Wimbo wa Taifa (Tanzania)

Comments

Nahisi baba/mlezi wa huyu mtoto ni "Mswahili". Kwa vyo vyote vile, anastahili pongezi kwa juhudi zake za kumfundisha binti yake wimbo huu mzuri wa taifa letu. Si jambo rahisi kwa watoto waliozaliwa/kukulia huku ughaibuni kujifunza mambo ya utamaduni wa wazazi wao kule nyumbani. Nimezipenda hizi juhudi. Pengine nami nitaanzisha kwaya ya hawa mabinti zangu hivi karibuni - niwafundishe kuimba huu wimbo na nyimbo zinginezo za Kisukuma.

Wimbo pekee wa Kiswahili ambao wanaufahamu ni "simama kaa, simama kaa,...." Nimeipenda hii video!
Mbele said…
Profesa Matondo, hata mimi nilifurahishwa sana na juhudi ya bwana huyu kukafundisha katoto kadogo namna hii, hadi kaweze kuimba vizuri hivi. Niliona ni ajabu, kwa kweli, na niliguswa sana. Halafu, anavyokashangilia haka katoto hapa mwishoni, naona anakajenga katika njia ya kujiamini. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa bwana huyu.
Kusema kweli wimbo wetu wa Taifa ni rahisi sana kujifunza wanangu hawawezi kuomba wimbo wa taifa wa hapa lakini wanaweza kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania. najivuna sana na wanaueneza shuleni kwao kkwa kuwafundisha watoto wenzao. Ahsante kwa kuigundua hii video.
John Mwaipopo said…
hivi huu ni wimbo wa taifa letu au ni wimbo wa taifa la afrika kusini kwa kiswahili?
Anonymous said…
Matatizo ya wengi wetu tulio Ughaibuni hasa hapa USA nimegundua hutuwafundishi watoto wetu Kiswahili,ukweli tunawatia Umasikini watoto wetu tuige mfano wa watoto wa Kispenishi na Wahindi.Kujua lugha zaidi ya moja ni muhimu sana hasa uliyo na Asili nayo.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini