Posts

Showing posts from February, 2009

Nchi Zinazoendelea: Ni Zipi Hizo?

Dhana ya "nchi zinazoendelea" imejengeka vichwani mwa watu, tangu zamani. Pamoja na dhana hiyo, kuna pia dhana ya "nchi zilizoendelea." Je, dhana hizo zina mantiki yoyote? Binafsi, ingawa zamani nilikuwa na mawazo kama wengine, kwamba kuna nchi zilizoendelea na zile zisizoendelea au zinazoendelea, miaka hii nimegundua kuwa dhana hizi hazina mantiki, na ni ushahidi wa kasumba vichwani mwa watu, au elimu duni. Kwa mujibu wa dhana hizo, nchi kama Marekani, Uingereza, Sweden, Ujerumani, na Japani zinahesabiwa kuwa zimeendelea. Lakini nchi kama Tanzania, Kenya, na Uganda zinahesabiwa kuwa nchi zinazoendelea. Kwa nini nasema dhana hizi ni duni? Kwanza, hakuna nchi duniani ambayo imesimama tu. Kila nchi iko katika mchakato na mabadiliko katika uchumi, siasa, utamaduni, na kadhalika. Marekani ya mwaka juzi ni tofauti na Marekani ya leo, na Marekani ya miaka mitano ijayo itakuwa tofauti na hii ya leo. Na ndivyo ilivyo kwa nchi zote. Kama ni tekinolojia, kwa mfano, tekinol

Kuwasomea Watoto Vitabu

Enzi za mababu na mabibi zetu, ilikuwa ni kawaida kwa wazee kukaa na watoto jioni na kuwasimulia hadithi. Utamaduni huu ulikuwa sehemu ya maisha. Ilikuwa ni sehemu ya elimu waliyopewa hao watoto. Hapakuwa na shule tulizo nazo leo, wala vitabu, lakini wazee walikuwa walimu bora, waliotumia mbinu mbali mbali, kama hizi hadithi, katika kuwaelimisha watoto. Siku hizi, kutokana na kuwepo kwa vitabu, tunayo fursa ya kutumia vitabu kuendeleza elimu ya watoto. Kama hatuna uwezo wa kuwasimulia hadithi kwa mtindo wa mababu na mabibi zetu, tunayo fursa ya kuwasomea vitabu. Wenzetu katika nchi kama Marekani wanaendeleza utamaduni huu kwa kuwasomea watoto hadithi za vitabuni. Watoto wa kiMarekani wanategemea mzazi awasomee vitabu. Ni kawaida kwa mzazi kumsomea mtoto kitabu kabla hajalala. Mashuleni na kwenye maktaba za Marekani, kuna utaratibu wa kuwa na vipindi vya kuwasomea watoto vitabu. Watu wanajitolea kwenda maktabani au mashuleni kufanya kazi hiyo, wawe ni wafanyakazi maofisini, madaktari,