliunda lugha kama chombo mahsusi cha kumwezesha kufanya yote hayo. Uundaji wa lugha halikuwa jambo rahisi, tangu kuvipa majina viumbe na vitu vyote vilivyomzunguka hadi kusema na kuelewana na binadamu wengine. Kila mwaka, mwalimu Todd Carlson, ambaye amekuwa akinialika, anawaelezea wanafunzi kuhusu utafiti wangu juu ya fasihi simulizi na falsafa za jadi, na anawasomesha kitabu changu cha Matengo Folktales . Hadithi, nyimbo na semi ni baadhi ya mikondo aliyotumia binadamu kuyaelezea mazingira yake na kukidhi duku duku ya akili ya

Watanzania jitokezeni kwenye mijadala ya elimu

Habari hii imechapishwa katika gazeti la Habari Leo Imeandikwa na Na Simon Nyalobi; Tarehe: 7th November 2009 WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kuandika machapisho ya utafiti wao na kujitokeza katika mijadala ya kimataifa kuhusu elimu badala ya kuogopa na kukaa pembeni. Mwito huo ulitolewa jana Dar es Salaam na Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Oxfam tawi la Tanzania, Mary Soko wakati wa akifunga warsha ya siku tatu ya Jumuiya ya Utendaji wa Elimu nchini iliyokuwa na washiriki 40 kutoka maeneo mbalimbali nchini. Soko alisema kuwa Wataznania wengi hawajitokezi katika makongamano ya kimataifa kuonesha utafiti wao ikilinganishwa na mataifa mengine hususani Nigeria ambayo raia wake hujitokeza kila kongamano la usomaji wa vitabu linapotokea. Alisema kuwa hata makongamano yanayofanyika hapa nchini, hayana muamko kwa kuwa watanzania wengi wamekuwa nyuma kushiriki. Kutokana na hali hiyo, amewataka sasa kujitokeza kila yanapotokea makongamano ya usomaji wa vitabu ili kuiweka nchi

Vitabu Bila Karatasi

Kitu kimoja ambacho kinampambanua mwanadamu na viumbe wengine ni tekinolojia. Chimbuko la binadamu lilifungamana na uwezo wake wa kutengeneza na kutumia zana mbali mbali, kuanzia zana za miti na mawe, hadi chuma na leo zana zinazoendeshwa na umeme au nguvu za nyuklia. Katika maendeleo haya ya tekinolojia, binadamu amegundua na kuweza kutumia nishati mbali mbali, kama vile maji, upepo na jua. Uandishi na uchapishaji vimefungamana na maendeleo ya tekinolojia. Tangu binadamu wa kwanza alivyoandika michoro kwenye miamba au kuta za mapango, kwenye ngozi za wanyama, vibao vya udongo, au karatasi, yote hayo ni matunda ya tekinolojia. Leo kuna mashine na mitambo ya aina aina ya kuchapisha magazeti na vitabu. Maendeleo ya tekinolojia ya uchapishaji yametufikisha mahali ambapo uchapishaji sasa unaweza kufanyika bila karatasi. Vitabu vinaandikwa na kusomwa bila kutumia karatasi, bali kwa mtindo wa digitali. Kwa mtindo huu wa digitali, mtu anaandika kitabu chake kwa kutumia kompyuta, na anakihif

Tutajengaje Utamaduni wa Kusoma Vitabu?

Leo asubuhi nilienda kwenye mji wa Brooklyn Park, Minnesota, kuhudhuria kikao cha kamati inayojishughulisha na masuala ya kujenga na kuboresha mahusiano baina ya waAfrika na waMarekani Weusi. Baada ya kikao, wakati narudi kwenye mji ninapoishi, nilipita kwenye mji wa Apple Valley, nikaingia katika duka la vitabu la Half Price Books. Ni duka ambalo nimelitembelea mara nyingi. Half Price Books ni mtandao mkubwa wa maduka ya vitabu hapa Marekani, ambao una maduka katika miji mingi kama inavyoonekana hapa . Kama kawaida, ninapoingia katika maduka ya vitabu hapa Marekani, nawakuta watu wa kila aina wakizungukazunguka kutafuta vitabu, wakivisoma, na wakivinunua. Kuna maduka mengi ya vitabu hapa Marekani ambamo watu wanaleta vitabu vyao kuviuza, na wengine wanakuja kununua. Unaweza kuja kuuza vitabu vyako na kununua vitabu vingine. Nimewahi kufanya hivyo. Maduka ya Half Price Books yanafuata mtindo huo. Kwa hivi, daima utawaona watu wakija na mifuko au makasha ya vitabu vya kuuza, wakati huo

Kijitabu Kuhusu "Things Fall Apart"

Riwaya ya Chinua Achebe, Things Fall Apart , inafahamika duniani kote. Inatumika sana mashuleni. Mimi kama mwalimu wa fasihi nimefundisha riwaya hii kwa miaka mingi, hadi nikaandika mwongozo kwa wasomaji, wanafunzi, na walimu. Mwongozo huu ni kijitabu ambacho kinapatikana mtandaoni. Bofya hapa . Lakini, kama watu wasemavyo, tunakwenda na wakati. Tarehe 1 Novemba, 2009 nimekichapisha kijitabu hiki kama "e-book." Yeyote mwenye kifaa kiitwacho "e-reader," au "e-book reader," anaweza kukiingiza katika kifaa hicho, akakisoma. Bofya hapa .

Tanzania --Twanga Pepeta -- Watoto

KWANZA JAMII limetua Mwanza

Image
Gazeti la KWANZA JAMII linapatikana Mwanza, kwa mujibu wa picha hizi zilizotoka katika blogu ya Mjengwa tarehe 29 Oktoba, 2009 na 30 Oktoba, 2009 . Nami napenda kufuatilia maendeleo ya gazeti hili.

KWANZA JAMII Mikumi

Image
Picha hii imechapishwa tarehe 28 Oktoba, 2009, katika blogu ya Mjengwa . Maggid Mjengwa amepiga picha hii Mikumi. Mimi kama mwandishi katika gazeti la KWANZA JAMII nafurahi kuona gazeti hili, ambalo bado changa, linavyojikongoja na kuendelea kuenea nchini, hadi kwenye miji midogo na vijijini. Siku chache zilizopita tulipata habari za KWANZA JAMII kufika kijijini Roya. Bofya hapa . Kama wahenga walivyosema, pole pole ya kobe humfikisha mbali.

Warsha Dar es Salaam: Utamaduni na Utandawazi

Image
Tarehe 5 Septemba, mwaka huu, niliendesha warsha Dar es Salaam, kuhusu Utamaduni na Utandawazi. Warsha hii iliandaliwa na Tanzania Discount Club. Siku chache kabla, tarehe 29 Agosti, niliendesha warsha nyingine Tanga, kuhusu Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo. Warsha hii, ambayo ilihudhuriwa na watu wa mataifa mbali mbali, nimeiongelea kidogo hapa na hapa . Warsha hii ya Dar es Salaam ilinipa fursa ya kukutana na waTanzania kutoka sekta binafsi, taasisi mbali mbali na Ubalozi wa Marekani. Warsha ilidumu kuanzia saa nne na nusu asubuhi hadi saa 11 jioni. Sehemu ya kwanza ilihusu masuala ya jumla: dhana ya utamaduni, kama nilivyoielezea katika kitabu changu Africans and Americans , na dhana ya utandawazi. Kwa mtazamo wangu, utandawazi ni jambo ambalo lilianza zamani kabisa, pale binadamu wa mwanzo walivyosambaa duniani wakitokea Afrika Mashariki. Hapo ndipo utandawazi ulipoanzia, na baada ya hapo, kumekuwa na aina na awamu mbali mbali za utandawazi, hadi kufikia zama zetu hizi, amba

Mwalimu Angerudi Leo Angejisikiaje?

Makala hii imechapishwa katika KWANZA JAMII, Oktoba 13-19, 2009 Profesa Joseph L. Mbele Imetimia miaka kumi tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipofariki London, Oktoba 14, 1999. Ni jambo jema kutumia muda huu kumkumbuka kwa namna ya pekee, kwa mchango wake kwa Tanganyika (na baadaye Tanzania), Afrika na dunia kwa ujumla. Ni vizuri pia kutumia muda huu kutafakari mwenendo wa nchi yetu, tukilinganisha na makusudio aliyokuwa nayo Mwalimu wakati wa uhai wake. Mchango wa Mwalimu katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika unatambulika. Akishirikiana na viongozi wengine wa sehemu mbali mbali za nchi, wa dini na rangi mbali mbali, na wananchi kwa ujumla, Mwalimu Nyerere aliongoza Tanganyika kufikia Uhuru, Desemba 9, 1961. Hapo alitoa hotuba ambayo maneno yake ni vigumu kusahaulika, kwa jinsi yalivyoelezea kwa ufasaha hisia na matumaini ya Taifa letu changa. Mwalimu alisema, “Sisi tunataka kuwasha mwenge, na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, ili umulike hata nje ya mipaka yetu,

Tamasha la Vitabu, Minneapolis, 2009

Image
Jana, tarehe 10 Oktoba, nilishiriki tamasha la vitabu mjini Minneapolis. Tamasha hili hufanyika kila mwaka mara moja. Nimeshahudhuria mara kadhaa miaka iliyopita, lakini hali ni mpya kila mwaka. Kwa mfano, waandishi maarufu wanaoalikwa kama wageni rasmi huwa tofauti kila mwaka. Pia, pamoja na kuwa baadhi ya waandishi na wachapishaji na wauza vitabu huja mwaka hadi mwaka, wako pia wengi ambayo ni wapya. Hapo juu mbele kabisa ni mezani pangu. Baadhi ya vitabu vyangu vinaonekana. Watu wanawahi, na milango ukumbi wa maonesho inapofunguliwa, saa nne asubuhi, ukumbi unafurika watu. Siku nzima hali ni hiyo hiyo; kuna msongamano wa watu wakiwa wanaangalia na kununua vitabu, wakiongea na waandishi na wachapishaji, na kadhalika. Waandishi wa kila aina wanakuwepo, wake kwa waume, wazee kwa vijana. Siku hizi wengi wanachapisha vitabu vyao kwa kutumia fursa zitokanazo na maendeleo ya tekinolojia, bila kupitia kwa wachapishaji kama ilivyokuwa zamani. Kila mtu anaweza kutumia tekinolojia hiyo ya k

Uraia wa nchi Mbili

Makala hii imechapishwa katika KWANZA JAMII, Oktoba 6-12, 2009 Profesa Joseph L. Mbele Tarehe 4 Septemba, 2009, nilipata fursa ya kukutana na ndugu Muhiddin Issa Michuzi, mwanablogu maarufu Tanzania. Pamoja na maongezi kuhusu masuala mbali mbali, alinifanyia mahojiano mafupi kwa ajili ya kuweka kwenye blogu yake. Suali moja aliloniuliza ni kuhusu msimamo wangu juu ya suala la uraia wa nchi mbili. Nilijibu kifupi, kutokana na uchache wa muda. Lakini suali hili limekuwa mawazoni mwangu kwa miaka kadhaa, tangu lilipoanza kuongelewa na waTanzania. Nilimweleza Ndugu Michuzi kuwa binafsi sitaki uraia wa nchi nyingine. Nilililelewa katika misingi ya kujitambua kuwa mimi ni mTanzania tu. Isipokuwa, nilisema kuwa watoto wa siku zijazo, watakuwa waishi katika dunia tofauti na yetu, na itakuwa dunia ambayo itakuwa imefungamana sana na kuwa kama kjiji. Hata mipaka ya nchi huenda haitakuwepo, wala nchi hazitakuwepo. Kwa hivi suala la uraia nalo litakuwa na sura tofatuti. Tukiacha suala la hisi

Sea--Papi Kocha, Nguza Viking

Diwani--"KWANZA JAMII Limefika Roya!"

Image
( Taarifa hii imechapishwa katika blogu ya Mjengwa tarehe 4 Oktoba, 2009. Nikiwa ni mwandishi mmojawapo wa KWANZA JAMII, nafurahi jinsi gazeti hili linavyojitahidi kuingia vijijini. Hata kijijini kwangu, Wilaya ya Mbinga, linafahamika ) Mchana huu Diwani wa Kata ya Roya Bw. Emmanuel Kigodi amempigia simu mwandishi wa KWANZA JAMII Victor Makinda kumjulisha kuwa nakala nne za KWANZA JAMII zimemfikia. Gazeti hilo limebeba habari kubwa ukurasa wa mbele yenye kuhusiana na ujambazi uliotokea kwenye kata hiyo hivi karibuni. Kwa mujibu wa Diwani Kigodi, gazeti hilo la KWANZA JAMII sasa limekuwa gumzo kijijini Roya na linazunguka kwa wanakijiji wenye hamu ya kusoma habari zake!

CUF Yaongelea Njama za CCM

Warsha: "Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo," (Tanga, Agosti 29)

Image
Tarehe 29 Agosti niliendesha warsha Tanga, Tanzania, mada ikiwa ni "Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo" . Warsha hii ilifanyika katika kituo kiitwacho Meeting Point Tanga na ilidumu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Hapo juu anaonekana Mama Ruth Nesje, mkurugenzi wa kituo, akinitambulisha kwa washiriki wa warsha. Niliamua kufanya warsha hii kutokana na uzoefu wangu wa kuelezea masuala haya ya utamaduni kwenye vyuo, taasisi, makampuni, makanisa, jumuia mbali mbali na watu binafsi huko Marekani. Warsha hii ilikuwa na mvuto mkubwa kwa washiriki na iliamuliwa kuwa zifanyike warsha hizi siku zijazo. Kitu kimoja kilicholeta msisimko na mjadala mkubwa ni makala yangu "Maendeleo ni Nini?" Ninapangia kuandika zaidi kuhusu warsha hii, na nyingine ambayo niliendesha Dar es Salaam tarehe 5 Septemba, ila nimeona niweke hii taarifa fupi hapa, kwa sasa. Kama kianzio, nimeweka picha chache zilizopigwa siku hiyo. (Photos by Vesla Eriksen)

Nimeonana na Mheshimiwa Michuzi

Image
Tarehe 4 Septemba, 2009 ilikuwa siku maalum kwangu, kwani nilipata bahati ya kuonana na gwiji wa blogu, Mheshimiwa Michuzi ofisini kwake pale Mtaa wa Samora, Dar es Salaam. Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuonana na gwiji huyo. Tuliongelea mambo mengi yahusuyo blogu na mawasiliano ya kisasa kwa ujumla. Kwa mfano, alikumbushia mkutano wa wanablogu unaopangwa kufanyika Dar es Salaam mwezi Desemba mwaka huu. Nilimwona Michuzi kuwa mtu mwenye hamu ya kuona maendeleo. Hasiti kutoa ushauri wa kuwasaidia wengine. Alisema kuwa anapitia blogu nyingi, na hapo akaniambia kuwa picha iliyopo kwenye blogu yangu si nzuri. Hapo hapo aliniambia nisimame na akanipiga picha nikaiweke kwenye blogu. Michuzi anaheshimu taaluma yake na anapenda kuona wanablogu wanasukuma mbele gurudumu la mawasiliano hayo kwa kila mmoja kutafuta kipengele maalum na kukiendeleza, iwe ni taaluma, burudani, na kadhalika. Michuzi alisema, kwa mfano, si kila mmoja anaiweza shughuli ya mwanahabari. Tuliongelea mengi, na pi

Simlaumu JK kwa kuzunguka duniani

(Makala hii imechapishwa katika KWANZA JAMII, Agosti 18-24, 2009) Profesa Joseph L. Mbele Katika makala zangu za hivi karibuni, nimegusia suala la kuiga mambo, kama vile mashindano ya urembo na suala la vyama vya siasa. Inaonekana suala hili litahitaji kushughulikiwa tena na tena. Katika makala yangu moja, niliongelea safari za JK nchi za nje, na baadhi ya watu walilalamika kuwa JK anasafiri mno. Walikumbushia kuwa viongozi wa nchi zingine za jirani, kama vile Kenya, hawasafiri hivyo, lakini nchi zao zinapiga hatua kutuzidi. Hitimisho likawa kwamba JK awaige viongozi hao; atumie muda mwingi nchini badala ya nje. Wazo kuwa JK afanye kama wanavyofanya viongozi wa nchi zingine linahitaji tafakari. Napenda kuliongelea wazo hilo, kwa kutumia mfano huo wa Kenya na Tanzania. Je, kiongozi wa Tanzania anaweza kuiendeleza Tanzania kwa kuiga anayofanya kiongozi wa Kenya? Tanzania inaweza kuendelea kwa kuiiga Kenya? Tanzania ni nchi yenye upekee. Kenya nayo ina upekee wake. Hizi nchi mbili zin

Tunahitaji Vyama vya Siasa?

(Makala hii imechapishwa katika KWANZA JAMII, Agosti 11-17, 2009) Profesa Joseph L. Mbele Jamii yetu, kama jamii zingine, inatafuta namna ya kujenga na kuimarisha demokrasia. Katika harakati hii, uamuzi ulifikiwa kwamba tuwe na vyama vya siasa, badala ya chama kimoja. Vyama vya siasa vinapiganiwa karibu kila mahali kwa imani kuwa ni njia muhimu ya kujenga demokrasia. Kama kuna nchi isiyo na vyama vya siasa, utawala wa nchi hiyo unahesabiwa kuwa si wa kidemokrasia. Kwa maana hii, kuuliza kama tunahitaji vyama vya siasa inaonekana ni upuuzi. Lakini mimi sioni kama ni suali la kipuuzi. Demokrasia ni nini? Ni aina ya utawala ambamo umma umeshika hatamu. Demokrasia ni utawala unaowakilisha na kuendeleza matakwa na maslahi ya umma. Hii ndio maana ya demokrasia. Dhana ya vyama haiko kwenye tafsiri hii, kwani sio msingi au uhai wa demokrasia. Ni namna gani demokrasia inaweza kujengwa? Ili demokrasia iwepo, ni lazima kuwe na vyama? Haya ndio masuali ya kujiuliza. Huko Ulaya, katika histor

Je, Tunaweza Tukawa na Mrembo wa Tanzania?

(Makala hii ilichapishwa katika KWANZA JAMII, Agosti 4, 2009) Profesa Joseph L. Mbele Kwa wiki kadhaa nimewazia kuandika makala kuhusu mashindano ya urembo. Katika Tanzania ya leo, mashindano hayo yameshamiri katika miji mikubwa na yanazidi kuenea. Kwa upande moja nimekuwa sipendezwi na mashindano hayo. Nimekuwa nikijiuliza kama yana maana gani katika jamii yetu, kwani ni wazi kuwa mwenendo wake ni wa kuigwa kutoka nchi za magharibi. Ninayachukulia kama ishara nyingine ya ukoloni mambo leo. Kwa upande mwingine, nimelazimika kukubali kuwa yamesaidia kwa namna mmoja au nyingine kuitangaza nchi yetu, wakati washiriki wanapoenda nje wakiwa na bendera ya nchi yetu. Vile vile, washindi wa mashindano hayo wameweza kufanya mambo ya maana katika jamii yetu. Wamekuwa watu maarufu nchini, wenye mvuto na uwezo wa kuhamasisha shughuli mbali mbali za manufaa kwa jamii. Wengine wameweza kujijengea msingi wa kujiendeleza kimaisha, kama vile kuwa wanamitindo katika nyanja za kimataifa. Hayo nimeya

Warsha: "Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo," (Tanga, Agosti 29)

Image

Nilivyoenda Zanzibar na Pemba Kuwaongelea Wamarekani

Image
Tarehe 16 Machi, 2005, nilipata barua pepe kutoka Ubalozi wa Marekani Tanzania. Ujumbe ulikuwa ni ombi kama nitakapokuwa Tanzania nitaweza kutoa mihadhara kwa waTanzania kuhusu utamaduni na jamii ya Wamarekani. Ujumbe ulifafanua kuwa itakuwa ni juu yangu kuamua nini cha kuongelea: mazuri, mabaya, hata mabaya kabisa. Nilikubali ombi hilo. Nilipofika Tanzania, niliwasiliana na Ubalozi, na maandalizi yalifanyika, kuniwezesha kwenda Zanzibar na Pemba, tarehe 15 na 16 Agosti, 2005. Matangazo yalitayarishwa na kubandikwa sehemu mbali mbali Zanzibar na Pemba. Nilisindikizwa kwenye ziara hii na Bwana David Colvin, ofisa utamaduni katika Ubalozi wa Marekani. Yeye ndiye aliyekuwa ananitambulisha kwa wenyeji wangu, kwani alikuwa amewazoea. Mhadhara wa kwanza ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Walikuja watu wengi. Kwa bahati nzuri baadhi nilikuwa nawafahamu, tangu walipokuwa wanafunzi wangu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Walikuwepo pia wanafunzi kutok