Posts

Showing posts from June, 2009

Makala ya "Kwanza Jamii" Yachapishwa Marekani

Wiki kadhaa zilizopita, nilipata mwaliko kutoka kwa Ndugu Maggid Mjengwa, kuwa niandike makala katika gazeti lake jipya la Kwanza Jamii . Nilikubali, na niliandika makala ya kwanza yenye kichwa "Maendeleo ni Nini?." Makala hii ilichapishwa mwezi Aprili, 2009. Siku moja, katika maongezi na Mmarekani Mweusi mmoja katika mji wa Minneapolis, nilimwambia kuwa nimeanza kuandika makala za kiSwahili katika gazeti moja la nyumbani Tanzania. Kwa vile alikuwa na duku duku ya kujua zaidi kuhusu makala hizo, nilimweleza kuhusu makala yangu hiyo ya kwanza. Huyu Mmarekani tulikuwa tumefahamiana kwa wiki kadhaa, tukiwa katika shughuli za kuandaa tamasha la utamaduni wa kiAfrika, liitwalo Afrifest . Alivutiwa na mada na mtazamo wa makala, akasema ingefaa kuchapishwa katika gazeti la mtandaoni ambalo yeye na watu wengine walikuwa wanaliandaa. Alisema kuwa mawazo niliyoandika kuhusu maendeleo yatawafaa watu wa Marekani pia, kama vile waMarekani Weusi, ambao nao wamepitia msukosuko wa kutawali

Dala dala: Katuni ya Fadhili

Image
Sijawahi kuwa na gari wala kuendesha gari Tanzania, ingawa mara kwa mara ninakuwa hapo. Nikiwa mahali kama Dar es Salaam, usafiri wangu ni kwa mguu au dala dala. Mara moja moja natumia teksi. Katuni hii, ambayo imetoka kwa Michuzi , imenigusa kwa ujumbe wake na namna yake ya kuyaelezea matatizo halisi kwa namna ya mchapo. Hii ni staili ambayo naipenda katika baadhi ya maandishi yangu. Nategemea sana kuwa msanii huyu atakusanya katuni zake na kuchapisha kitabu au vitabu, aweze kuvuna matunda ya kazi yake ambayo ni ngumu. Wasanii wetu wanafanya kazi kubwa sana kwa manufaa ya jamii, lakini wanahujumiwa haki zao na jamii. Nikiwa mwandishi, mwenye haki juu ya kazi zangu sawa na hao wasanii wetu, nawapigia debe ili wafaidike na kazi zao.

Nauza Vitabu Vyangu

Image
Leo nimeona niandike kuhusu jinsi nilivyoanza kuuza vitabu vyangu. Naamini habari yangu itawasaidia waandishi wengine. Mimi ni mwalimu, mtafiti, na mwandishi. Nimeshachapisha vitabu kadhaa. Lakini napenda niongelee vitabu viwili: Matengo Folktales na Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Nilichapisha Matengo Folktales mwaka 1999 hapa Marekani. Lazima nikiri kuwa mara baada ya kitabu kutoka, sikuwa na furaha sana. Ingawa nilikuwa nimetumia yapata miaka 23 kukiandaa kitabu hiki, na ingawa kutokana na ujuzi wangu wa taaluma hii nilijua kuwa ni kitabu muhimu, sikuwa na raha kilipotoka mtamboni. Kwa namna isiyoelezeka, nilijiuliza kama watu watakionaje. Vile vile nilifahamu kuwa, ingawa nilikuwa nimechoka kabisa kukiboresha kitabu hiki, kama ningeendelea kukishughulikia, ningeweza kukiboresha zaidi. Uandishi ndivyo ulivyo. Huwezi ukafikia hatua ya kusema kitabu chako kimekamilika, hakina upungufu wowote, na hakiwezi kuboreshwa zaidi. Hata hivi, wasomaji walipoanza

Binadamu Amnyonyesha Mnyama

Image
Picha hii, iliyotokea tarehe 8 Juni, 2009, kwa Mjengwa , ya mama anayemnyonyesha mwanawe upande mmoja na mnyama yatima upande mwingine imenivutia na inanifikirisha. Wengi wetu labda tutashangaa na kujiuliza kama huyu mama ana akili timamu. Lakini nadhani huyu mama anatufundisha au kutukumbusha mengi. Ni mama mwenye upendo na huruma. Habari hiyo hapa juu inasema kuwa huyu mama alikuwa anawalea watoto wake sambamba na huyu mnyama. Watoto na mnyama walikuwa wanacheza pamoja bila shida, na wakati wa kunyonyesha, mama anawanyonyesha wote kama inavyoonekana katika picha. Laiti nasi tungevipenda viumbe vyote namna hiyo hiyo. Lakini kwa wengi wetu, hata kuwapenda binadamu wenzetu tu ni shida. Uhasama, vita na magomvi hayaishi. Huko tulikotoka, binadamu na wanyama tulikuwa pamoja, bila utengano. Pole pole kiumbe kinachoitwa binadamu kilibadilika na kuwa hivyo kilivyo leo. Lakini msingi wa maumbile yetu na wanyama wengine ni ule ule. Kama sisi wanadamu tunaweza kunywa maziwa y

Vijimambo vya Nathan Mpangala

Image
Nimeipenda katuni hii, iliyowekwa tarehe 10 Juni, 2009 kwenye blogu ya Michuzi

Viumbe "Anonymous" Katika Blogu

Kila anayepitia blogu mbali mbali atakuwa anaona maandishi yaliyoandikwa na viumbe viitwavyo "Anonymous." Mwanzoni, nilikuwa sioni ajabu wala kufikiria suala la viumbe hivi. Lakini, siku za karibuni, nimeanza kuvifikiria. Ninapoona ujumbe umeandikwa na "Anonymous" huwa sioni sababu ya kujibu, kwani sielewi ni kiumbe gani kilichoandika, kama ni binadamu au mzimu. Na hata kama ni binadamu, sielewi kama ni jirani yangu au rafiki, ni mtu anayenifahamu au hanifahamu, na kadhalika. Halafu, nikiviwazia hivi viumbe, suala zima la mijadala linakuwa kama sinema au hadithi ya ajabu ya Ughaibuni, ilivyoandikwa na Shaaban Robert katika kitabu chake cha Adili na Nduguze . Ninapoona mlolongo wa maandishi kutoka kwa "Anonymous," nitajuaje kama ni "Anonymous" tofauti, au ni yule yule mmoja anatuchezea akili? Ni mambo ya Ughaibuni kabisa. Ni rahisi sana kwa "Anonymous" yule yule kuandika tena na tena, akitoa hoja mbali mbali, na sisi wasomaji tusigu

Safari za JK Nje ya Nchi

Makala hii imechapishwa katika Kwanza Jamii . Profesa Joseph L. Mbele Leo nimeamua kuongelea safari za Rais Kikwete, maarufu kama JK, katika nchi za nje. Suala hili linazungumzwa sana na waTanzania. Wako wanaodai kuwa JK anatumia muda mwingi mno nje ya nchi badala ya kubaki nchini na kushughulikia masuala ya nchi. Wako wanaodai kuwa JK anaenda kuomba omba misaada. Wengine wanasema kazi ya kuzunguka nje ni ya waziri wa mambo ya nchi za nje, na kwamba kwa vile JK alizoea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, bado hajabadilika, hata baada ya kuwa rais. Basi, kila mtu anasema yake, nami nimeona nichangie. Naanza kwa kukiri kuwa nchi ya nje ninayoifahamu kuliko zote ni Marekani. Nimeishi na waMarekani katika nchi yao kwa miaka mingi, nikiwafundisha na kujumuika nao kwa namna mbali mbali. Naweza kusema nawafahamu, na suala la safari za JK katika nchi za nje, naweza kuliongelea kwa kutumia mfano wa Marekani. Rais Kikwete ameshatembelea Marekani mara kadhaa, tangu awe rais. Binafsi, naona