Makanisa mengi ya ki-Luteri Marekani, ELCA , yana ushirikiano na makanisa ya ki-Luteri ya Tanzania na nchi zingine. Kanisa la Shepherd of the Valley , ambalo liko hapa Minnesota, lina uhusiano na kanisa la Tungamalenga, mkoani Iringa. Kwa taarifa zaidi, soma hapa. Nimewahi kutembelea Shepherd of the Valley kuongea na wanafunzi wa Chuo cha Gustavus Adolphus ambao walikuwa hapo kufanya maandalizi ya safari ya Tanzania, kama nilivyoelezea hapa . Kwa miaka mingi kiasi nilifahamu kuhusu uhusiano baina ya Shepherd of the Valley na Tungamalenga. Kila ninapoliwazia kanisa la Shepherd of the Valley , au ninapoliona, naiwazia Tungamalenga, ingawa mimi si m-Luteri. Kwa vile liko pembeni mwa barabara, ninaliona kanisa hilo kila ninapoenda kutoa mihadhara katika Chuo cha Mazingira . Sikuwahi kufika Tungamalenga, hadi mwaka jana, niliposafiri na wanafunzi wa ki-Marekani kutoka Iringa kwenda hifadhi ya Ruaha. Ghafla tulipita sehemu iitwayo Tungamalenga. Nilishtuka, kwa sababu sikuwa hata naj