Posts

Showing posts from October, 2013

Nimepata Wageni Leo

Image
Leo nimepata bahati ya kutembelewa na wageni wawili. Mmoja ni Mchungaji John Mhekwa kutoka Tungamalenga, Iringa. Mwingine ni Profesa Paula Swiggum wa chuo cha Gustavus Adolphus , St. Peter, Minnesota. Mchungaji Mhekwa hatukuwa tunafahamiana, lakini Profesa Swiggum tumefahamiana kwa miaka kadhaa, kwani katika programu yake ya kupeleka wanafunzi Tanzania, alinialika kuongea nao kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni, kama maandalizi ya safari. Wanafunzi walikuwa wanasoma kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Huo ulikuwa ni uamuzi wake. Mazungumzo yangu na hao wanafunzi yalihusu mambo niliyoandika katika kitabu hiki. Baada ya Profesa Swiggum kustaafu, profesa aliyemrithi, katika kuendesha programu hiyo, Barbara Zust, aliendelea na utaratibu huo . Kifupi ni kwamba Profesa Swiggum tumeanza zamani kiasi kushirikiana katika nyanja hizo. Leo ilikuwa fursa ya pekee ya kufahamiana na huyu mgeni mwingine, Mchungaji Mhekwa. Nimemwambia kuwa Tungamalenga

Tamasha la Vitabu Twin Cities, Oktoba 12, Lilifana

Image
Tamasha la vitabu, Twin Cities Book Festival , lililofanyika mjini St. Paul, Minnesota, jana, tarehe 12, lilienda vizuri. Niliondoka mapema asubuhi, yapata saa mbili, nikafika kwenye maaonesho saa tatu. Sikuwa nimechelewa, kwani wakati naandaa vitabu vyangu kwenye meza yangu, wengine nao walikuwa wakiandaaa, ingawa wengi walishapanga vitabu vyangu siku iliyotangulia Meza niliyopata, baada ya kulipia dola 80, ilikuwa namba 12. Nilikuwa nimejisajili kwa jina la Africonexion , ambayo kampuni yangu ndogo inayohusika na uchapishaji na uuzaji wa vitabu vyangu, na pia kuratibu mihadhara yangu ya kuchangia maelewano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali. Tangu nilipoisajili kampuni hii, shughuli zake zimekuwa zikifanyika zaidi hapa Marekani, lakini hatimaye, hasa nitakaporejea Tanzania baada ya kustaafu hapa Marekani, nataka kuijenga kampuni hii Tanzania, Africa Mashariki, na sehemu zingine.   Kama kawaida, watu walianza kuingia ukumbini tangu milango ilipofunguliwa. Ukiwaanga

Vijana Washikwa Mtwara Wakiwa Katika Mafunzo ya Al Shabaab na Al Qaida

Image
  Stori ambayo ilishika namba 1 kwenye habari 10 za AMPLIFAYA ya Clouds FM October 7 2013 ni hii ya Polisi Mtwara kukamata vijana 11 ambao walikua wakifanya mazoezi ya kijeshi waliyokua wakijifunza kutoka kwenye cd za magaidi zilizokua na mafunzo kutoka kwa makundi ya Al Shabaab na Al Qaeda. Taarifa zaidi unaweza kuzisoma hapo chini kwenye hiyo taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi. CHANZO: dj sek 0 comments: Post a Comment

Tamasha Kubwa la Vitabu, Twin Cities, Oktoba 12

Lile tamasha maarufu kabisa la vitabu ambalo limefanyika mjini Minneapolis kwa miaka mingi, mara moja kwa mwaka, limekaribia kabisa. Kuanzia mwaka jana, tamasha limehamia mjii St. Paul, kwenye viwanja vya State Fairgrounds. Hakuna tamasha kubwa zaidi ya hili katika eneo hili la Minnesota na majimbo ya jirani. Wanahudhuria watu yapata 7,000, wapenzi wa vitabu. Wanakuwepo waandishi, wachapishaji, wahariri, wachora picha za vitabuni, wahakiki, wauzaji wa vitabu na majarida. Wanahudhuria wazee, watu wazima, vijana, na watoto. Nimeshiriki tamasha hili kwa miaka mingi, kama mwandishi wa vitabu na mwelimishaji katika chuo kikuu na jamii. Kila mara nimepata fursa ya kuongea na wasomaji wa maandishi yangu na watu ambao sijawahi kuwafahamu kabla. Wanakuja na maoni, taarifa, na uzoefu mbali mbali. Tunabadilishana mawazo. Inakuwa ni kama shule muhimu sana. Tamasha linapoisha, jioni, najiona nimeelimika sana. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika vitabu na maandishi mengine. Namshukuru k