Simlaumu JK kwa kuzunguka duniani
(Makala hii imechapishwa katika KWANZA JAMII, Agosti 18-24, 2009) Profesa Joseph L. Mbele Katika makala zangu za hivi karibuni, nimegusia suala la kuiga mambo, kama vile mashindano ya urembo na suala la vyama vya siasa. Inaonekana suala hili litahitaji kushughulikiwa tena na tena. Katika makala yangu moja, niliongelea safari za JK nchi za nje, na baadhi ya watu walilalamika kuwa JK anasafiri mno. Walikumbushia kuwa viongozi wa nchi zingine za jirani, kama vile Kenya, hawasafiri hivyo, lakini nchi zao zinapiga hatua kutuzidi. Hitimisho likawa kwamba JK awaige viongozi hao; atumie muda mwingi nchini badala ya nje. Wazo kuwa JK afanye kama wanavyofanya viongozi wa nchi zingine linahitaji tafakari. Napenda kuliongelea wazo hilo, kwa kutumia mfano huo wa Kenya na Tanzania. Je, kiongozi wa Tanzania anaweza kuiendeleza Tanzania kwa kuiga anayofanya kiongozi wa Kenya? Tanzania inaweza kuendelea kwa kuiiga Kenya? Tanzania ni nchi yenye upekee. Kenya nayo ina upekee wake. Hizi nchi mbili zin