Posts

Showing posts from September, 2013

Wa-Tanzania Tusiwachokoze Wanya-Rwanda

WaTanzania tunapaswa kuwa waangalifu sana tunapoongea na Wanya-Rwanda au tunapowaongelea. Hao ni watu ambao wamepitia majanga ambayo waTanzania hatuwezi hata kufikiria. Wengi wao wameshuhudia ndugu, jamaa, marafiki wakiuawa kikatili. Wengi wameshuhudia familia yao yote ikichinjwa kwa mapanga. Wengi waliachwa wakiwa wakiwa tangu utotoni. Majanga yaliyowapata, sisi waTanzania hatujawahi kushuhudia katika maisha yetu, na hata tukijaribu kufikiria, tutakuwa tunaelea hewani tu. Undani wake na ukweli wake hatutaweza kuuelewa. Wa-Tanzania tunashangaa kwa nini wanya-Rwanda wamepandisha jazba sana kutokana na ushauri wa Rais Kikwete kwamba wafanye mazungumzo na wapinzani wao walioko Kongo. Hatuelewi kwa nini ushauri uliotolewa kwa nia njema, kwa vigezo vyetu, umewatibua kiasi hicho. Wa-Tanzania wengi wameamua wanya-Rwanda wamevuka mpaka katika msimamo wao. Ninaamini wa-Tanzania tunakosea katika kudhani hivyo. Angalia Israel. Mauaji ya kimbari yaliyowapata wa-Yahudi miaka ya elfu moja mia