Posts

Showing posts from 2012

Milima Haikutani

Image
Wa-Swahili husema, milima haikutani bali binadamu hukutana. Hayo yalinipata mjini Karatu mwaka 2008 nilipokutana na mzee ambaye anaonekana nami pichani. Siku hiyo ilikuwa siku ya mnada mjini Karatu, siku ambayo hutokea mara moja kwa mwezi. Katika umati mkubwa wa watu, yeye na mimi tulijikuta uso kwa uso. Yeye alinitambua mara moja, akauliza: "Profesa Mbele?" Nilimwambia ndio mimi. Tulifurahi sana, tukaanza michapo. Mzee huyu nilimfahamu mwaka 1996 wakati nafanya utafiti wa masimulizi ya jadi kuhusu shujaa wa wa-Iraqw aitwaye Saygilo Magena. Utafiti huu ulinipeleka kwenye miji na vijijini kama vile Mbulu, Mamaisara, na Karatu. Kati ya watu walionisaidia sana ni huyu mzee ambaye jina lake ni John Qamlali. Baada ya kufahamiana kule Mbulu, tulikutana tena mjini Arusha, tukaongea sana. Anajua sana habari za wa-Iraqw na ameshawasaidia watafiti wengine wa mataifa mbali mbali. Ninazo kanda za maongezi yetu. Kukutana tena mwaka 2008, miaka zaidi ya kumi tangu tulipokutana ma

Maaskofu Watoa Tamko Juu Ya Masuala Mbali Mbali

TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKUTANO MKUU WA NNE WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TCF ) TAMKO RASMI “ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA” Utangulizi Katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, Tanzania Christian Forum – TCF, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Desemba, 2012; Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na kutathmini juu ya wajibu wa Kanisa na Utume wake wa Kinabii kwa taifa letu. Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha taasisi kuu za Umoja wa Makanisa nchini kama ifuatavyo;- Jumuiya ya Kikristo Tanzania - CCT Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania - PCT Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (observers) Tafakari Tafakari yetu ilianza kwa kujiuliza yafuatayo: 1. Ni mwenend

Shaaban Robert na Nyerere: Waandishi Muhimu kwa Kila m-Tanzania

Image
Kwa miaka michache iliyopita, wakati nimejitosa katika kusoma maandishi ya Shaaban Robert, nimejiwa na mawazo mbali mbali ambayo naona ni muhimu. Kwa bahati nzuri, nimechapisha makala mbili juu ya Shaaban Robert, moja katika Encyclopedia of African Literature , na nyingine katika CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Napenda kunukuu machache niliyoandika katika Encyclopedia of African Literature : Shaaban Robert displayed profound awareness of the human condition; he opposed injustice, championed freedom, and extolled the dignity of labour. He was sensitive to the condition of women. He wrote poems celebrating women, and a biography of Siti Binti Saad, the famous female taarab singer, recounting the meteoric rise to fame of this woman from a humble rural background in a male-dominated world which put incredible obstacles in her path. He was proud of his Swahili language and culture, which he understood very well, appropriated, and celebrated in and through his writings. However, he deeply resp

Habari Njema: Kitabu cha "Hemingway and Africa" Kimefika

Image
Leo nina furaha sana. Kisa? Kitabu nilichoagiza, Hemingway and Africa , kimefika leo. Kila ninapojipatia kitabu kipya ninafurahi. Ukizingatia kuwa hadi sasa nina vitabu zaidi ya elfu tatu, utaona kuwa nimekuwa mwenye furaha, tena na tena. Huenda nitaishi miaka kadhaa ya ziada kutokana na hiyo furaha. Pamoja na hayo yote, hiki kitabu cha Hemingway and Africa ni cha pekee. Mwanzo kukiona ni pale nilipokiazima kutoka maktaba ya Chuo Kikuu cha Minnesota, nikakisoma. Kilinigusa kwa namna ya pekee, kwa jinsi kilivyosheheni taarifa na uchambuzi mpya, nikaamua lazima niwe na nakala. Kama unavyoniona pichani, nimekishika kitabu hiki nikiwa nimefurahi sawa na mtu aliyejishindia kreti ya bia. Ninataja bia kwa makusudi. Kitabu hiki, chenye kurasa 398, bei yake ni dola 80 ambayo kwa madafu ni zaidi ya 120,000. Ukienda baa na hela hizo, unapata kreti mbili za bia, kuku mzima, na nauli ya teksi ya kukurudisha kwenu Mbagala. Kama wewe si mtu wa baa, hizo hela ni mchango tosha wa sherehe kama vi

Hongera JWTZ Kwa Kufungua Maktaba

Image
Nimevutiwa sana na taarifa juzi kuwa Rais Kikwete, Amiri Jeshi wa Tanzania, amefungua maktaba ya kisasa kwenye chuo cha mafunzo cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Monduli. Ni habari njema kabisa. Mimi ni mdau mkubwa wa maktaba na katika blogu hii ninaziongelea mara kwa mara. Mifano ni maktaba za  Tanga ,  Dar es Salaam ,  Songea ,  Lushoto ,  Moshi ,  Iringa , na  Southdale . Kwa miaka mingi sijawahi kusikia rais au kiongozi mwingine wa kitaifa Tanzania akifungua maktaba, ukiachilia mbali tarehe 9 Desemba, 1967, ambapo Mwalimu Nyerere alifungua Maktaba Kuu ya Taifa, Dar es Salaam. Pita katika maktaba yoyote Tanzania, utaona kuwa maktaba ni kitu ambacho wa-Tanzania hawakithamini sana, isipokuwa labda wanafunzi. Na hao wanafunzi wanaonekana maktabani endapo wamebanwa sana na mwalimu au wanakabiliwa na mitihani. Wakaazi wa Tanga, kwa mfano, wamekuwa na bahati ya kuwa na maktaba tangu mwaka 1958, kabla ya Uhuru. Ingebidi wawe juu kabisa kitaifa kwenye suala la elimu. Lakini wapi

Serikali Yapongeza Kuanzishwa Kitivo cha Udaktari Songea

Image
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akisalimia wananchi baada ya kuwasili Peramiho. Kushoto kwake ni ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega akifuatiwa na Mratibu wa Kitivo cha Udaktari Peramiho Chuo cha Mt Augustino Tawi la Songea Padre Dunstan M. Mbano Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akikagua maeneo ya kitivo cha udaktari Peramiho. Kushoto kwake ni Joseph Joseph Mkirikiti na kulia kwake ni ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega akifuatiwa na Mrati bu wa K itivo cha Udaktari Peramiho Padre Dunstan Mbano Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akielekezwa jambo na ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega . Jengo la utawala ambalo bado halijaanza kutumika Jengo la hosteli ya wanafunzi ambalo bado halijaanza kutumika Jengo la Maa b ara K itivo cha U da ktari Peramiho baada ya ukarabati ambalo bado halijaanza kufanya kazi ku t okana na ukosefu wa vifaa vya kufundishia

Mungu ni Mmoja: Anaitwa Allah, Brahman, Chiuta, Ruwa na Kadhalika

Uzuri wa kuwa na blogu yako ni kuwa hutawaliwi na mtu katika kuamua nini cha kuandika. Uamuzi wote ni wako. Nimesema kabla kuwa katika blogu yangu hii, masuala ambayo yanasemwa kuwa ni nyeti, kama dini, ni ruksa kujadiliwa. Tena sio tu ruksa, bali muhimu kujadiliwa . Leo napenda kutoa hoja kuwa Mungu ni mmoja: anaitwa Allah, Brahman, Chiuta, Ruwa, na kadhalika, kutokana na kuwepo kwa lugha nyingi hapa duniani. Huyu ndiye aliye juu ya yote, mwenye uwezo wote, kama inavyosemwa katika ki-Arabu, "Allahu akbar." Ni dhana ya msingi katika dini zetu. Kama wewe ni mu-Islam, halafu unasema kuwa Allah ni tofauti na Mungu wanayemwabudu wa-Kristu, au Mungu wanayemwabudu wa-Hindu, jichunguze upya, kwani utakuwa unasema kuna miungu zaidi ya mmoja. Utakuwa unaongelea kuwepo kwa mungu mwingine zaidi ya Allah. U-Islam hautambui kuwepo kwa Mungu mwingine zaidi ya Allah. Kama wewe ni m-Kristu, halafu unasema kuwa Mungu unayemwabudu ni tofauti na Allah, basi inabidi ujichunguze, kwa misin

Baridi Kali Minnesota

Image
Jimbo la Minnesota ni moja ya sehemu zinazopata baridi kali kuliko zote Marekani, wakati wa miezi ya baridi. Jana imeanguka theluji nyingi, kama inavyoonekana pichani, katika eneo la Chuo cha St. Olaf . Wakati kama huo ni hatari kuendesha magari, na ajali huwa nyingi, yaani magari kugongana barabarani, au kuteleza na kutumbukia mitaroni. Baridi hii haizoeleki hata kama mtu umepambana nayo miaka na miaka. Inapokuja, ni bora kubaki nyumbani, kama huna sababu ya lazima ya kwenda nje, na kama unakwenda nje, ni lazima kujizatiti kwa mavazi yatakiwayo. Vinginevyo, baridi hii itakuletea madhara. Kuna watu wanaokufa kutokana na kuwa nje kwenye baridi hii. Katikati ya picha hapa kushoto linaonekana gari maalum ambalo kazi yake ni kusafisha njia na barabara kutokana na kufunikwa na theluji.

Simba wa Tsavo

Image
Leo napenda kuongelea habari ya simba wa Tsavo. Ni habari iliyokuwa inatusisimua sana tulipokuwa shuleni, baina ya darasa la tano na la nane. Kulikuwa na kitabu, Simba wa Tsavo , ambacho kilichapishwa mwaka 1966. Ni tafsiri ya kitabu cha J.H. Patterson kilichoitwa The Man Eaters of Tsavo . Kitabu hiki kilielezea matukio ya kutisha wakati ujenzi wa daraja la reli kwenye mto Tsavo, nchini Kenya, miaka mia na kitu iliyopita. Kilielezea namna simba walivyokuwa wakiwavizia, kuwadaka na kuwaua wafanya kazi kwenye eneo la hili daraja wakawaua watu zaidi ya mia, hadi, hatimaye, Patterson alipofanikiwa kuwaua, mwezi Desemba 1898. Hiyo ndio habari tuliyosoma tukiwa shuleni, miaka hiyo ya sitini na kitu. Lakini, kwa miaka hii ya karibuni, yapata miaka kumi, nimekutana na taarifa nyingine nyingi kuhusu simba wa Tsavo. Je, unajua wale simba waliishia wapi? Katika kusoma habari za mwandishi Ernest Hemingway, ambaye alizaliwa mwaka 1899 eneo la jirani na Chicago, nimegundua kuwa alipokuwa mto

Barua za Ernest Hemingway, 1907-1922

Image
Leo nimekipata kitabu cha barua za Hemingway ambacho nilikitaja katika blogu hii siku chache zilizopita. Kama nilivyoandika, nilikiona kwa mara ya kwanza katika duka la vitabu hapa Chuoni St. Olaf. Lakini nakala ile ilinunuliwa hima, ikabidi niagize. Hemingway alikuwa mwandishi makini wa barua. Hata mwanae, Mzee Patrick Hemingway, amethibitisha hivyo. Kwa ujumla, Hemingway hakutaka wala kutarajia kuwa barua zake zichapishwe. Alikuwa na mazoea ya kuandika barua zake kwa uwazi na hata kutumia lugha ambayo inaonekana kali au yenye kukiuka maadili. Baada ya Hemingway kufariki, mwaka 1961, suala la kuchapisha au kutochapisha maandishi ya Hemingway ambayo alikuwa hajayachapisha lilijitokeza na kuwa kubwa. Maandishi yake mengine alikuwa hajamaliza kuyarekebisha. Barua zake alikuwa hajaazimia zichapishwe. Suala likawa nini kifanyike. Wasomaji wa maandishi ya Hemingway walisukumwa na kiu ya kutaka kusoma maandishi yake yote. Wahariri na watafiti walitaka hivyo pia. Familia yake ilikuwa

Wa-Kristu Wasilimu; Wa-Islam Waingia u-Kristu

Image
Dini ni moja ya mada ambazo nazizungumzia sana katika blogu yangu. Leo napenda kugusia tena mada ya mtu kubadili dini. Niliwahi kuandika kuhusu mada hiyo, nikatamka kuwa kubadili dini ni haki ya mtu, kwa mujibu wa dhamiri yake. Soma hapa .  Dini ni safari ambayo binadamu anasafiri. Kwa wengine ni safari ngumu yenye vikwazo vingi. Kwa wengine ni safari nyepesi, kwa maana kwamba wametulia kabisa katika imani yao. Namshukuru Muumba kwamba mimi ni mmoja wa hao waliotulia, ingawa nilipokuwa kijana nilihangaika na kutetereka kiasi fulani. Ukiangalia mtandaoni, kama vile YouTube, utaona taarifa nyingi za watu wanaobadili dini, kutoka u-Islam kuingia u-Kristu, kutoka u-Kristu kuingia u-Islam, na kadhalika. Maelfu ya watu wanafanya hivyo muda wote. Katika YouTube utawaona wengi wakitoa ushuhuda kuhusu walivyohamia dini nyingine na nini kiliwafanya wahame.  Kwa mtazamo wangu, hayo ni mambo yao binafsi, baina yao na Muumba. Hayaongezi wala kuteteresha imani yangu. Hapa chini ni taarifa ya w

Nimekutana na Kobina Aidoo

Image
Siku chache zilizopita, Kobina Aidoo kutoka Ghana alitembelea hapa Chuoni St Olaf kutoa mhadhara kama sehemu ya maazimisho ya Africa Weeks. Maazimisho hayo huandaliwa kila mwaka na jumuia ya wanafunzi iitwayo Karibu. Sikuwa nimesikia jina la Kobina Aidoo, ila nilihudhuria mhadhara wake. Ni kijana mwenye kipaji anayeinukia katika nyanja za filamu na uanaharakati katika kuelimisha jamii. Aliongelea suala la nani ni mw-Amerika Mweusi, akaleta changamoto nyingi zinazowakabili watu weusi wanaoishi hapa Marekani katika kujitambua na kujitambulisha. Baada ya kusema machache, alituonyesha DVD yake ambayo imajaa kauli na mitazamo ya watu weusi wanaoishi Marekani, wakiwa wametokea nchi mbali mbali za Afrika na bara la Marekani. Ni mitazamo inayofikirisha na kuchangamsha akili. Inatupanua mawazo kuhusu utata wa suala hilo la nani ni m-Marekani Mweusi, na kwa ambaye hakufahamu, inashtua kuona migogoro baina ya waMarekani weusi wa asili na watu weusi ambao ni wahamiaji wa miaka ya karibu

Naiwazia Songea

Image
Nyumbani ni nyumbani. Leo nimeikumbuka Songea, nikaamua kuleta picha mbili tatu nilizopiga mwaka huu. Hapa kushoto ni barabara itokayo stendi kuu kuelekea bomani, hatua chache tu kutoka duka la vitabu la Kanisa Katoliki. Nyuma ya haya majengo ndipo kilipo Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki . Hapa ni taswira ya uwanja wa Maji Maji, kutoka juu. Nilipiga picha hii kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli niliyofikia, ng'ambo ya barabara kutoka kituo kikuu cha polisi. Kule ng'ambo ni kitongoji cha Lizaboni, njiani kuelekea Peramiho , Mbinga , na Mbamba Bay . Hapa kushoto ni stendi kuu nikiwa na dada yangu na mdogo wangu.

Mwandishi Hemingway: Vitabu Vipya

Image
Ernest Hemingway ni kati ya waandishi maarufu kabisa duniani. Alizaliwa mwaka 1899 karibu na mji wa Chicago, akafa kwa kujipiga risasi nyumbani kwake kwenye jimbo la Idaho mwaka 1961. Katika maisha yake, aliandika sana, akianzia kama ripota wa gazeti la Kansas City Star. Maandishi yake ni pamoja na riwaya, hadithi fupi, insha, masimulizi ya safari zake, barua magazetini, mashairi, na maelfu ya barua. Tangu wakati wa uhai wake hadi leo, watu wengi sana wamechambua maandishi yake na kuelezea maisha yake. Vitabu kumhusu Hemingway vinaendelea kuchapishwa. Miezi ya karibuni, vimechapishwa vitabu kama Hemingway and Africa , Hemingway's Boat , na The Letters of Ernest Hemingway: Volume 1,1907-1922 . Kitabu cha The Letters of Ernest Hemingway: Volume 1, 1907-1922 nilikiona kwa mara ya kwanza miezi michache iliyopita katika duka la vitabu la Chuo cha St. Olaf. Ni kitabu muhimu sana kwa jinsi kinavyojumlisha kila barua ya Hemingway inayojulikana kwa kipindi cha miaka iliyotajwa. Nin

Tanzania: Nchi ya Mavuvuzela

Image
Kama ilivyo kawaida yake, Kipanya hakosi neno. Kwenye katuni hapa kushoto katoboa ukweli: Tanzania ni nchi ya mavuvuzela. Tukubaliane kwa hilo.

Wanafunzi Wangu wa ki-Ingereza Muhula Huu

Image
Leo nimepiga picha na baadhi ya wanafunzi wangu ambao nimekuwa nikiwafundisha muhula huu somo la uandishi wa lugha ya ki-Ingereza. Wanafunzi wote wanaosoma hapa chuoni St. Olaf wanatakiwa kusoma somo hilo kama msingi wa masomo ya chuo. Kwa vile wanafunzi ni wengi, tunawagawa katika madarasa madogo, yasiyozidi wanafunzi 18 kila darasa. Uchache huu unamwezesha mwalimu kumsaidia kila mwanafunzi ipasavyo, kwa kuhakiki uandishi wake na kumpa mawaidha. Ninapenda kufundisha masomo yote ninayofundisha. Ninawapenda wanafunzi. Lakini kwa vile mimi ni mwandishi, ninapenda kwa namna ya pekee kufundisha uandishi wa lugha ya ki-Ingereza . Kutumia ki-Ingereza vizuri kabisa ni mtihani mkubwa, kama mwandishi maarufu Ernest Hemingway alivyokiri na kutukumbusha . Hata huku ughaibuni kwa wenye lugha hii, wengi hujiandikia tu na kuamini kuwa wameandika ki-Ingereza vizuri. Kukaa nao na kuwaonyesha njia nzuri ni bahati na baraka ambayo ninaifurahia.

Rais Obama Anunua Vitabu

Image
Jana Rais Obama aliripotiwa akinunua vitabu kwenye duka dogo, kwa lengo la kuchangia mapato ya wafanya biashara wadogo. Alitanguzana na binti zake, akanunua vitabu 15 vya watoto, kwa ajili ya kuwagawia ndugu. Picha ionekanayo hapa ni ya J. Scott Applewhite, Associated Press. Niliposoma taarifa hii, nilijiuliza je, ni lini tumewahi kuwaona vigogo wa Bongo wakinunua vitabu? Ni lini umewahi kumwona kigogo wa Bongo akiwa na wanawe katika duka la vitabu? Pia nilikumbuka kuwa niliwahi kuuliza katika blogu hii kama unaweza kumpa m-Tanzania kitabu kama zawadi ya Krismasi au Idd el Fitri. Soma hapa .  Kama vigogo wa Bongo wangekuwa na utamaduni wa kuvithamini vitabu, wangeweza kuleta mabadiliko makubwa nchini. Wangeweza kuanzisha maktaba vijijini. Wangeweza kuanzisha klabu za usomaji wa vitabu. Vigogo hao husafiri sana nje ya nchi. Kwenye viwanja vya ndege, iwe ni O'Hare, Schippol, Heathrow, Johannesburg, au Istanbul, kuna maduka ya vitabu. Vigogo hao wangeweza kununua vitabu kila w

Kanisa Katoliki Mjini New Prague, Minnesota

Image
Jana nilifika mjini New Prague hapa Minnesota, kwa shughuli binafsi. Nilishawahi kupita kwenye mji huu mara kadhaa, na kitu kimoja kilichonivutia tangu mwanzo ni kanisa Katoliki ambalo liko katikati ya mji, pembeni mwa barabara. Watu waliniambia tangu zamani kuwa kanisa hili lilijengwa na wahamiaji kutoka Czechoslovakia, na kwamba madirisha yake ya vioo (stained glass) yanavutia sana. Nilikuwa na hamu ya siku moja kwenda kusali hapo na pia kuangalia hayo madirisha. Mimi hupenda nyumba za ibada za dini mbali mbali kama nilivyoeleza hapa na hapa . Jana, kwa vile nilikuwa mjini hapo, nilihakikisha nimepiga picha ya kanisa hilo, ingawaje ni kwa nje tu. Nilipata fursa ya kuona kuwa pembeni mwa kanisa kuna shule. Huu ni utamaduni wa kanisa Katoliki, kwamba panapojengwa kanisa, na huduma zingine ziwepo, hasa shule na hospitali. Nilivyoliangalia hilo kanisa na hiyo shule, nilikumbuka kijijini kwangu, kwani kule nako hali ni hiyo hiyo.

Kwa wa-Luteri wa Tungamalenga, Iringa

Image
Makanisa mengi ya ki-Luteri Marekani, ELCA , yana ushirikiano na makanisa ya ki-Luteri ya Tanzania na nchi zingine. Kanisa la Shepherd of the Valley , ambalo liko hapa Minnesota, lina uhusiano na kanisa la Tungamalenga, mkoani Iringa. Kwa taarifa zaidi, soma hapa. Nimewahi kutembelea Shepherd of the Valley kuongea na wanafunzi wa Chuo cha Gustavus Adolphus ambao walikuwa hapo kufanya maandalizi ya safari ya Tanzania, kama nilivyoelezea hapa . Kwa miaka mingi kiasi nilifahamu kuhusu uhusiano baina ya Shepherd of the Valley na Tungamalenga.  Kila ninapoliwazia kanisa la Shepherd of the Valley , au ninapoliona, naiwazia Tungamalenga, ingawa mimi si m-Luteri. Kwa vile liko pembeni mwa barabara, ninaliona kanisa hilo kila ninapoenda kutoa mihadhara katika Chuo cha Mazingira . Sikuwahi kufika Tungamalenga, hadi mwaka jana, niliposafiri na wanafunzi wa ki-Marekani kutoka Iringa kwenda hifadhi ya Ruaha. Ghafla tulipita sehemu iitwayo Tungamalenga. Nilishtuka, kwa sababu sikuwa hata naj

Mdau Wangu Mpya, Mhadhiri wa Mankato

Image
Nimempata mdau mpya, mhadhiri katika chuo cha North Central, mjini Mankato, Minnesota. Natumia neno mdau au wadau kwa maana ya wasomaji wa vitabu vyangu ambao wanajitokeza na kujitambulisha kwangu. Nina kawaida ya kuwataja wadau hao katika hii blogu yangu, kama unavyoweza kusoma hapa na hapa . Leo napenda nimwongelee huyu mdau mpya, Mhadhiri Davis. Wiki kadhaa zilizopita, nilipigiwa simu na Profesa Scott Fee wa Chuo Kikuu cha Minnesota, Mankato, akisema kuwa wakati anapiga simu, yuko katika mazungumzo na Mhadhiri Becky Davis, wakiongelea kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Alinipa fursa nikasalimiana na Mhadhiri Davis, ambaye anaonekana pichani hapa kushoto. Waalimu hao walikuwa katika maandalizi ya kupeleka wanafunzi Afrika Kusini. Pamoja na kuongelea upatikanaji rahisi wa nakala za kitabu hiki, walikuwa wananialika Mankato kuongea na wanafunzi. Bila kusita, niliupokea mwaliko wao. Falsafa yangu ni kuwa Mungu kanipa fursa ya kuelimika sio i

Kitabu cha Mazungumzo ya Nelson Mandela

Image
Leo nimenunua kitabu cha Nelson Mandela, Conversations with Myself . Ingawa sijui nitakisoma lini, kutokana na utitiri wa vitabu vyangu, nimekinunua kutokana na umaarufu wa Mandela na kutokana na ukweli kwamba kumbukumbu zake na mawaidha yake ni hazina kubwa. Idadi ya vitabu vinavyosimulia na kuchambua mchango wa Mandela vinaendelea kuchapishwa. Yeye mwenyewe pia amejitahidi kuandika. Kwa mfano, tulipokuwa vijana, tulikifahamu kitabu chake kiitwacho   Long Walk to Freedom . Haikuwa rahisi mtu usikijue kitabu hiki, kwani kilichapishwa katika mfululizo maarufu wa vitabu vya shirika la Heinemann, ambalo tulilifahamu sana kutokana na vitabu vyake ambavyo tulikuwa tunavisoma. Miaka ya karibuni, Mandela amejikakamua akaandaa kitabu cha hadithi, Nelson Mandela's Favorite African Folktales . Ni mkusanyiko wa hadithi za asili za ki-Afrika. Kwa kuangalia juu juu, nimeona kuwa hiki kitabu cha Conversations with Myself ni mkusanyiko wa barua mbali mbali za Mandela na maandishi mengin

Nimeenda Tena Chuo Cha Mazingira, Minnesota

Image
Leo nilitembelea tena Chuo cha Mazingira , mjini Apple Valley. Kama alivyofanya mwaka hadi mwaka, Mwalimu Todd Carlson alinialika kwenda kuongea na wanafunzi wake kuhusu uwiano baina ya masimulizi ya jadi na mazingira. Mwalimu Todd Carlson, anaonekana pichani kushoto kabisa Mwalimu Carlson huwaeleza wanafunzi kuhusu masimulizi ya jamii mbali mbali za asili, kama vile wa-Marekani Wekundu, wenyeji wa asili wa Australia, na pia wa-Khoisan wa pande za kusini mwa Afrika. Anatumia pia kitabu changu cha Matengo Folktales . Kila ninapoenda kuongea na wanafunzi hao, nawakuta wamesoma angalau sehemu fulani muhimu za kitabu hicho.   Kutokana na maandalizi hayo anayofanya Mwalimu Carlson, mazungumzo yangu na wanafunzi pamoja na masuali yao huwa ya kiwango cha juu. Kama ilivyokuwa safari zilizopita, sote tumefurahia ziara yangu ya leo.

U-Islam Watekwa Nyara

Image
Leo nimejipatia kitabu kiitwacho The Great Theft: Wrestling Islam From the Extremists . Mwandishi ni Khaled Abou El Fadl, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, ambaye kwenye jalada nyuma ya kitabu, ametajwa kuwa "one of the world's preeminent Islamic scholars and an accomplished Islamic jurist." Nikitafsiri kwa ki-Swahili, ni kwamba mwandishi huyu ni mmoja wa wataalam wa u-Islam ambao wanaongoza hapa duniani na pia ni mwanasheria mahiri wa sheria za ki-Islam. Nimeanza kukisoma kitabu hiki leo hii. Tayari ninaona kuwa hiki kitabu ni moto wa kuotea mbali, kwa jinsi kinavyouelezea na kuutafsiri u-Islam kwa mujibu wa misahafu yake, na kwa jinsi kinavyowabomoa hao wanaoitwa wa-Islam wenye siasa kali. Mwandishi anawabainisha kuwa ni wapotoshaji, kwenye masuala kama nafasi ya wanawake katika u-Islam, jihad, haki za binadamu, ugaidi, na vita. Kitabu hiki kinanikumbusha kitabu changu kingine, kiitwacho Muhammad: A Biography of the Prophet , ambacho

Lord of the Flies: Riwaya ya William Golding

Image
Kila siku naviangalia vitabu vyangu nilivyo navyo hapa ughaibuni. Ni vingi sana. Jana nilikichomoa kitabu kimojawapo, Lord of the Flies , kilichotungwa na William Golding, ili nikiongelee hapa katika blogu yangu. Lord of the Flies ni moja ya vitabu vilivyonigusa sana nilipokisoma nikiwa sekondari. Kilikuwa ni kitabu kimojawapo cha lazima katika somo la "Literature." Kilituvutia sana vijana wa wakati ule. Ni kitabu cha hadithi ya kubuniwa, yenye ujumbe mzito kuhusu tabia ya binadamu. Tunawaona vijana wadogo kutoka U-Ingereza wakiwa wamepata ajali ya meli na kuachwa katika kisiwa peke yao. Hakuna mtu mzima. Wanawajibika kujipanga ili waweze kuendelea kuishi, kwa kutegemea uwindaji humo kisiwani, na wanawajibika kujitungia utaratibu wa kuendesha jamii yao. Hao ni watoto waliolelewa katika maadili mazuri huko kwao u-Ingereza, lakini katika mazingira ya kupotelea humo kisiwani, tunawaona wakididimia kimaadili, na hatimaye tunashuhudia wanavyoanza kuwa wabaya kabisa, na hii

Taarifa kwa Umma Kuhusu Hatma ya MwanaHalisi

Image
Leo 28 Oktoba 2012 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bidamu (THRD-Coalition), wadau wanaounda mtandao huu na mwanachama mwanzilishi wa Mtandao likiwa ni shirika lenye majukumu ya ya kutetea uhuru wa habari kusini mwa Afrika (MISA-Tan) tunaendelea kwa pamoja kuonyesha kusikitishwa kwetu kwa kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi. Kwa mara kadhaa sasa tunawakutanisha tena lengo likiwa ni kuendelea kuishawishi serikali ilifungulie gazeti la Mwanahalisi. Kwa vile hoja yetu ya kutaka kuliona gazeti la Mwanahalisi likiwa mitaani haijatimia basi na sisi kwa upande wetu kazi yetu bado haijatimia. Tunatambua umuhimu wa kuheshimu sheria za nchi, lakini kwa upande mwingine tunaona kwamba ipo haja ya sisi watetezi wa haki za binadamu kupitia kwenye vyombo vya habari na pia kwenye mashirika mengine yanayounda mtandao huu kuishawishi serikali kuachana na sheria gandamizi ambazo ni za kidikteta kama sheria hii ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo hukiuka misingi ya haki za binadamu na uta

Mdau Profesa Aliyenihamasisha Kuandika Kitabu

Image
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, Profesa John Greenler wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison . Alikuja hapa Chuoni St. Olaf na binti yake. Kama umesoma kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , utaona nimemtaja Profesa Greenler kwenye ukurasa wa "Acknowledgements." Profesa huyu tulifahamiana miaka yapata kumi iliyopita kwenye mikutano ya washauri wa programu ya Associated Colleges of the Midwest (ACM) ambayo hupeleka wanafunzi Tanzania. Miaka ile yeye alikuwa anafundisha Chuo cha Beloit . Wakati wa kupanga na kutathmini hali ya program kila mwaka, nachangia kwa namna ya pekee masuala yanayohusu tofauti za tamaduni, ambayo ni changamoto kwa wa-Marekani na wa-Tanzania. Kwenye mikutano yetu hiyo, nilikuwa, na bado niko, mstari wa mbele kufafanua matukio mbali mbali na mambo mengine wanayokumbana nayo wanafunzi katika kuishi na wa-Tanzania. Profesa Greenler alipochukua fursa ya kupeleka wanafunzi Tanzania, aliniomba niandik

Ngoma Nzito Marekani: Tanzania Je?

Image
Pamoja na mapungufu yake yote, siasa Marekani ina mambo kadhaa ya kupigiwa mfano. Kinachonivutia zaidi ni mijadala inyofanyika baina ya wagombea kabla ya uchaguzi. Leo, kwa mfano, tumeshuhudia pambano la tatu baina ya Obama na Romney Mijadala ya namna hii inawapa wapiga kura fursa ya kuwasikiliza wagombea. Vile vile naiona kama namna ya kuwaheshimu wapiga kura. Mfumo wa Marekani unatambua kuwa wapiga kura wana haki ya kuwasikia wagombea wakiongelea masuala kadha wa kadha katika kupambanishwa na wapinzani wao. Ninakerwa ninapokumbuka mambo yalivyo kwetu Tanzania. Ninakerwa nikikumbuka jinsi CCM ilivyotoroka midahalo mwaka 2010. Ni dharau kwa wapiga kura. Tatizo ni jinsi wapiga kura wengi walivyo mbumbumbu, wasitambue kuwa hili lilikuwa dharau. Walipiga kura kama vile hawajadharauliwa. Hebu fikiria mambo yangekuwaje ule mwaka 2010 iwapo Kikwete angepambana na Slaa katika midahalo mitatu hivi, ambayo ingeonekana katika televisheni na kusikika redioni. Lakini tulinyimwa fursa hii,

Mtume Hatetewi kwa Dhulma na Ujinga

Mtume Hatetewi Kwa Dhulma Na Ujinga Uislamu Na Shari'ah Zake Imekusanywa Na: ‘Uthmaan Beecher Imefasiriwa Na: Abu Suhayl Shukrani njema zinamstahili Allaah, rahmah na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad, na aali zake na maswahaba zake na Waislamu wote. Ama baada ya hayo Hakuna Muislamu ambaye anaweza kukubaliana na kutukanwa, kudhalilishwa, kudhauruliwa na kusingiziwa mambo mabaya Mtume wetu mpendwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ma-Imaam wa Ahlus-Sunnah kama Imam Maalik, al-Layth, Ahmad, na Ash-Shaafi’iy, wamekubaliana kwa pamoja kwamba yeyote atakayemvunjia heshima, kumtukana au kumdhalilisha au kumtia ila Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa amekufuru, na adhabu inayomstahili kwa yule anayeishi katika dola ya Kiislamu na akafanya hivyo ni kifo, adhabu ambayo itakuwa katika mikono ya mtawala wa Kiislamu. Hapana shaka kwamba mashambulizi ya aina hii kwa Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yatasababisha hasir