Maonesho ya Vitabu Blaine, Minnesota

Aprili 26-28, nilishiriki maonesho ya vitabu yaliyoandaliwa na Bukola Oriola kusherehekea miaka kumi tangu kuchapishwa kwa kitabu chake cha kwanza, Imprisoned: The Travails of a Trafficked Victim. Kwa kuwa nimeshiriki maonesho mengi ya vitabu, naweza kusema kwamba maonesho haya aliyoandaa Bukola yalikuwa ya pekoe.

Kwa uzoefu wangu, nimeona maonesho yakidumu siku moja, lakini haya ya Bukola yalidumu situ tutu. Kwa hovyo, yalitoa fursa kwa yeyote kuhudhuria siku mojawapo, ambaye hakuweza kuhudhuria siku nyingine.

Ingawa Bukola aliandaa maonesho haya kusherehekea miaka kumiss ya kitabu shake, aliwaalika waandishi wengine kushiriki. Nami niliwasilisha  vitabu vyqngu. Hakuhitaji tuwepo muda wote wa maonesho, bali wakati maalum uliopangwa kwa mwandishi moja moja kuonekana jukwaani kwa saa moja.

Nilitumia muda mrefu kiasi kwenye maonesho, tarehe 26 na 28. Nilionana na waandishi kadhaa, wakiwemo ninaowafahamu, kama vile Rita Apaloo, mwandishi wa African Women Connect: How I started and grew a networking group of African immigrant women for friendship, business, and community.

Nilikutana na kuongea na watu wengi, nikaongea nao na kubadilishana mawazo na uzoefu. Kila maonesho ya vitabu ambayo nimehudhuria yamekuwa ya manufaa sana.  Haya maonesho ya Bukola mayo yalikuwa hovyo, na anastahili kushukuriwa kea juhudi zake za kuhamasisha usomaji na kuwawezesha waandishi.Comments

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini