Tuesday, June 23, 2009

Dala dala: Katuni ya Fadhili

Sijawahi kuwa na gari wala kuendesha gari Tanzania, ingawa mara kwa mara ninakuwa hapo. Nikiwa mahali kama Dar es Salaam, usafiri wangu ni kwa mguu au dala dala. Mara moja moja natumia teksi. Katuni hii, ambayo imetoka kwa Michuzi, imenigusa kwa ujumbe wake na namna yake ya kuyaelezea matatizo halisi kwa namna ya mchapo. Hii ni staili ambayo naipenda katika baadhi ya maandishi yangu.

Nategemea sana kuwa msanii huyu atakusanya katuni zake na kuchapisha kitabu au vitabu, aweze kuvuna matunda ya kazi yake ambayo ni ngumu. Wasanii wetu wanafanya kazi kubwa sana kwa manufaa ya jamii, lakini wanahujumiwa haki zao na jamii. Nikiwa mwandishi, mwenye haki juu ya kazi zangu sawa na hao wasanii wetu, nawapigia debe ili wafaidike na kazi zao.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Dar kazi kwelikweli maana hiyo foleni. kama unataka kuwahi ofisini basi ondoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi.

Bennet said...

Njia kama za mbagala huwezi kupanda ukiwa na laptop na tai namna hiyo, kule lazima uwe na jeans na fulana tena ikiwezekana uwe na nguo ya kubadilisha ukifika ofisini maana hii uliyo vaa kwenye daladala itafika ikiwa chafu na imekunjamana

Kuna jamaa baada ya kushuka kajikuta mguu mmoja kabadilishana na mtu mwingine kiatu kwa kandambili bila kujijua hahahha (lol)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...