Posts

Showing posts from 2013

Nimepata Zawadi Murua ya Krismasi Leo

Image
Wafuatiliaji wa fasihi ya ki-Ingereza wanafahamu kuwa juzuu la pili la barua za Hemingway, limechapishwa mwaka huu. Sawa na juzuu la kwanza, hili ni buku kubwa, kurasa 519. Leo nimepokea kifurushi kutoka Amazon.com. Binti yangu Zawadi aliponiletea nilishangaa, maana sijaagiza kitabu kutoka Amazon kwa miezi kadhaa. Nilipofungua kifurushi sikuamini macho yangu. Ni juzuu hilo nililolitaja. Nimefurahi sana. Nilikuwa natamani kufanya mkakati wa kununua. Lakini Mungu mkubwa, kamwongoza huyu bwana aninunulie hiki hiki ambacho roho yangu ilikuwa inatamani. Bwana aliyeniletea ni David Cooper, mzazi wa mwanafunzi mmojawapo wa wale waliokuja Tanzania mwezi Januari mwaka huu kwenye kozi ya Hemingway. Baba huyu ni msomaji makini wa Hemingway na waandishi wengine. Ni huyu bwana, anayeishi Ohio, alipoambiwa na kijana wake kwamba natamani siku moja kwenda Montana kuongea na Mzee Patrick Hemingway, mtoto pekee wa Ernest Hemingway aliebaki, alisema atatusafirisha kwa ndege yake. Siku ilipofika

Mama Kutoka Togo Kawahi Kununua Zawadi za Krismasi

Image
Mama mmoja kutoka Togo ambaye ni rafiki ya familia yangu, alitutembelea wiki kama tatu zilizopita. Kati ya mambo mengine, alsema anataka kununua nakala mbili za kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Alisema ni zawadi ya Krismasi kwa marafiki zake waliopo hapa hapa Marekani. Huyu mama ni kati ya wasomaji wa mwanzo kabisa wa kitabu hiki mara kilipochapishwa, mwanzoni mwa mwaka 2005. Alikipenda sana na kuanzia pale akawa anakipigia debe kwa watu mbali mbali. Hata kuna wakati ndugu yake alikuja kutoka Togo, akamtafutia nakala, ambayo alienda nayo Togo. Namshukuru mama huyu. Nanatafakari suala hilo. Kuna vitabu vingi sana hapa Marekani ambavyo vinafaa kama zawadi kwa ndugu na marafiki. Lakini mama huyu kachagua kitabu changu. Halafu huyu mama hana kibarua au kipato cha ajabu: anafanya kazi ya kutunza wazee hospitalini. Lakini, mama huyu, pamoja na ugumu wa kupata hela hapa Marekani, pamoja na ugumu wa matumizi kwa ujumla, kabana hela akaamua kunu

Kwa Wapumbavu wa Kigoma Wanaoleta Vurugu Kwenye Mikutano ya Dr. Slaa

Huu ni ujumbe kwenu wapumbavu wa sehemu mbalimbali za Kigoma ambao mmekuwa mkileta vurugu kwenye mikutano ya Dr. Slaa, katibu mkuu wa CHADEMA. Ni moja ya haki za binadamu kutafuta, kupata, au kusambaza taarifa na mitazamo katika masuala mbali mbali yanayoihusu jamii. Someni tangazo la kimataifa la haki za binadamu. Taarifa hizo hupatikana kwa namna mbalimbali, kuanzia vyombo vya habari hadi mikutano. Nimeona picha za makundi ya watu wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Dr. Slaa. Hiyo ni haki yao, mojawapo ya haki za binadamu. Lakini nimeona pia taarifa za wapumbavu wachache, kama vile Kasulu, wakija kuvuruga au kujaribu kuvuruga mikutano hiyo. Hao ni wapumbavu. Kenge wakubwa. CCM, chama ambacho kimeshika hatamu katika nchi hii, chenye wajibu wa kuongoza na kuelimisha jamii, kimekaa kimya. CCM naijumlisha katika kundi hili la wapumbavu. Zito Kabwe, ambaye anatajwa na hao wavurugaji kwamba wanamtambua yeye, naye hajasema kitu. Naye ni mpumbavu. Kuna haki zingine za binadamu zinazohus

Wajinga Hunena, CCM Ilileta Uhuru Tanganyika

Kiwango cha ujinga Tanzania kinatisha. Utawasikia wengi wakisema kuwa CCM ilileta Uhuru Tanganyika mwaka 1961. Wajinga wengine, kuanzia wanasiasa hadi watu wa mitaani, husema kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 52. Utamsikia mwanasiasa anaiponda CCM kwa kuuliza, "Miaka yote 52 ya utawala wa CCM, wananchi mmenufaika vipi?" Na utammsikia kada wa CCM akitamba, "CCM ni chama chenye uzoefu wa miaka 52. Hapakuwa na CCM mwaka 1961. Chama kilicholeta Uhuru Tanganyika ni TANU. Wala CCM haijawa madarakani miaka 52. Kuna mengi katika historia ya Tanganyika na Tanzania ambayo yanasahaulika au kupotoshwa kwa sababu ya uzembe wa wa-Tanzania. Wajinga wengine wanasema kuwa leo tunasherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania au Tanzania Bara. Mwaka 1961 hapakuwa na nchi iliyoitwa Tanzania wala Tanzania Bara. Nchi iliyopata Uhuru mwaka ule ni Tanganyika. Inasikitisha.

Ninayo Pia Blogu ya Ki-Ingereza, Jamani

Wadau wa blogu hii ya hapakwetu, samahani kama sikuweka wazi tangu mwanzo kuwa ninayo pia blogu ya ki-Ingereza. Inaitwa "Mbele" na anwani yake ni hii: http://www.josephmbele.blogspot.com. Niliamua kuanzisha na kuendesha blogu hii ya ki-Kiingereza ili kuchangia elimu hasa katika masuala ya fasihi ya ki-Ingereza. Mimi ni mwalimu wa somo hili mwenye uzoefu tangu miaka ya mwanzoni ya sabini na kitu. Nilifundisha katika idara ya Literature, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1976, nikasomea shahada ya udaktari Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani, 1980-86, na kuanzia mwaka 1991 nimekuwa nikifundisha katika idara ya ki-Ingereza ya chuo cha St. Olaf hapa Marekani. Katika blogu hii ya "Mbele" mara kwa mara ninaongelea vitabu, hasa vitabu vya fasihi. Uchambuzi wangu vitabu hivi unasomwa duniani kote. Nimeona kuwa uchambuzi wangu wa riwaya ya The Old Man and the Medal unapitiwa kuliko andiko jingine lolote na watu kutoka duniani kota. Nina uzoefu na ufah

Kitabu Kinapendwa

Image
Tangu nichapishe vitabu vyangu mtandaoni, ninaweza kufuatilia mauzo kila siku. Nimefungua duka mtandaoni , na nimetoa ushauri kwa waandishi wengine, hasa wa-Tanzania, kuhusu uzuri na ubora wa tekinolojia hii. Ushauri wangu nimeutoa katika kitabu kiitwacho CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Lakini inaeleweka kuwa ukiwa na wazo ukaliweka kitabuni, usitegemee kama wa-Tanzania wataliona. Huu ni ukweli ambao umesemwa tena na tena. Nami sidhani kama nina la kuongeza. Papo hapo, falsafa yangu ni kuwa ukiwa na jambo la manufaa, waeleze wengine. Kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences ndicho chenye mauzo kuliko vingine vyote. Kila ninapoona kimenunuliwa, najiuliza ni nani huyu aliyenunua. Pengine inakuwa ni nakala moja, lakini pengine ni nakala za kutosheleza darasa. Nami sijui ni nani kaagiza. Hiki kitendawili kinanifanya niwe na dukuduku, na nafahamu kuwa sitapata jawabu. Kuna wakati zinapita siku nyingi kidogo bila mtu kukinunua, lakini wakati mwingine hali

Nimenunua "Nomad," Kitabu cha Ayaan Hirsi Ali

Image
Miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia jina la Ayaan Hirsi Ali, mwandishi kutoka Somalia, ambaye alikuwa ameikimbia nchi yake na alikuwa anaishi Uholandi, ambako alifanikiwa hata kuwa mbunge. Ilionekana ni mwandishi mkorofi, kwa maana ya kwamba wengi walikerwa na kukasirishwa alivyokuwa anahoji utamaduni wa wa-Somali na u-Islam, hasa kuhusu masuala ya haki za wanawake. Nilisoma kuhusu kitabu chake Infidel , ambacho kilisemekana kiliwakasirisha wa-Islam wengi. Nilikuwa na dukuduku ya kusoma maandishi yake, lakini, kutokana na majukumu mengi, sikufuatilia. Hata hivi, nimezingatia ukweli kuwa, kuliko kutegemea ya kuambiwa, muhimu mtu kujisomea mwenyewe. Leo nimenunua kitabu cha Ayaan Hirsi Ali kiitwacho Nomad . Ingawa ninasoma vitu vingi kila siku, nitakipa kitabu hiki kipaumbele. Wakati huo huo, nitanunua vitabu vyake vingine. Insh'Allah, nitapata wasaa wa kuelezea nawazo yake.

Nimepata Wageni Leo

Image
Leo nimepata bahati ya kutembelewa na wageni wawili. Mmoja ni Mchungaji John Mhekwa kutoka Tungamalenga, Iringa. Mwingine ni Profesa Paula Swiggum wa chuo cha Gustavus Adolphus , St. Peter, Minnesota. Mchungaji Mhekwa hatukuwa tunafahamiana, lakini Profesa Swiggum tumefahamiana kwa miaka kadhaa, kwani katika programu yake ya kupeleka wanafunzi Tanzania, alinialika kuongea nao kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni, kama maandalizi ya safari. Wanafunzi walikuwa wanasoma kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Huo ulikuwa ni uamuzi wake. Mazungumzo yangu na hao wanafunzi yalihusu mambo niliyoandika katika kitabu hiki. Baada ya Profesa Swiggum kustaafu, profesa aliyemrithi, katika kuendesha programu hiyo, Barbara Zust, aliendelea na utaratibu huo . Kifupi ni kwamba Profesa Swiggum tumeanza zamani kiasi kushirikiana katika nyanja hizo. Leo ilikuwa fursa ya pekee ya kufahamiana na huyu mgeni mwingine, Mchungaji Mhekwa. Nimemwambia kuwa Tungamalenga

Tamasha la Vitabu Twin Cities, Oktoba 12, Lilifana

Image
Tamasha la vitabu, Twin Cities Book Festival , lililofanyika mjini St. Paul, Minnesota, jana, tarehe 12, lilienda vizuri. Niliondoka mapema asubuhi, yapata saa mbili, nikafika kwenye maaonesho saa tatu. Sikuwa nimechelewa, kwani wakati naandaa vitabu vyangu kwenye meza yangu, wengine nao walikuwa wakiandaaa, ingawa wengi walishapanga vitabu vyangu siku iliyotangulia Meza niliyopata, baada ya kulipia dola 80, ilikuwa namba 12. Nilikuwa nimejisajili kwa jina la Africonexion , ambayo kampuni yangu ndogo inayohusika na uchapishaji na uuzaji wa vitabu vyangu, na pia kuratibu mihadhara yangu ya kuchangia maelewano baina ya watu wa tamaduni mbali mbali. Tangu nilipoisajili kampuni hii, shughuli zake zimekuwa zikifanyika zaidi hapa Marekani, lakini hatimaye, hasa nitakaporejea Tanzania baada ya kustaafu hapa Marekani, nataka kuijenga kampuni hii Tanzania, Africa Mashariki, na sehemu zingine.   Kama kawaida, watu walianza kuingia ukumbini tangu milango ilipofunguliwa. Ukiwaanga

Vijana Washikwa Mtwara Wakiwa Katika Mafunzo ya Al Shabaab na Al Qaida

Image
  Stori ambayo ilishika namba 1 kwenye habari 10 za AMPLIFAYA ya Clouds FM October 7 2013 ni hii ya Polisi Mtwara kukamata vijana 11 ambao walikua wakifanya mazoezi ya kijeshi waliyokua wakijifunza kutoka kwenye cd za magaidi zilizokua na mafunzo kutoka kwa makundi ya Al Shabaab na Al Qaeda. Taarifa zaidi unaweza kuzisoma hapo chini kwenye hiyo taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi. CHANZO: dj sek 0 comments: Post a Comment

Tamasha Kubwa la Vitabu, Twin Cities, Oktoba 12

Lile tamasha maarufu kabisa la vitabu ambalo limefanyika mjini Minneapolis kwa miaka mingi, mara moja kwa mwaka, limekaribia kabisa. Kuanzia mwaka jana, tamasha limehamia mjii St. Paul, kwenye viwanja vya State Fairgrounds. Hakuna tamasha kubwa zaidi ya hili katika eneo hili la Minnesota na majimbo ya jirani. Wanahudhuria watu yapata 7,000, wapenzi wa vitabu. Wanakuwepo waandishi, wachapishaji, wahariri, wachora picha za vitabuni, wahakiki, wauzaji wa vitabu na majarida. Wanahudhuria wazee, watu wazima, vijana, na watoto. Nimeshiriki tamasha hili kwa miaka mingi, kama mwandishi wa vitabu na mwelimishaji katika chuo kikuu na jamii. Kila mara nimepata fursa ya kuongea na wasomaji wa maandishi yangu na watu ambao sijawahi kuwafahamu kabla. Wanakuja na maoni, taarifa, na uzoefu mbali mbali. Tunabadilishana mawazo. Inakuwa ni kama shule muhimu sana. Tamasha linapoisha, jioni, najiona nimeelimika sana. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika vitabu na maandishi mengine. Namshukuru k

Wa-Tanzania Tusiwachokoze Wanya-Rwanda

WaTanzania tunapaswa kuwa waangalifu sana tunapoongea na Wanya-Rwanda au tunapowaongelea. Hao ni watu ambao wamepitia majanga ambayo waTanzania hatuwezi hata kufikiria. Wengi wao wameshuhudia ndugu, jamaa, marafiki wakiuawa kikatili. Wengi wameshuhudia familia yao yote ikichinjwa kwa mapanga. Wengi waliachwa wakiwa wakiwa tangu utotoni. Majanga yaliyowapata, sisi waTanzania hatujawahi kushuhudia katika maisha yetu, na hata tukijaribu kufikiria, tutakuwa tunaelea hewani tu. Undani wake na ukweli wake hatutaweza kuuelewa. Wa-Tanzania tunashangaa kwa nini wanya-Rwanda wamepandisha jazba sana kutokana na ushauri wa Rais Kikwete kwamba wafanye mazungumzo na wapinzani wao walioko Kongo. Hatuelewi kwa nini ushauri uliotolewa kwa nia njema, kwa vigezo vyetu, umewatibua kiasi hicho. Wa-Tanzania wengi wameamua wanya-Rwanda wamevuka mpaka katika msimamo wao. Ninaamini wa-Tanzania tunakosea katika kudhani hivyo. Angalia Israel. Mauaji ya kimbari yaliyowapata wa-Yahudi miaka ya elfu moja mia

Zawadi Baada ya Mhadhara Finland

Image
Bado nina mengi ya kusema kuhusu safari  yangu ya wiki iliyopita nchini Finland, kwenye mkutano. Nina kumbukumbu nyingi, na kama nilivyowahi kusema zamani, blogu yangu ni mahali ninapojiwekea mambo yangu binafsi. Kama nilivyotamka , nilialikwa kutoa mhadhara maalum, ambao hapa Marekani huitwa "keynote address." Mada yangu ilikuwa "The Epic as a Discourse on National Identity." Baada ya kutoa mhadhara, mtoa mhadhara alikuwa anakabidhiwa ua. Ua hilo ni shukrani ya waandaaji wa mkutano. Hapa kushoto anaonekana Profesa Pekka Hakamies, mwenyekiti wa kamati ya maandilizi, ambaye aliniletea mwaliko. Tulioalikwa kutoa hiyo mihadhara maalum tulikuwa watano, kila mtu akatoa mhadhara wake kwa wakati tofauti. Mhadhara wa aina hiyo hutolewa mbele ya washiriki wote wa mkutano, na unategemewa kuweka msingi au changamoto za kujadiliwa na washiriki katika vikao mbali mbali ambamo mada mbali mbali hutolewa. Katika kuhudhuria hivyo vikao vya baadaye, nilifurahi kuw

Ziara Yangu Finland Imefanikiwa Sana

Image
Tarehe 19 hadi 24 nilikuwa kwenye Chuo Kikuu cha Turku, Finland, kwenye mkutano wa kitaaluma. Nilialikwa nikatoe mmoja ya mihadhara maalum, "keynote address." Mhadhara wangu ulikuwa "The Epic as a Discourse on National Identity." Utafiti, ufundishaji na uandishi wangu kuanzia kwenye mwaka 1977 umekuwa zaidi kuhusu masimulizi kama yale ya Iliad, Odyssey, Dede Korkut, Sundiata, Liongo Fumo, Kilenzi, Beowulf, Gassire, Ibonia, na Kalevala. Anayeonekana pichani kulia, ni Profesa Pekka Hakamies, mwenyekiti wa jopo la maandalizi, aliyenialika. Washiriki walikuja kutoka pande mbali mbali za dunia. Hapa kushoto niko mbele ya kanisa moja, mjini Turku. Sikupata muda wa kuingia ndani, bali nilikuwa napita hapo nje kila nikiwa njiani baina ya hoteli nilyofikia na sehemu ya mkutano, mwendo wa dakika kama 15 kwa mguu. Jioni ya tarehe 23 nilialikwa Helsinki, kwa chakula cha jioni. Hapo nilikutana na wa-Tanzania kadhaa waliokuja kujumuika nami. Ukarimu wao

Nangojea Kukaguliwa "Eapoti"

Image
Wadau, wiki ijayo ninasafiri kwenda Finland, kwenye mkutano, nikitokea uwanja wa ndege wa Minneapolis. Sasa kuna haka kasuala ka waBongo kukaguliwa sana kwenye hivyo viwanja vya ndege. Nasubiri zamu yangu. Hii mijitu iliyotufikisha hapa imetuhujumu sana waBongo. Nasikia mingine ni mijitu mikubwa serikalini, na mingine eti ni mifanyabiashara. Biashara gani hii kama si uroho wa fisi, ujambazi, na uuaji? Hii mijitu imechangia kuathirika kwa afya na maisha ya wengi nchini, na kinachoudhi ni kuwa inaachwa iendelee kutanua na kufanya hujuma hizo. Haya ni baadhi ya matunda ya kuwa na CCM madarakani. Nchi hii iko mikononi mwa CCM. Nawapongeza wana-CCM na vikofia vyao, na magwanda yao ya kijani, kwa kutufikisha hapa tulipo. Miaka yote iliyopita, nilikuwa najivunia kuwa m-Tanzania, kutokana na kazi kubwa aliyofanya Mwalimu Nyerere. Ilikuwa ni heshima kuwaambia watu popote duniani kuwa mimi ni m-Tanzania. Miaka hii ya leo najisikia aibu kuwa m-Tanzania.

Afrifest 2013 Ilifana Minnesota

Image
Jana, mjini Brooklyn Park hapa Minnesota, yalifanyika maonesho ya Afrifest. Afrifest ni tamasha linalofanyika mara moja kwa mwaka, likiwajumuisha watu wenye Asili ya Afrika na wengine wowote wale, kwa lengo la kufahamiana, kujielimisha, na kujipatia burdani mbali mbali. Watu wa kila aina walishiriki, wazee, vijana, na watoto. Hapa kushoto tunawaona watoto wakiwa na mpiga ngoma maarufu hapa Minnesota. Aliwaonyesha namna ya kupiga ngoma, na pia aliwaelezea maana na matumizi ya ngoma katika tamaduni za Afrika. Watu walikuwa wameambiwa kuwa tamasha lilipangiwa kuanza saa sita mchana. Kuanzia hapo watu walikuwa wanafika, kwa wakati wao. Vijana kutoka benki ya Wells Fargo walifanya kazi nzuri ya kujitolea, kuwahudumia waliohudhuria. Walikuwa wamevalia tisheti nyekundu. Hapa ni banda ambapo watu walikuwa wanajipatia chakule. Wahusika wanajua sana kuandaa vyakula, kama vile wali na kuku. Siku nzima, kulikuwa na muziki kuto

Afrifest 2013, Minnesota

Image
Kesho, Agosti 10, ndio ile siku ya tamasha la Afrifest hapa Minnesota. Ni tamasha linalofanyika mara moja kwa mwaka, kwa lengo la kuwakutanisha watu wenye asili ya Afrika na wengine pia. Afrifest ni fursa ya kufahamiana, kuelimishana, na kuburudika na maonesho mbali mbali ya michezo na tamaduni. Kwa taarifa zaidi kuhusu tamasha la kesho, angalia tangazo nililobandika hapa. Pia soma nilivyoandika katika blogu yangu ya ki-Ingereza . Kama una watoto, na unakaa maeneo haya ya Twin Cities, jiulize watoto hao wana fursa zipi za kupanua mawazo ili wawe raia wa dunia ya utandawazi wa leo. Unawaandaa vipi waweza kuwa na uzoefu wa kufanya kazi na kushirikiana na watu wa mataifa na tamaduni mbali mbali. Ni wazi kuna vitu vikubwa ambavyo mzazi unaweza kufanya kwa lengo hilo. Lakini vile vile, kuna vitu kama haya matamasha ambayo yanachangia. Mimi kama mtafiti, mwalimu na mwandishi nahudhuria Afrifest kila mwaka. Napata fursa ya kufahamiana na watu, kukutana na wale ambao tunafahamiana, kuo

Mapendekezo ya Mwigulu Nchemba Kuhusu Ajira kwa Vijana

Image
Jana, kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mwigulu Nchemba ametoa mapendekezo kuhusu ajira, ambayo anasema atayawasilisha Bungeni kama hoja binafsi : Habari vijana wenzangu, Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA. HINTS, 1) Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi. Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI; (A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI (B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja (C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA H

Tundu Lissu: Pigeni Kelele Kuokoa Watanzania

Image
Lissu: Pigeni kelele kuokoa Watanzania Penulis : mtandao-net on Saturday, August 3, 2013 | 10:09 PM CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeutaka umoja wa vijana wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IYDU) kupiga kelele kote duniani ili kuwanusuru Watanzania wanaouawa hovyo kwa sababu za tofauti za siasa hapa nchini. Akizungumza na uongozi wa umoja huo (IYDU) jijini Dar es Salaam wiki hii, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu alisema ni wakati wa vijana kuwaokoa wenzao wa Tanzania ambao kujiunga kwao na siasa kumesababisha wachukiwe na watawala. “Watu wanauawa hadharani na hakuna hatua zinazochukuliwa…nendeni katika nchi zenu katika mabunge yenu mkapige kelele katika haya yanayotokea Tanzania; inaweza kusaidia na mkawa mmewasaidia Watanzania,” alisema Lissu. Tundu Lissu alisema viongozi wengi wamekamatwa na kufunguliwa kesi nyingi mahakamani, na hivyo kuifanya CHADEMA kuwa katika wakati mgumu kuliko mwingine wowote katika uendeshaji wa siasa za vyama vingi

Mbongo Akikaguliwa "Eapoti" Ughaibuni

Image

Wageni Kutoka Tanzania

Image
Wiki hii nimekuwa na bahati hapa Minnesota ya kukutana na wageni wawili kutoka Tanzania. Mgeni wa kwanza, Ndugu Charles Mpanda kutoka Arusha, tulionana tarehe 25 mjini Rochester, tukapiga picha inayoonekana hapa kushoto. Habari ya tukio hili niliandika hapa . Nitaandika zaidi katika blogu hii ya "hapakwetu." Leo nimeenda mjini New Prague, kuonana na mgeni mwingine, Fr. Setonga, ambaye naonekana naye katika hiyo picha ya chini. Fr. Setonga tumewasiliana kwa miaka mingi kidogo, kwa simu na barua pepe, ila hatukuwahi kuonana. Leo imekuwa bahati ya kuonana. Tumeongelea masuala mbali mbali, kuhusu dini yetu, kuhusu juhudi na mafanikio ya Kanisa Katoliki katika sekta ya elimu, sehemu mbali mbali duniani, kwa karne hadi karne, kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu. Hii inatokana na msimamo wa Kanisa Katoliki wa kuthamini sana elimu. Kwangu mimi niliyesomeshwa katika shule za Kanisa Katoliki, ni jambo la kujivunia na kushukuru kwamba walinifundisha maa

Mwaliko Mkutanoni Finland

Nimepata mwaliko kwenda kushiriki mkutano wa wanataaluma Finland, katika chuo kikuu cha Turku. Mkutano ufanyika kuanzia tarehe 19 hadi 24 Agosti na mada yake itakuwa The Role of Theory in Folkloristics and Comparative Religion." Nitakuwa mmoja wa watoa mada wateule, na mhadhara wangu utahusu "The Epic as Discourse on National Identity," kama ilivyotajwa katika programu hii hapa . Mkutano huu wa wanataaluma umeandaliwa kwa kumbukumbu ya marehemu Profesa Lauri Honko, mmoja wa wataalam wakubwa kabisa duniani katika. Wa-Tanzania labda watafurahi kusikia kuwa Profesa Honko alifanya utafiti sehemu mbali mbali za dunia, ikiwemo Tanzania. Niliwahi kumwona,  na kuwa naye kwa wiki kama mbili hivi, wakati nilipohudhuria warsha ya watafiti ambayo aliiendesha Turku mwaka 1991. Alikuwa ni mtaalam sana, aliyekuwa anaongea kwa kujiamini kabisa, lakini mtu mtaratibu na mpole. Ukisoma vitabu vyake na makala zake, unaona wazi kabisa kuwa alikuwa mwenye mawazo mazito yenye kutoa mchango m

Kiu ya Kusoma Vitabu

Daima nina kiu ya kusoma vitabu.  Sio rahisi unikute sina kitabu. Hii sio tu kwa vile mimi ni mwalimu. Ni tabia ambayo nilijengeka nayo tangu nikiwa kijana mdogo. Kuwa mwalimu kumenipa motisha zaidi ya kusoma sana vitabu. Wakati huu ninapoandika, wanafunzi wangu na mimi tumemaliza kusoma Half of a Yellow Sun kilichoandikwa na Chimamanda Ngozi Adichie. Sote tumekifurahia sana. Lakini, mwandishi huyu amechapisha hivi karibuni na kitabu kingine kiitwacho Americanah , ambacho tayari kinazungumziwa sana miongoni mwa wapenda vitabu. Kwa hivi, nami najipanga kujipatia kitabu hiki, nikisome. Kitabu kingine ambacho tumekimaliza katika darasa tofauti siku chache zilizopita ni Midnight's Children cha Salman Rushdie.  Kitabu hiki ni kama chemsha bongo, kwa jinsi kilivyotumia mbinu mbali mbali za kuelezea maisha ya mhusika mkuu Saleem Sinai. Maisha hayo yamefungamana na historia ya India, tangu dakika ile India ilipopata uhuru, usiku wa manane, mwaka 1947. Rushdie amechanganya matukio ya

Chezea Arusha Weye

Image
Katuni hii imenipendeza. Sina zaidi, bali niseme tu haka kajibwa kanatisha. Tena usiombee kukutana nako. Ingawa mchoraji hajataja mambo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika siku chache zilizopita, katuni inayapeleka mawazo yetu kwenye uchaguzi huo, ambao matokeo yake yamekuwa CHADEMA kushinda kata zote nne zilizokuwa zinashindaniwa. Matokeo hayo hayakunishangaza. Kwa miaka kadhaa, katika pitapita zangu Arusha, nikiongea na madereva wa teksi, mafundi viatu, na wauza mitumba, nimejionea nguvu za CHADEMA katika mji ule. Nilithubutu hata kuandika makala kuhusu nguvu ya CHADEMA mjini Arusha. Makala hiyo ni hii hapa . Niliandika hayo, na leo ninaandika tena, ingawa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Tumeanza Kusoma "Abyssinian Chronicles"

Image
Baada ya kumaliza kitabu cha Half of a Yellow Sun, darasa langu la fasihi ya Afrika tumekuwa tukisoma Abyssinian Chronicles , riwaya ya Moses Isegawa. Moses Isegawa ni kijana aliyezaliwa na kukulia Uganda. Lakini mwaka 1990 aliondoka Uganda akaenda kuishi Netherlands, akiwa amechukua uraia wa nchi ile. Nilikuwa nimesikia habari za kitabu chake hiki kwa miaka kadhaa. Nilinunua nakala, ila sikupata fursa ya kukisoma, ingawa nilikipitia juu juu. Hata hivyo katika kukipitia hivyo, niliona wazi kabisa kuwa ni kitabu murua, kilichoelezea kwa ufasaha na mvuto mkubwa maisha ya leo ya watu wa Uganda, kuanzia kijijini hadi mjini. Nilipokuwa naandaa kozi yangu hii, miezi michache iliyopita, niliamua kitabu hiki kiwemo katika orodha yangu. Tumesoma karibu kurasa 100 tu,  wakati kitabu kina kurasa 480. Kiasi tulichosoma kimetupa fursa ya kuongelea dhamira mbali mbali zinazojitokeza, kama vile mila na desturi za arusi, masuala ya wahusika, na sanaa. Kwa upande wangu, nimekuwa nikiwaambia w

Taasisi ya Sir Emeka Offor Yachangia Vitabu

Image
Sir Emeka Offor Foundation of Nigeria donates $600,000 to St. Paul-based Books for Africa; Largest donation ever Thursday, 27 June 2013 17:35 Books for Africa photo The Nigeria-based Sir Emeka Offor Foundation has donated $600,000 to Books For Africa (BFA), which will support the shipment of more than a million books to the children of Nigeria and across Africa. "This donation represents the largest single donation we have ever received at Books For Africa, so naturally we are quite excited," said Patrick Plonski, executive director of BFA. "The generosity of Sir Emeka Offor in advancing education across the African continent is an outstanding example for others to follow." Tom Warth, who founded BFA in 1988, said that the "benefits that will accrue to the young people of Africa through this generous donation are immeasurable. We at Books For Africa stru

Tumemaliza Kusoma "Half of a Yellow Sun"

Image
Kwa wiki hizi sita, katika kipindi hiki cha "summer," nimekuwa nikifundisha kozi juu ya fasihi ya Afrika. Jana tumemaliza kusoma Half of a Yellow Sun , riwaya ya Chimamanda Ngozi Adichie wa Nigeria.  Huyu ni mwandishi chipukizi, lakini tayari ameshajipatia umaarufu sana na nyota yake inazidi kung'ara. Amechapisha vitabu kadhaa akianzia na Purple Hibiscus na The Thing Around Your Neck . Ninavyo vitabu hivyo, na nimeshawahi kufundisha Purple Hibiscus .  Hivi karibuni, amechapisha Americanah , kitabu ambacho kinaongelewa sana miongoni mwa wasomaji, walimu, na wahakiki. Kilipochapishwa kitabu cha Half of a Yellow Sun , nilisoma taarifa zake. Taarifa hizi zilielezea kuwa kitabu hiki kinahusu vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Nigeria, ambapo sehemu ya kusini mashariki ilijitenga na kutangaza kuwa imekuwa taifa huru la Biafra. Mwaka 2008 Chimamanda Ngozi Adichie alikuwa mmoja wa waandishi walioalikwa kuhudhuria tamasha la vitabu Minneapolis. Alikuja kuzindua kitabu cha

Makala ya "New York Times" Yaongelea Udhalimu Tanzania

Nicholas Kulish wa gazeti la New York Times amechapisha makala kuhusu vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikifanyika Tanzania, vitendo ambavyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Isome makala hiyo hapa

Mganga wa Kienyeji Akamatwa Akijaribu Kuloga Ndani ya Mahakama Kisutu

Image
MGANGA WA KIENYEJI AKAMWATA AKIJARIBU KULOGA NDANI YA MAHAMAKA YA HAKIMU MKAZI KISUTU LEO MGANGA WA KIENYEJI HUYU HAPA PICHANI, RAJABU ZUBERI(30),MKAZI WA Kerege,Muheza Tanga, akiwa chini ya ulinzi wa wanausalama leo saa mbili asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, baada kifaa maalum cha upekezi kumnasa mganga huyo akiwa na vifaa hivyo vya uganga ambavyo alikuwa amekuja navyo mahakamani hapo kwaajili ya kufanyia mambo ya kishirikina katika kesi moja inayomkabili  mmoja wa washtakiwa mahakamani hapo. Hongereni sana wanausalama kwa kazi nzuri ya kumnasa mtu huyo kwani mmesaidia kuvuruga azma yake.Picha kwa hisani ya Happy Katabazi CHANZO: Jamii Forums

Waraka kwa Rais Obama Kutoka kwa Kamati ya Ulinzi wa Wanahabari

Image
Powered by Translate The Committee to Protect Journalists writes to President @BarackObama ahead of his meeting with President @jmkikwete Imewekwa 26.6.13 The Committee to Protect Journalists wrote to U.S. President Barack Obama ahead of his meetings with Tanzanian President Jakaya Kikwete next week to ask that he bring up the critical importance of press freedom to economic development and democracy. June 25, 2013 His Excellency Barack Obama President of the United States of America White House Via facsimile: +1 202-456-2461 Dear President Obama: Ahead of your first trip to East Africa, we would like to bring to your attention the deteriorating state of press freedom in Tanzania. In your meetings with Tanzanian President Jakaya Kikwete, we ask that you discuss the critical importance of press freedom to economic development and democracy. In the past year, CPJ has documented a rise in threats and attacks against j