Maonesho ya Vitabu Blaine, Minnesota

Aprili 26-28, nilishiriki maonesho ya vitabu yaliyoandaliwa na Bukola Oriola kusherehekea miaka kumi tangu kuchapishwa kwa kitabu chake cha kwanza, Imprisoned: The Travails of a Trafficked Victim . Kwa kuwa nimeshiriki maonesho mengi ya vitabu, naweza kusema kwamba maonesho haya aliyoandaa Bukola yalikuwa ya pekoe. Kwa uzoefu wangu, nimeona maonesho yakidumu siku moja, lakini haya ya Bukola yalidumu situ tutu. Kwa hovyo, yalitoa fursa kwa yeyote kuhudhuria siku mojawapo, ambaye hakuweza kuhudhuria siku nyingine. Ingawa Bukola aliandaa maonesho haya kusherehekea miaka kumiss ya kitabu shake, aliwaalika waandishi wengine kushiriki. Nami niliwasilisha vitabu vyqngu. Hakuhitaji tuwepo muda wote wa maonesho, bali wakati maalum uliopangwa kwa mwandishi moja moja kuonekana jukwaani kwa saa moja. Nilitumia muda mrefu kiasi kwenye maonesho, tarehe 26 na 28. Nilionana na waandishi kadhaa, wakiwemo ninaowafahamu, kama vile Rita Apaloo, mwandishi wa African Women Connect: How I star