Posts

Showing posts from 2016

Vitabu Tulivyosoma Mwaka 2016

Zikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya kwisha mwaka 2016, nimeona wa-Tanzania kadhaa wakijitokeza katika mtandao wa Facebook na kutaja vitabu walivyosoma mwaka huu. Jambo hili limenifurahisha, nikizingatia kuwa nimekuwa nikihamasisha usomaji wa vitabu, kwa kutumia blogu yangu hii, blogu za wengine, na pia katika kitabu changu, CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Ninawapongeza watu hao kwa kuonyesha mfano mzuri. Ninawapongeza pia wasomaji waliojitokeza na kuchangia suala hili kwa namna mbali mbali, kama vile kuvijadili vitabu hivyo, kuulizia upatikanaji wake, au kupendekeza vitabu vingine. Kuhusu upatikanaji wa vitabu, watu wamepeana taarifa za maduka ya vitabu, na pia upatikanaji wa vitabu pepe mtandaoni. Ni jambo la kuvutia kwamba kuna wa-Tanzania wanaotambua matumizi ya manufaa ya tekinolojia ya mtandao. Mazungumzo haya yameonyesha mambo kadhaa. Jambo moja ni kuwa wako wa-Tanzania wanaojibidisha kusoma vitabu. Jambo jingine ni kuwa wanasoma vitabu vya aina mbali mbali, kama vile vya si

Nimejutia Kusoma "Hamlet" Wakati wa Sikukuu

Image
Siku kadhaa zilizopita, nilianza kusoma Hamlet ,  tamthilia ya Shakespeare, kama nilivyoandika katika blog ya ki-Ingereza. Tamthilia hii haikuwa ngeni kwangu. Ni moja ya tungo za Shakespeare ambazo nimezifahamu au kuzisoma tangu ujana wangu. Lakini kuna jambo ambalo sikulizingatia nilipoamua kusoma Hamlet wakati huu, ambao ni wa sikukuu ya Krismasi. Ulikuwa si wakati muafaka wa kusoma Hamlet , hadithi yenye matukio ya kusikitisha. Mkondo mkuu wa hadithi hii ni jinsi baba ya Hamlet alivyouawa na ndugu yake, mfalme Claudius, ambaye miezi miwili tu kufuatia msiba huo alimwoa mama yake Hamlet. Mambo haya yanampa Hamlet msongo mkubwa wa mawazo. Mzimu wa marehemu baba yake unamtokea Hamlet na kumweleza ufedhuli uliofanyika na kisha kumwelekeza alipize kisasi. Hamlet anatafakari afanye nini. Hasira na huzuni zake anazieleza kwa hisia na ufasaha tena na tena, kwa mfano katika tamko hili: Ham . O that this too too solid flesh would melt Thaw and resolve itself into dew! Or that the E

Zawadi ya Krismasi

Image
Siku tatu zilizopita, jirani yangu m-Marekani, mama mwenye umri zaidi yangu, aliniomba nimsainie nakala za kitabu cha Africans and Americans Embracing Cultural Differences . Alikuwa amevinunua kwa ajili ya kuwapelekea rafiki zake, wa-Marekani wenzake, kama zawadi ya Krismasi. Jambo hili lilitosha kunifanya niandike ujumbe katika blogu yangu, kwani linadhihirisha jadi ninayoiona hapa Marekani, kama nilivyowahi kudokeza katika blogu hii. Lakini nimehamasika kuandika baada ya kusoma makala ambayo ameichapisha Christian Bwaya katika blogu yake. Ameelezea umuhimu wa zawadi kwa watoto na mambo ya kuzingatia katika kutoa zawadi kwa watoto. Kati ya mifano ya zawadi alizotaja ni vitabu. Ni jambo muhimu, nami kama mwalimu ninaliafiki moja kwa moja. Nimejionea jinsi watoto wanavyopenda vitabu, sio tu hapa Marekani, bali pia Tanzania. Nimeandika mara kwa mara umuhimu wa kuwasomea watoto vitabu na kuwajenga watoto katika utamaduni wa kusoma vitabu. Huwa ninafarijika ninaposoma taarifa z

Dunia Yetu ya Maigizo

Shakespeare alisema, tena na tena, kuwa dunia ni jukwaa la maigizo ambapo kila mtu hujitokeza na kuigiza nafasi yake na kisha hutoweka zake. Maelezo haya naona ni kianzio muafaka cha kutafakari mambo ya dunia yetu. Ili kuchangia tafakari hiyo, nanukuu Hamlet , tamthilia maarufu ya Shakespeare, kutoka onyesho la 2, sehemu ya 2, ambapo tunasikia maongezi baina ya Polonius na Hamlet:     Pol . My lord, I have news to tell you.     Ham . My lord, I have news to tell you: when Roscius was an actor in Rome--     Pol . The actors are come hither, my lord.     Ham . Buzz, buzz!     Pol . Upon my honor--     Ham . Then came each actor on his ass--     Pol . The best actors in the world, either for tragedy, comedy, history, pastoral, pastoral-comical, historical pastoral, tragical-historical, tragical-comical-historical-pastoral; scene individable, or poem unlimited, Seneca cannot be too heavy, nor Plautus too light. For the law of writ and the liberty, these are the only men. Tangu

Wosia wa Rabindranath Tagore Kuhusu Uhuru wa Kutoa Maoni

Image
Rabindranath Tagore ni mmoja wa waandishi maarufu kabisa waliowahi kuishi. Alizaliwa mwaka 1861 Calcutta na kufariki 1941. Aliheshimika duniani kote wakati wa uhai wake na bado anaheshimika. Aliandika mashairi, tamthilia, insha, riwaya, hadithi fupi, na pia maelfu ya barua. Niliwahi kufundisha utungo wake maarufu Gitanjali , hapa chuoni St. Olaf. Tagore alikuwa mwalimu aliyetukuka, kioo cha ubinadamu wa kweli ("humanism"), mwenye fikra pevu na nzito juu ya maisha na maadili. Watu maarufu kama W.B. Yeats, Mahatma Gandhi na Albert Einstein, walimmwenzi sana. Mwaka 1913 alipata tuzo ya Nobel katika fasihi. Nina vitabu vyake vitatu, kimojawapo kikiwa Rabindranath Tagore: An Anthology . Kutoka katika kitabu hiki nimenukuu sehemu ya ujumbe wa tarehe 25 Septemba, 1930, kwa gazeti la Izvestia la Urusi. Ni ujumbe unaopaswa kutafakariwa na kuzingatiwa, tunaposhuhudia ukandamizaji wa uhuru wa watu kujieleza. Ili kuufikisha ujumbe kwa watu wasiojua ki-Ingereza, nimejaribu kuutafsi

Leo Nimemaliza Kufundisha Muhula wa Kwanza

Leo nimemaliza kufundisha muhula wa kwanza. Nilikuwa ninafundisha kozi tatu: "First Year Writing," "African Literature," na "Muslim Women Writers." Nilihitimisha ufundishaji wa "First Year Writin"g wiki iliyopita, ili kuwapa wanafunzi muda wa kuandika insha kuu ya mwisho. Katika kozi hii, ninafundisha uandishi bora wa ki-Ingereza, na uangalifu unaotakiwa katika vipengele vyote , kuanzia neno, hadi sentensi, hadi insha. Katika African Literature tumemalizia muhula tukisoma riwaya ya Mia Couto, The Tuner of Silences . Mia Couto ni mwandishi wa Msumbiji, ambaye ni maarufu sana. Amepata sifa na tuzo kem kem, ikiwemo tuzo ya Neustadt.   The Tuner of Silences ni riwaya inayosisimua akili kwa jinsi ilivyosheheni ubunifu wa kisanaa na kifikra. Kuna mengi ya kutafakari katika riwaya hii, hasa yatokanayo na dini, fasihi linganishi, historia, falsafa kama vile "existentialism," na mikondo ya falsafa ya sanaa kama vile "surrealism."

The Rime of the Ancient Mariner: Samuel Taylor Coleridge

Image
Jana na leo nimesoma The Rime of the Ancient Mariner , utenzi maarufu wa Samuel Taylor Coleridge, ambao ni moja ya tungo za ki-Ingereza nilizokuwa ninazipenda wakati wa ujana wangu, kama nilivyoandika katika blogu hii. Nimefurahi kuusoma tena, baada ya miaka mingi, wakati ambapo akili yangu imepevuka zaidi kutokana na kusoma tungo nyingi za fasihi. Katika kusema hivi, ninakumbuka kauli ya mshairi William Wordsworth, katika shairi lake maarufu, "Lines Written a Few Miles Above Tintern Abbey," anavyoongelea namna alivyotembelea, katika utu uzima wake, eneo ambalo alilizoea alipokuwa kijana. Matokeo ya kufanya hivyo ni kwamba, ingawa hawezi tena kuyaona mazingira yale kwa hisia za ujanani, sasa anayaona kwa kutumia akili ya kiutu uzima. Aina zote mbili za maono anazienzi, ingawa zinatofautiana. Nami ninajisikia hivyo hivyo katika kusoma wakati huu The Rime of the Ancient Mariner . Nimeweza kuuweka utungo huu katika mkabala wa tungo nilizosoma kwa miaka ya baina ya ujana

Tamko la CUF Kuelekea Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika

Image
Kesho, Alhamisi, tarehe 9 Disemba, 2016 ni siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika, Watanzania tunaadhimisha miaka 55 ya kuwa huru baada ya harakati za miaka mingi ya kudai uhuru wa nchi yetu kutoka kwa wakoloni waliotutawala. The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinaungana na wananchi wote katika kuadhimisha siku hii muhimu katika historia ya nchi yetu, na kutoa wito kwao kuendelea kusimamia malengo, dhamira, na nia za viongozi wetu katika kupigania Uhuru kama yalivyowahi kusema na kuainishwa kuwa ni kupambana na maadui wakubwa watatu ambao ni Umasikini, Ujinga, na Maradhi. Sambamba na siku ya uhuru wa Tanganyika, tarehe 9 Disemba, ni siku ya maadhimisho ya kimataifa kuhusiana na waathirika wa mauaji ya halaiki na kuzuia jinai zake, ( International Day of Commemoration and Dignity of the Victims of the Crime of Genocide and of the Prevention of this Crime ) kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa (UN) kwa tamko lake namba (A/RES69/363). Tarehe hi

Msikilize Rais Yahya Jammeh Anavyokubali Ushindi wa Mpinzani

Image
Msikilize Rais Yahya Jammeh wa Gambia anavyokubali matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo mpinzani ameshinda. Rais Jammey, bila kusita, anasema kuwa kwa kura zao, wananchi wa Gambia wamenena, naye anayapokea matokeo. Anampongeza mpinzani kwa ushindi wake, na anaahidi kumpa ushirikiano kuanzia kipindi hiki cha mpito. Anamwombea baraka za Allah katika kuiongoza nchi ya Gambia, na anawashukuru watu wa Gambia.

Ndugu wa Uganda Anataka Kitabu

Image
Kama ilivyo kawaida katika blogu hii, ninapenda kujiwekea kumbukumbu mbali mbali. Jana niliwatembelea akina mama wawili wa-Kenya waishio Brooklyn Park, Minnesota, ambao walitaka tukutane ili niweze kuwapa ushauri kuhusu fursa za kujiendeleza kielimu ya juu na katika ajira. Wakati tulipokuwa katika maongezi, waliwasiliana na bwana mmoja wa kutoka Uganda, wakamwita kuja kuungana nasi. Tulizungumza kuhusu masuala mbali mbali, yakiwemo masuali waliyoniuliza juu ya ufundishaji na uandishi wangu. Mmoja wa hao akina mama nilikuwa nimemwahidi kumpa nakala ya kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Huyu jamaa wa Uganda aliniulizia namna ya kukipata kitabu kile, nikamweleza kuwa anaweza kukipata mtandaoni Amazon.com au lulu.com/spotlight/mbele, au kutoka kwangu. Nikamshauri kwamba kwa upnde wa gharama, ni rahisi zaidi kukinunua Amazon.com. Lakini yeye alisisitiza kuwa nimpelekee, akanipa na anwani yake. , M-Ganda huyu amenikumbusha wa-Ganda wengine nilio

Maandalizi ya Wanachuo wa Gustavus Adolphus Waendao Tanzania

Image
Jana nilipata ujumbe kutoka kwa Profesa Barbara Zust wa Chuo cha Gustavus Adolphus akiulizia iwapo nitaweza kwenda kuongea na wanafunzi wanaojiandaa kwenda naye Tanzania kwa safari ya kimasomo. Ameniambia kuwa watakuwa na kikao cha maandalizi ya safari tarehe 2 na 3 Januari, katika kituo cha mikutano cha Mount Olivet . Nimefanya mazungumzo hayo tena na tena miaka iliyopita. Katika ujumbe wake, Profesa Zust amekumbushia kuwa, kama ilivyo jadi, wanafunzi hao watakuwa wameshasoma kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Pia amekumbushia jinsi wanafunzi wanavyoshukuru na kufurahia kwamba wanapokuwa Tanzania wanakutana na yale ambayo ninakuwa nimewaeleza kitabuni na katika mazungumzo. Taarifa hii ni muhimu kwangu, na ndio maana ninaiweka hapa katika blogu yangu, kama kumbukumbu. Kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, nimeitika mwaliko wa Profesa Zust na kumwambia kuwa nitakwenda kukutana nao tarehe 2 Januari. Kama kawaida, panapo majaliwa, nitaandika taar

Kitabu cha Historia ya Chai

Image
Leo nimenunua kitabu, A Brief History of Tea , cha Roy Moxham, nilichokiona jana katika duka la vitabu la hapa chuoni St. Olaf. Nilivutiwa na taarifa kwenye jalada la nyuma: Behind the wholesale image of the world's most popular drink lies a strangely murky and often violent past. When tea began to be imported into the West from China in the seventeenth century, its high price and heavy taxes made it an immediate target for smuggling and dispute at every level, culminating in international incidents like the notorious Boston Tea Party. In China itself the British financed their tea dealings by the ruthless imposition of the opium trade. Intrepid British tea planters soon began flocking to Africa, India and Ceylon, setting up huge plantations. Workers could be bought and sold like slaves. Maelezo haya yalinisisimua nikaona sherti nikinunue kitabu hiki. Niliona wazi kuwa kitanielimisha kuhusu mengi tusiyoyajua juu ya chai, kinywaji ambacho wengi tunakitumia. Mambo hayo ni pa

"A Far Cry From Africa," Shairi la Derek Walcott

Image
Tangu nilipoanza kufundisha katika chuo cha St. Olaf, mwaka 1991, nimepata fursa ya kusoma na kufundisha fasihi iliyoandikwa kwa ki-Ingereza kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyowezekana nilipokuwa ninafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwandishi mmojawapo ambaye kazi zake nimezishughulikia sana ni Derek Walcott wa St. Lucia, pande za Caribbean, maarufu kwa utunzi wa mashairi na tamthilia, ambaye alipata tuzo ya Nobel mwaka 1992. Nimesoma na kufundisha mashairi yake mengi na tamthilia zake kadhaa. Moja ya mashairi hayo ni "A Far Cry From Africa," ambalo lilichapishwa mwaka 1962. Linaelezea mahuzuniko juu ya vita ya Mau Mau nchini Kenya iliyodumu kuanzia mwaka 1952 hadi 1960. Masetla wazungu walipigana na wa-Afrika waliotaka kuchukua ardhi yao iliyoporwa. Kwa kuwa Derek Walcott ni chotara, damu ya kizungu na ki-Afrika, alihisi vita hiyo ikitokea ndani ya nafsi yake. Uhasama na ukatili wa pande hizo mbili aliuhisi mithili ya su

Ninaendelea Kusoma "Hamlet"

Image
Miaka miwili iliyopita, niliandika katika blogu hii kuwa nina tabia ya kusoma vitabu kiholela. Wakati wowote nina vitabu kadhaa ninavyovisoma, bila mpangilio maalum, na pengine bila nia ya kufikia mwisho wa kitabu chochote. Kusoma kwa namna hii hakuna ubaya wowote, bali kuna manufaa. Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, katika seminari ya Likonde, mwalimu wetu, Padri Lambert OSB alituhimiza tuwe na mazoea ya kusoma sana vitabu, na pia mazoea ya kuvipitia vitabu kijuu juu, ambayo kwa ki-Ingereza huitwa "browsing." Nikiachilia mbali vitabu ninavyofundisha, wakati huu nimezama zaidi katika kusoma Hamlet , kama nilivyoandika katika blogu hii.  Ninasoma Hamlet pole pole, ili kuyanasa vizuri akilini yaliyomo, hasa maudhui kuhusu maisha, maadili, na tabia za binadamu. Kusoma pole pole kunaniwezesha kukifurahia ki-Ingereza cha Shakespeare, ingawa si rahisi kama ki-Ingereza tunachotumia leo. Tofauti kati ya ki-Ingereza cha leo na kile cha Shakespeare ninaifananisha na tofauti

"Ozymandias:" Shairi la Shelley na Tafsiri Yangu

Percy Bysshe Shelley ni mmoja kati ya washairi maarufu kabisa katika ki-Ingereza, ambaye nilimtaja jana katika blogu hii. Alizaliwa mwaka 1792 akafariki mwaka 1822. Ni mmoja wa washairi wanaojumlishwa katika mkondo uitwao "Romanticism," ambamo wanaorodheshwa pia washairi wa ki-Ingereza kama William Blake, William Wordsworth, Samuel Taylor Coleridge, na Lord Byron. "Romanticism" ni mkondo uliojitokeza katika mataifa na lugha zingine pia, kama vile Ujerumani na Ufaransa. Kwa waandishi wa Afrika au wenye asili ya Afrika waliotumia ki-Faransa, "Romanticism" ilijitokeza kama "Negritude," jambo ambalo nimeelezea katika mwongozo wa Song of Lawino . "Ozymandias" ni shairi mojawapo maarufu la Shelley. Ninakumbuka kuwa nililisoma kwa mara ya kwanza nilipokuwa sekondari, miaka ya kuanzia 1967. Kitu kimoja kinacholitambulisha shairi hili kuwa ni la mkondo wa "Romanticism" ni ule mtazamo wake ambao Edward Said aliuita "Orientalism

Mashairi Mazuri ya Ki-Ingereza

Tangu ujana wangu, nimebahatika kusoma na kuyafurahia mashairi mazuri ya ki-Ingereza. Ninakumbuka nilivyoingia kidato cha tano, Mkwawa High School, mwaka 1971, nikakutana na Mugyabuso Mulokozi na Kulikoyela Kahigi ambao nao walikuwa wanafunzi. Walikuwa na kitabu cha mashairi ya ki-Ingereza, tukawa tunayasoma na kuyafurahia. Mifano ni shairi la Thomas Hardy, "An Ancient to Ancients." Mashairi ya Shakespeare yaitwayo "sonnets" yalituvutia. Mfano ni "Sonnet 18" ambayo mstari wake wa kwanza ni "Shall I compare thee to a summer's day?" Shairi la Samuel Taylor Coleridge, "The Rime of the Ancient Mariner," lilikuwa daima mawazoni mwetu. Shairi la W.B. Yeats, "The Second Coming," ni moja ya mashairi yaliyonigusa sana, kama nilivyoandika katika blogu hii. Shairi la Walter de la Mare, "The Listeners," limeng'ang'ania akili mwangu tangu enzi zile. Mashairi mengine tulisoma darasani, kama vile yale ya Percy Bys

Ninajikumbusha "Hamlet"

Image
Wiki hii, pamoja na majukumu ya kawaida ya kufundisha, nimeamua kujikumbusha enzi za ujana wangu kwa kusoma Hamlet , tamthilia mojawapo maarufu kabisa ya Shakespeare. Kila ninapokumbuka tamthilia hii, ninakumbuka nilivyoangalia filamu yake yapata mwaka 1971, Mkwawa High School, Iringa.  Sir Laurence Olivier aliigiza nafasi ya Hamlet, kama nilivyogusia katika blogu hii. Miaka ile ya ujana, tulifahamu ki-Ingereza vizuri hadi kusoma maandishi ya Shakespeare na kuyafurahia. Shakespeare ni kipimo kizuri cha ufahamu wa ki-Ingereza. Umahiri wake katika kutumia maneno na kutunga sentensi unadhihirika katika tungo zake zote. Ninanukuu hapa hotuba ya Claudius, mfalme wa Denmark, kwa Hamlet, ambayo ni kielelezo cha umahiri huo: Tis sweet and commendable in your nature, Hamlet, To give these mourning duties to your father; But you must know, your father lost a father; That father lost, lost his, and the survivor bound In filial obligation for some term To do obsequious sorrow. But to

Nimeteuliwa Kwenye Bodi ya Rochester International Association

Image
Mwezi huu nimeteuliwa kujiunga na bodi ya Rochester International Association, ambayo makao yake ni mjini Rochester, Minnesota. Rochester International Association inashughulika na program mbali mbali za kujenga mahusiano mema miongoni mwa watu wa mataifa na tamaduni mbali mbali. Moja ya programu hizo ni tamasha liitwalo World Festival, linalofanyika kila mwaka. Nimewahi kushiriki tamasha hili mara mbili, nikaelezea habari zake katika blogu yangu ya ki-Ingereza, na blogu hii ya hapakwetu. Shughuli za bodi ni za kujitolea. Kwa miaka yote niliyoishi hapa Marekani, nimejionea jinsi wa-Marekani wanavyozijali shughuli za kujitolea, nami nimekuwa nikishiriki shughuli za aina hiyo, kama vile katika programu zinazowapeleka wanafunzi Afrika. Kujitolea kwa manufaa ya jamii kunaleta faraja na furaha moyoni. Kushiriki kwangu katika Rochester International Association kutaniwezesha kuchangia mawazo katika masuala ya tamaduni kama nilivyoyaelezea katika kitabu changu, Africans and Ameri

Buriani Mwandishi John Calvin Rezmerski

Image
Leo hapa Minnesota zimeenea taarifa za kufariki kwa mwandishi John Calvin Rezmerski. Taarifa moja imechapishwa katika Minneapolis Star Tribune . Nilipata bahati ya kuonana naye miaka michache iliyopita mjini Mankato, Minnesota, kwenye tamasha la vitabu, Deep Valley Book Festival. Tuliongea, nikanunua kitabu chake cha mashairi kiitwacho What Do I Know?: New & Selected Poems , ambacho alikisaini hivi: for Joseph Mbele-- Wonderful to talk with you at Deep Valley Book Festival, John Calvin Rezmerski Taarifa tulizopata leo zinaelezea mambo mema mengi ya bwana Rezmerski: alikuwa mwandishi makini wa mashairi, msimuliaji hadithi, mwalimu aliyependwa, mkarimu kwa watu. Kuhusu falsafa ya ushairi ya Rezmerski, Bill Holm, ambaye ni mwandishi maarufu hapa Minnesota, aliwahi kuandika: "John Rezmerski believes that poetry lives inside the daily speech of ordinary people, that the ear and the mouth are connected to the imagination and the heart." Dhana hiyo ya ushairi inanikum

Mteja wa Uingereza Kanunua Kitabu

Image
Leo kwenye tovuti ninapochapisha vitabu vyangu nimeona kuwa mteja aliyeko Uingereza amenunua nakala ya Notes on Achebe's Things Fall Apart . Uzuri wa uchapishaji wa namna hii ninayotumia ni kuwa mwandishi unaweza kufuatilia taarifa kama hizi za mauzo, ukajua kitabu kimenunuliwa sehemu gani ya dunia, nakala ngapi, na malipo yako ni kiasi gani. Kwa miaka yote tangu nilipoanza kuchapisha vitabu kwenye tovuti ya lulu.com maelfu ya wateja walionunua vitabu vyangu wamefanya hivyo kutokea hapa Marekani. Nilikuwa na hisia kuwa hii ni kwa kuwa utamaduni wa kununua vitu mtandaoni ulikuwa bado kujengeka sehemu zingine za dunia. Ninahisi kuwa huyu mteja aliyenunua Notes on Achebe's Things Fall Apart ni mwalimu wa fasihi. Kama ni hivyo, ninafurahi kuwa atapata mawazo mapya juu ya Things Fall Apart . Ingawa kuna miongozo mingi ya Things Fall Apart , mwongozo wangu umepata umaarufu hata ukateuliwa kama mwongozo kwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Cornell, ambacho kina jina kubwa

Nimenunua Webster's Concise Dictionary and Thesaurus

Image
Jana nilinunua nakala ya Webster's New World Concise Dictionary and Thesaurus , iliyochapishwa mwaka 2014. Hili ni toleo jipya la kitabu hiki ambacho kimekuwa kikichapishwa kwa miaka mingi. Kitabu hiki ni hazina ya pekee kwa kuwa kinajumlisha kamusi na "thesaurus." Kwa wale wasiofahamu tofauti za vitu hivi viwili, napenda kusema kwa kifupi kwamba kamusi hutoa tafsiri za maneno. "Thesaurus," badala ya kutoa tafsiri ya neno, huorodhesha maneno ambayo maana zake zinafanana au kukaribiana na neno hilo. Kwa mfano, katika kitabu nilichonunua leo, sehemu ya thesaurus, neno "docile" limewekewa maneno yafuatayo: "meek, mild, tractable, pliant, submissive, accommodating, adaptable, resigned, agreeable, willing, obliging, well-behaved, manageable, tame, yielding, teachable, easily influenced, easygoing, usable, soft, childlike." Mfano huu unaonyesha wazi ubora na upekee wa "thesaurus." Kwa kuyaorodhesha maneno yenye maana zinazofanan

Black African Voices: Tungo za Afrika

Image
Pamoja na kwamba fasihi ya Afrika, kama ilivyo ulimwenguni kote, inastawi kwa kasi kadiri miaka inavyopita, na waandishi wapya hujijokeza na kujipambanua, ni lazima pia kukumbuka na kusoma uandishi wa zamani. Kwa yeyote anayependa fasihi, awe ni mwanafunzi, mwalimu au msomaji wa kawaida, usomaji wa aina hii ni jambo lisilohitaji mjadala. Fasihi inahitaji usomaji usio na kikomo, sio tu kwa kuwa ina historia ndefu, bali pia kwa kuwa inastawi ulimwenguni kote na daima inaendelea kuchanua kama maua. Mimi, mwalimu wa fasihi, ninazingatia umuhimu wa kufundisha kazi za tangu zamani hadi leo. Fasihi ya kila taifa au sehemu yoyote ya dunia ina historia, na fasihi inayoandikwa leo ni mwendelezo wa mkondo ulioanza zamani. Katika siku hizi chache, nimekuwa ninasoma Black African Voices , kitabu kilichohaririwa na James E. Miller na wenzake. Sikumbuki ni lini nilikinunua kitabu hiki, lakini mara kwa mara katika kuangalia vitabu vyangu, nilikuwa ninakichungulia kitabu hiki, nikawa ninakumbuk

Miaka 80 ya "The Snows of Kilimanjaro"

Image
Kwa mara nyingine tena, ninaandika ujumbe kuhusu kutimia kwa miaka 80 tangu hadithi ya Ernest Hemingway, 'The Snows of Kilimanjaro" ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. Niliandika ujumbe wa aina hiyo katika blogu hii. Leo nimesoma tena ujumbe wangu, nikajiridhisha kwamba niliyosema ndiyo ninayoamini hadi sasa. Jambo moja kubwa kabisa ni kuwa wa-Tanzania tunajipotezea fursa za wazi za kutumia hazina kama hii hadithi ya Hemingway kuitangaza nchi yetu. Niliandika katika ujumbe wangu baadhi ya mambo ambayo tungeyafanya mwaka huu wa kumbukumbu. Lakini mwaka unaelekea ukingoni, na hakuna tulichofanya. Hii ni hasara ya kukosa utamaduni wa kusoma vitabu. Tunashindwa hata kutumia fursa zilizo wazi. Nimeona niandike ujumbe huu leo kwa sababu wiki hii, hapa katika Chuo cha St. Olaf ninapofundisha, litatokea jambo la pekee linalohusiana na Ernest Hemingway. Keshokutwa, tarehe 28, pataonyeshwa kwa mara ya kwanza filamu ya "Papa's Shadow," ambayo niliwahi kuielezea katika

Ninarekebisha Kitabu Nilichochapisha Mtandaoni

Image
Mara kwa mara, ninaongelea suala la kuchapisha vitabu mtandaoni, kutokana na uzoefu wangu. Ninatarajia kuwapa wengine uzoefu wangu wa kutumia tekinolojia za uchapishaji mtandaoni, ambazo zinatoa fursa tele kwa yeyote kujikomboa na taabu na vikwazo vya uchapishaji wa jadi. Faida mojawapo ya uchapishaji wa aina ninayotumia kuchapishia vitabu vyangu ni fursa isiyo na mipaka ya kurekebisha kitabu chako wakati wowote uonapo dosari ndani yake au fursa ya kukiboresha. Hilo linawezekana kwa kuwa mswada wako unakuwa umehifadhiwa kama faili la kielektroniki mtandaoni, hata kama hukuuhifadhi katika kompyuta, disketi, au kifaa kingine. Mimi ninatumia mtandao wa lulu.com. Hapo, ukishachapisha kitabu, nakala ya mswada inahifadhiwa hapo hapo mtandaoni. Unapotaka kurekebisha kitabu chako, unachofanya ni kuuingiza "(down-loading") mswada katika "flash drive" na kuufanyia marekebisho. Kisha unaurudisha ("up-loading") sehemu ya kuchapishia. Yeyote atakayekinunua baa

Siku ya Mashujaa wa Kenya, Rochester, Minnesota

Image
Jana nilikwenda mjini Rochester, Minnesota, kuhudhuria sherehe ya siku ya Mashujaa wa Kenya. Hii ni sikukuu ambayo wa-Kenya huifanya kila mwaka tarehe 20 Oktoba, kuwakumbuka mashujaa wa tangu enzi za kupigania uhuru hadi leo. Sherehe ya jana iliandaliwa na jumuia ya wa-Kenya waishio Rochester. Nilipata taarifa ya sikukuu hii kutoka kwa Olivia Njogu, m-Kenya aishiye Rochester, na mwanabodi wa  Rochester International Association . Anaonekana pichani hapa kushoto, wa pili kutoka kulia. Chama hiki huandaa tamasha la kimataifa kila mwaka, na Olivia tulifahamiana niliposhiriki tamasha hilo mwaka huu, kama nilivyoelezea  katika blogu hii.  Baada ya tamasha, Olivia alisoma kitabu changu  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , na kisha akaniandikia kunielezea alivyokipenda. Taarifa hiyo niliiandika katika blogu hii.   . Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kuhudhuria sherehe za wa-Kenya hapa Marekani. Daima nimependezwa kujumuika nao, kama nilivyowahi kuandika katika blog