Posts

Showing posts from March, 2019

Kitabu Kinatumika Chuo Kikuu China

Image
Tarehe 7 Februari, wakati namalizia maandalizi ya warsha kuhusu Culture and Globalization, niliyofanya Dar es Salaam, nilipata taarifa ya kufurahisha kutoka kwa kijana mTanzania asomaye China. Kijana huyu, Seleman Pharles Mabala, aliniambia kuwa siku moja profesa wao mChina aliwaambia wasome kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences ,  katika kozi ya "Cultural Differences and Cross-cultural Communication." Chuo hicho kiitwacho University of Electronic Science and Technology , kiko katika mji wa Chengdu, katika jimbo la Sichuan.  Aliniambia kuwa alifurahi sana kumsikia profesa akisema kuwa kitabu kimeandikwa na mTanzania. Alipiga picha kama kumbukumbu akawapelekea marafiki nyumbani. Kijana aliendelea kuniambia: "Nakupa hongera sana na mimi hii kwa njia moja ama nyingine imenitia nguvu ya kuendelea kusoma kwa bidii nifikie angalau nusu yako!" Ninafurahi kuwa nimeweza kumtia kijana huyu hamasa ya kusoma kwa bidii. Kwangu kama mwalimu,