SHAMBULIZI DHIDI YA TUNDU LISU LASIKITISHA WATANZANIA: Maaskofu waonya

MAASKOFU Katoliki Tanzania wamelaani vitendo vya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani vinavyoendelea nchini na kusema kuwa vitendo hivyo vinalifedhehesha Taifa kwa kuwa ni dhambi, uhalifu na siyo utamaduni wa Tanzania. Wamesema hayo katika tamko walilolitoa Septemba 11, 2017 ambapo wametaka vitendo hivyo vikomeshwe mara moja. “Tunatamani kuona wale wote walio nyuma ya matukio haya ya vurugu, mauaji, utekaji na utesaji wanatafutwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” imeeleza sehemu ya tamko hilo. Akiongelea tamko hilo la maaskofu, Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania, Padri Dkt. Charles Kitima amesema kuwa Maaskofu wametoa tamko hilo kwa kuwa ni haki na wajibu wao wa msingi kama taasisi iliyo na wajibu ndani ya jamii ya kulea maadili ya watu na kulinda utu wa kila binadamu. Amesema kuwa Kanisa kama taasisi lina jukumu la kuhakikisha malezi ya uadilifu kwa viongozi na kwa umma yanazingatiwa na yanapewa kipaumbele, na kuongeza kuwa Katiba