Kwa wenye kuifahamu fasihi ya ki-Ingereza, jina la Emily Bronte linafahamika vizuri. Emily na dada zake Charlotte na Anne ni waandishi maarufu wa mashairi na riwaya. Emily anafahamika zaidi kwa riwaya yake, Wuthering Heights, na Charlotte anafahamika kwa riwaya yake, Jane Eyre. Katika kukua kwangu na kusoma fasihi Tanzania, nilikuwa ninawafahamu hao dada wawili, lakini si mdogo wao Anne, ambaye nimekuja kuelewa baadaye kwamba naye alikuwa mwandishi wa mashairi na riwaya. Hao dada watatu, maarufu kama "the Bronte Sisters," ni maarufu katika fasihi ya ki-Ingereza.
Hizo ni kumbukumbu za juu juu kuhusu hao dada watatu. Lakini leo ninaleta shairi moja la Emily, ambalo nimelisoma kwa mara ya kwanza wiki hii. Limenivutia sana kwa jinsi linavyofikirisha kutokana na mbinu zake za kuwasilisha mtazamo juu ya kitu kinachoitwa matumaini. Tofauti na ufahamu wetu wa kitu kiitwacho matumaini, shairi linayaelezea matumaini kama si kitu cha kuaminiwa au kutegemewa. Mshairi anayaelezea matumaini kama si rafiki wa imara wa kuaminiwa, bali ni kitu kisichojali hali yake ngumu, chenye mizengwe, na hatimaye chatoweka na kumwacha kwenye mataa, kama wasemavyo watu mitaani. Ili kulitendea haki shairi hili, bora kila mtu ajisomee na kutafakari.
Hope
Hope was but a timid friend;
She sat without the grated den,
Watching how my fate would tend,
Even as selfish-hearted men.
She was cruel in her fear;
Through the bars, one dreary
day,
I looked out to see her there,
And she turned her face away!
Like a false guard, false watch keeping,
Still, in strife, she whispered peace;
She would sing while I was weeping;
If I listened, she would cease.
False she was, and unrelenting;
When my last joys strewed the ground,
Even Sorrow saw, repenting,
Those sad relics scattered round;
Hope, whose whisper would have given
Balm to all my frenzied pain,
Stretched her wings, and soared to heaven,
Went, and ne'er returned again!
Showing posts with label shairi. Show all posts
Showing posts with label shairi. Show all posts
Friday, September 1, 2017
Saturday, May 27, 2017
"Witchcraft by a Picture" (John Donne)
Juzi, nilinunua kitabu cha mashairi kiitwacho The Works of John Donne, kama nilivyosema katika blogu hii. John Donne aliishi Uingereza, hasa London, miaka ya 1572-1631.Katika kuyasoma mashairi yake, nimeona kuwa yanahitaji utulivu wa pekee, na tafakari, kwani matumizi yake ya lugha yanaonyesha uangalifu mkubwa. Ki-Ingereza chake ni cha miaka ile, ambayo ni miaka ya William Shakespeare, si cha leo. Hapa naleta shairi mojawapo, "Witchcraft by a Picture." Labda siku moja nitapata ujasiri wa kujaribu kulitafsiri kwa ki-Swahili.
Witchcraft by a Picture
I fixe mine eye on thine, and there
Pitty my picture burning in thine eye,
My picture drown'd in a transparent teare,
When I looke lower I espie;
Hadst thou the wicked skill
By pictures made and mard, to kill,
How many wayes mightst thou performe thy will?
But now I have drunke thy sweet salt teares,
And though thou poure more I'll depart;
My picture vanish'd, vanish feares,
That I can be endamag'd by that art;
Though thou retaine of mee
One picture more, yet that will bee,
Being in thine owne heart, from all malice free.
Saturday, February 25, 2017
Tafsiri Yangu ya "A Time to Talk" (Robert Frost)
Leo nimetafsiri shairi fupi la Robert Frost, "A Time to Talk." Hili ni shairi nililolisoma kwa mara ya kwanza miaka mitatu iliyopita, baada ya binti yangu Zawadi kuninunulia kitabu cha mashairi ya Frost, Robert Frost: Selected Poems. Kama nilivyoelezea katika blogu hii, nilikuwa nimelazwa hospitalini mjini Minneapolis, na binti yangu, kwa kujua ninavyopenda vitabu, alininunulia hiki kitabu kinisaidie kukabili hali niliyokuwemo.Shairi hili la "A Time to Talk" lina mawaidha mazito kuhusu maisha. Linatukumbusha umuhimu wa uungwana na ukarimu katika mahusiano yetu binadamu. Tuache fikra ya kwamba hatuna muda wa kujumuika na wenzetu, kujuliana hali, na kadhalika. Robert Frost anavyoelezea mambo katika shairi hili ananikumbusha maisha ya vijijini, ambayo niliishi tangu utotoni. Kusalimiana ni wajibu, na watu hutumia muda kujuliana hali.
Bila shaka, Frost anaukosoa utamaduni wa ubinafsi, na utamaduni wa kila mtu na maisha yake. Anaikosoa hali ambayo wanafalsafa kama Karl Marx na wafuasi wake wameiongelea vizuri kwa kutumia dhana ya "alienation." Anavyoongelea kuhusu kuwa na muda wa kuongea na wenzetu, ninaona kuwa Frost anaikejeli jamii ambayo imejiaminisha kuwa muda ni hela ("time is money"). Ninavyosema hayo mambo yanayohusu utamaduni, kama yalivyoelezwa katika shairi hili, ninakumbuka nilivyoyaelezea katika kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Kwa kumalizia, napenda nirudie jambo ambalo ninalitamka daima. Kutafsiri kazi ya fasihi ni shughuli ngumu yenye mitego na vipingamizi vingi. Nilivyojaribu kulitafsiri shairi la Frost, simaanishi kuwa tafsiri yangu ndio kilele cha ufanisi. Msomaji makini anayezifahamu vizuri sana lugha za ki-Ingereza na ki-Swahili, na sio lugha tu, bali lugha ya kifasihi, bila shaka ataona vipengele ambayo vingeweza kuboreshwa. Kwa mfano, katika mstari wa pili, utatafsirije "a meaning walk," ili uziwasilishe kwa ki-Swahili dhana zilizomo katika huo usemi wa ki-Ingereza?
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
A TIME TO TALK (Robert Frost, 1874-1963)
When a friend calls to me from the road
And slows his horse to a meaning walk,
I don't stand still and look around
On all the hills I haven't hoed,
And shout from where I am, What is it?
No, not as there is a time to talk.
I thrust my hoe in the mellow ground,
Blade-end up and five feet tall,
And plod: I go up to the stone wall
For a friendly visit.
MUDA WA MAONGEZI
Rafiki anaponiita kutoka barabarani
Huku akipunguza kwa makusudi mwendo wa farasi wake,
Sisimami tu na kuangalia huko na huko
Kubaini idadi ya vilima ambavyo bado sijalima
Na kisha kupaaza sauti pale nilipo, Vipi?
Hapana, hapana kwani kuna muda wa kuongea.
Nasimika jembe langu katika ardhi tepetepe,
Ubapa wa jembe ukiwa juu futi tano toka ardhini,
Na ninatembea taratibu: ninaelekea kwenye ukuta wa mawe
Kukutana na rafiki.
Friday, February 24, 2017
Ninafurahia Kusoma "Eugene Onegin"
Siku chache zilizopita, niliandika kuwa utungo wa Pushkin, Eugene Onegin, ni mtihani. Madhumuni ya kuandika taarifa ile ilikuwa ni kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wangu, sio kufanya uchambuzi au tathmini ya utungo. Nilivyotaja dhana ya mtihani, nilimaanisha kuwa utungo huo unahitaji tafakari ya dhati kuelewa vizuri. Wazo hilo lilijengeka akili mwangu wakati nasoma sura ya kwanza ya Eugene Onegin.Lakini lazima nikiri pia kuwa kuna beti ambazo hazihitaji juhudi kubwa kuzielewa. Kwa kuwa ninasoma tafsiri, siwezi kujua kama ugumu unatokana na utungo wa asili au tafsiri. Kwa pamoja, ingawa ni tafsiri, hizi beti zote zinavutia kwa ukwasi wa sanaa. Mfano ni beti mbili za mwanzo wa sura ya pili ya Eugene Onegin:
They bored Onegin past all measure
These woodlands, though a charming spot.
A friend of innocent, sweet pleasure
Might well thank Heaven for this plot.
The lonely manor found protection
From wind in hills, and in reflection
It danced upon the brook below.
The distant meadows' blurry glow
Was gold from untold blooms collected.
Far hamlets glistened through the air,
And flocks sought pasture here and there.
A garden, grand but long neglected,
Was choked with weeds grown thick and tight:
Fine shelter for a dreamy sprite.
The stately manse had been erected
As manses ought to be: to last.
'Twas solid, tranquil, well-protected:
A tasteful tribute to the past.
The rooms were high and overawing,
And in the drawing-room, some drawing --
Tsarina, tsar -- graced every tall
And plushly damask-covered wall.
The ovens featured flow'ry tiles.
Although this sounds passe today,
The reason why, I can't quite say.
At any rate, to all such styles
The squire was equally undrawn:
At old rooms, new rooms, he'd just yawn.
Katika beti hizi, tunaona kuwa Onegin, ambaye ndiye mhusika mkuu, ni mtu wa ajabu. Mazingira ambayo yangemvutia binadamu mwingine, yeye hayamshitui, wala haoni mvuto wake. Mazingira haya yanaelezwa kwa mtindo unaonikumbusha mkondo wa fasihi uitwao "Romanticism," kama inavyodhihirika, kwa mfano, katika shairi la William Wordsworth, "Lines Composed a Few Miles Above Tintern Abbey," ambalo linaanza hivi :
Five years have past; five summers, with the length
Of five long winters! and again I hear
These waters, rolling from their mountain-springs
With a soft inland murmur.--Once again
Do I behold these steep and lofty cliffs,
That on a wide secluded scene impress
Thoughts of more deep seclusion; and connect
The landscape with the quiet of the sky.
Pushkin alifahamu fasihi za mataifa mbali mbali, kama nilivyogusia katika blogu hii.
Hata hao waandishi wa mkondo wa "Romanticism" aliwafahamu. Kwa mfano, katika sura ya pili ya Eugene Onegin, kwa mfano, Pushkin anawataja Goethe na Schiller, waandishi maarufu wa Ujerumani.
Sunday, January 1, 2017
Shari ya Mwaka Mpya: "The Second Coming"
Kwa kawaida, kwa kuwa wasomaji wengi wa blogu hii ni wa-Tanzania wenzangu, tunavyoanza mwaka mpya, ningewatakia heri ya mwaka mpya. Badala yake, kwa kuzingatia tunakoelekea kisiasa, ninaleta shairi la William Butler Yeats, "The Second Coming," ambalo niliwahi kuliweka katika blogu hii. Angalau kwa jinsi ninavyolisoma shairi hili, ninaona lina ujumbe unaofaa zaidi kuliko "heri ya mwaka mpya."
The Second Coming
Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst
Are full of passionate intensity.
Surely some revelation is at hand;
Surely the Second Coming is at hand.
The Second Coming! Hardly are those words out
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
A shape with lion body and the head of a man,
A gaze blank and pitiless as the sun,
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds.
The darkness drops again; but now I know
That twenty centuries of stony sleep
Were vexed to nightmare by a rocking cradle,
And what rough beast, its hour come round at last,
Slouches towards Bethlehem to be born?
Source: The Collected Poems of W. B. Yeats (1989)

Friday, December 9, 2016
The Rime of the Ancient Mariner: Samuel Taylor Coleridge
Jana na leo nimesoma The Rime of the Ancient Mariner, utenzi maarufu wa Samuel Taylor Coleridge, ambao ni moja ya tungo za ki-Ingereza nilizokuwa ninazipenda wakati wa ujana wangu, kama nilivyoandika katika blogu hii. Nimefurahi kuusoma tena, baada ya miaka mingi, wakati ambapo akili yangu imepevuka zaidi kutokana na kusoma tungo nyingi za fasihi.Katika kusema hivi, ninakumbuka kauli ya mshairi William Wordsworth, katika shairi lake maarufu, "Lines Written a Few Miles Above Tintern Abbey," anavyoongelea namna alivyotembelea, katika utu uzima wake, eneo ambalo alilizoea alipokuwa kijana. Matokeo ya kufanya hivyo ni kwamba, ingawa hawezi tena kuyaona mazingira yale kwa hisia za ujanani, sasa anayaona kwa kutumia akili ya kiutu uzima. Aina zote mbili za maono anazienzi, ingawa zinatofautiana.
Nami ninajisikia hivyo hivyo katika kusoma wakati huu The Rime of the Ancient Mariner. Nimeweza kuuweka utungo huu katika mkabala wa tungo nilizosoma kwa miaka ya baina ya ujana wangu na umri nilio nao sasa. Ninawazia hadithi ya kale ya Misri iitwayo, "The Tale of the Shipwrecked Sailor," utenzi wa Odyssey wa Homer, hadithi za baharia Sindbad, riwaya ya Daniel Defoe, Robinson Crusoe; riwaya ya Herman Melville, Moby Dick; na Utenzi wa Masaibu.
It is an ancient Mariner,
And he stoppeth one of three.
'By thy long grey beard and glittering eye,
Now wherefore stopp'st thou me?
'The Bridegroom's doors are opened wide,
And I am next of kin;
The guests are met, the feast is set:
May'st hear the merry din.'
He holds him with his skinny hand,
'There was a ship,' quoth he.
'Hold off! unhand me, grey-beard loon!'
Eftsoons his hand dropt he.
He holds him with his glittering eye--
The Wedding-Guest stood still,
And listens like a three years' child:
The Mariner hath his will.
Kuanzia hapo, huyu baharia mkongwe anamsimulia kijana yaliyomsibu katika safari baharini, yeye na mabaharia wenzake. Ni kisa cha mikosi, majanga na vifo vya wenzake wote akasalimika yeye, na tangu hapo katika maisha yake, hupatwa na maumivu fulani nafsini mwake ambayo suluhu yake ni kumnasa mtu wa kumsimulia kisa chake.
The Rime of the Ancient Mariner ni kisa cha kusisimua. Coleridge anazisukuma hisia zetu kupitia hali mbali mbali: mshangao, hofu, masikitiko, na huruma. Pamoja na kwamba hatimaye tunafarijika kwa jinsi mzee huyu alivyonusurika, tunabaki na majonzi kwa vifo vya mabaharia wenzake. Baada ya kuelewa kisa kizima, tunaelewa kwa nini mzee huyu anamteka kwa uchawi wa macho yake kijana anayekwenda arusini na kumfanya asikilize kisa chake hadi mwisho.
Thursday, November 24, 2016
"A Far Cry From Africa," Shairi la Derek Walcott
Tangu nilipoanza kufundisha katika chuo cha St. Olaf, mwaka 1991, nimepata fursa ya kusoma na kufundisha fasihi iliyoandikwa kwa ki-Ingereza kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyowezekana nilipokuwa ninafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwandishi mmojawapo ambaye kazi zake nimezishughulikia sana ni Derek Walcott wa St. Lucia, pande za Caribbean, maarufu kwa utunzi wa mashairi na tamthilia, ambaye alipata tuzo ya Nobel mwaka 1992.Nimesoma na kufundisha mashairi yake mengi na tamthilia zake kadhaa. Moja ya mashairi hayo ni "A Far Cry From Africa," ambalo lilichapishwa mwaka 1962. Linaelezea mahuzuniko juu ya vita ya Mau Mau nchini Kenya iliyodumu kuanzia mwaka 1952 hadi 1960. Masetla wazungu walipigana na wa-Afrika waliotaka kuchukua ardhi yao iliyoporwa. Kwa kuwa Derek Walcott ni chotara, damu ya kizungu na ki-Afrika, alihisi vita hiyo ikitokea ndani ya nafsi yake. Uhasama na ukatili wa pande hizo mbili aliuhisi mithili ya sumu katika mishipa ya damu yake. Alijihisi kama mateka aliyekosa namna ya kujinasua.
Walcott anaimudu lugha ya ki-Ingereza kwa namna inayonikumbusha umahiri wa Shakespeare. Nitafurahi iwapo nitapata ujasiri wa kujaribu kulitafsiri shairi kwa ki-Swahili.
-------------------------------------------------------------------------------
A Far Cry From Africa
Derek Walcott
A wind is ruffling the tawny pelt
Of Africa, Kikuyu, quick as flies,
Batten upon the bloodstreams of the veldt.
Corpses are scattered through a paradise.
Only the worm, colonel of carrion, cries:
'Waste no compassion on these separate dead!'
Statistics justify and scholars seize
The salients of colonial policy.
What is that to the white child hacked in bed?
To savages, expendable as Jews?
Threshed out by beaters, the long rushes break
In a white dust of ibises whose cries
Have wheeled since civilizations dawn
From the parched river or beast-teeming plain.
The violence of beast on beast is read
As natural law, but upright man
Seeks his divinity by inflicting pain.
Delirious as these worried beasts, his wars
Dance to the tightened carcass of a drum,
While he calls courage still that native dread
Of the white peace contracted by the dead.
Again brutish necessity wipes its hands
Upon the napkin of a dirty cause, again
A waste of our compassion, as with Spain,
The gorilla wrestles with the superman.
I who am poisoned with the blood of both,
Where shall I turn, divided to the vein?
I who have cursed
The drunken officer of British rule, how choose
Between this Africa and the English tongue I love?
Betray them both, or give back what they give?
How can I face such slaughter and be cool?
How can I turn from Africa and live?
Saturday, November 19, 2016
"Ozymandias:" Shairi la Shelley na Tafsiri Yangu
Percy Bysshe Shelley ni mmoja kati ya washairi maarufu kabisa katika ki-Ingereza, ambaye nilimtaja jana katika blogu hii. Alizaliwa mwaka 1792 akafariki mwaka 1822. Ni mmoja wa washairi wanaojumlishwa katika mkondo uitwao "Romanticism," ambamo wanaorodheshwa pia washairi wa ki-Ingereza kama William Blake, William Wordsworth, Samuel Taylor Coleridge, na Lord Byron. "Romanticism" ni mkondo uliojitokeza katika mataifa na lugha zingine pia, kama vile Ujerumani na Ufaransa. Kwa waandishi wa Afrika au wenye asili ya Afrika waliotumia ki-Faransa, "Romanticism" ilijitokeza kama "Negritude," jambo ambalo nimeelezea katika mwongozo wa Song of Lawino.
"Ozymandias" ni shairi mojawapo maarufu la Shelley. Ninakumbuka kuwa nililisoma kwa mara ya kwanza nilipokuwa sekondari, miaka ya kuanzia 1967. Kitu kimoja kinacholitambulisha shairi hili kuwa ni la mkondo wa "Romanticism" ni ule mtazamo wake ambao Edward Said aliuita "Orientalism." Lengo langu hapa si kuongelea "Romanticism" wala "Orientalism," bali kutaja mambo mawili matatu yanayohusu shairi la "Ozymandias" na suala la tafsiri.
Suala la kutafsiri kazi za fasihi nimeliongea tena na tena katika blogu hii. Pamoja na ugumu wake, ninaona kuwa baada ya mahangaiko yote, inakuja raha ya aina yake. Sio raha au furaha inayotujia tunaposhinda shindano au mtihani, kwani katika kutafsiri hakuna ushindi. Kinachotokea ni kuwa mtu unafanikiwa kuuzalisha upya utungo unaowania kuutafsiri.
"Ozymandias" ni shairi ambalo ninalielewa vizuri kabisa lilivyo katika ki-Ingereza. Lakini, nilivyojaribu kulitafsiri, tangu jana, limenihangaisha. Nimejionea jinsi ufahamu wangu wa ki-Swahili unavyopwaya. Nimejikuta nikijiuliza iwapo madai yetu wa-Tanzania kuwa tunakifahamu vizuri ki-Swahili ni ya kweli au ni porojo. Nilipata taabu zaidi kutafsiri mstari wa tano na mistari mitatu ya mwisho. Pamoja na kwamba nimeweka tafsiri yangu hapa, siridhiki nayo.
Kuhusu dhamira, shairi la "Ozymandias" lina mengi ya kujadiliwa. Kwa mtazamo wa fasihi linganishi, dhamira ya kisa cha msafiri inajitokeza katika tungo nyingi za tangu zamani. Mfano moja ni hadithi ya Misri ya kale iitwayo "The Tale of the Shipwrecked Sailor." Kuna pia hadithi za baharia Sindbad. Pia kuna shairi la Samuel Taylor Coleridge, "The Rime of the Ancient Mariner." Tungo zote hizi zina mambo ya ajabu na mtazamo juu ya ulimwengu na tabia za binadamu.
Vile vile, "Ozymandias" ni shairi lenye ujumbe mzito. Ni onyo kwa wanadamu kuwa utukufu wa hapa duniani, uimara wa himaya au udikteta ni vitu ambavyo vina mwisho. Ujumbe huu umo pia katika tungo zingine maarufu, kama vile utenzi wa Al Inkishafi. Naishia hapo.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ozymandias
Percy Bysshe Shelley, 1792-1822
Imesimama jangwani....Karibu nayo, mchangani,
Ukiwa umezama nusu, uso uliopasuka vipande umelala, mnuno wake,
Na mdomo uliokunyata, na dhihaka ya mamlaka yabisi
Vyabainisha kwamba mchongaji alizifahamu sawasawa hisia zile
Ambazo bado zimedumu, zikiwa zimebandikwa katika vitu hivi visivyo hai,
Mkono uliovidhihaki, na moyo uliovilisha,
Na kwenye sehemu ya kusimamia yanaonekana maneno haya:
'Jina langu ni Ozymandias, Mfalme wa Wafalme:
Yaoneni niliyofanikisha, enyi wenye mamlaka makuu, mkate tamaa!'
Hakuna kilichosalia, pembeni mwa uharibifu
Wa ile sanamu kuu iliyoporomoka, bila upeo bila chochote
Mchanga mpweke umetanda hadi mbali kabisa."

I met a traveller from an antique land,
Who said: "Two vast and trunkless legs of stone
Stand in the desert.... Near them, on the sand,
Half sunk, a shattered visage lies, whose frown,
And wrinkled lip, and sneer of cold command,
Tell that its sculptor well those passions read
Which yet survive, stamped on these lifeless things,
The hand that mocked them, and the heart that fed;
And on the pedestal, these words appear:
'My name is Ozymandias, King of Kings;
Look on my Works, ye Mighty and despair!'
Nothing beside remains. Round the decay
Of that colossal Wreck, boundless and bare
The lone and level sands stretch far away."
Tafsiri
Nilimkuta msafiri kutoka nchi ya kale
Ambaye alisema, "Miguu miwili ya mawe mikubwa sana isiyo na kiwiliwiliWho said: "Two vast and trunkless legs of stone
Stand in the desert.... Near them, on the sand,
Half sunk, a shattered visage lies, whose frown,
And wrinkled lip, and sneer of cold command,
Tell that its sculptor well those passions read
Which yet survive, stamped on these lifeless things,
The hand that mocked them, and the heart that fed;
And on the pedestal, these words appear:
'My name is Ozymandias, King of Kings;
Look on my Works, ye Mighty and despair!'
Nothing beside remains. Round the decay
Of that colossal Wreck, boundless and bare
The lone and level sands stretch far away."
Tafsiri
Nilimkuta msafiri kutoka nchi ya kale
Imesimama jangwani....Karibu nayo, mchangani,
Ukiwa umezama nusu, uso uliopasuka vipande umelala, mnuno wake,
Na mdomo uliokunyata, na dhihaka ya mamlaka yabisi
Vyabainisha kwamba mchongaji alizifahamu sawasawa hisia zile
Ambazo bado zimedumu, zikiwa zimebandikwa katika vitu hivi visivyo hai,
Mkono uliovidhihaki, na moyo uliovilisha,
Na kwenye sehemu ya kusimamia yanaonekana maneno haya:
'Jina langu ni Ozymandias, Mfalme wa Wafalme:
Yaoneni niliyofanikisha, enyi wenye mamlaka makuu, mkate tamaa!'
Hakuna kilichosalia, pembeni mwa uharibifu
Wa ile sanamu kuu iliyoporomoka, bila upeo bila chochote
Mchanga mpweke umetanda hadi mbali kabisa."
Wednesday, October 5, 2016
Tafsiri ya "Ye Tradefull Merchants," Shairi la Edmund Spencer
Siku kadhaa zilizopita nilichapisha mashairi mawili ya Edmund Spencer katika blogu hii. Nilivutiwa na wazo la kuyatafsiri mashairi haya, ingawa magumu, ili kuchangamsha akili yangu na kujipima ufahamu wangu wa lugha.Siku ile ile, nilijaribu kutafsiri "Ye Tradefull Merchant," tangu mwanzo hadi mwisho, halafu nikaamua kuiweka kando tafsiri yangu, kwa kuwa sikuridhika na namna nilivyotafsiri vipengele viwili vitatu. Leo, bila kutegemea wala kupangia, nimepata hamu ya kurekebisha vipengele hivyo.
Ninafahamu kwamba, kwa mujibu wa nadharia za tafsiri, tafsiri ni dhana tata. Kutafsiri ni sawa na kujaribu kukikamata kitu kinachoteleza sana. Kwa ujumla, tunajidanganya au tunadanganyana tunaposema tumetafsiri utungo wowote wa fasihi. Hata hivyo, kwa kuzingatia jadi yetu ya kujidanganya na kudanganyana, ninaleta tafsiri yangu ya "Ye Tradefull Merchants."
---------------------------------------------------------------------------------------------
YE TRADEFULL MERCHANTS (Edmund Spencer)
Ye tradefull merchants, that with weary toyle,
Do seeke most pretious things to make your gain,
And both the Indias of their treasures spoile,
What needeth you to seeke so farre in vaine?
For loe! my love doth in her selfe containe
All this worlds riches that may farre be found:
If saphyres, loe! her eies be saphyres plaine;
If rubies, loe! hir lips be rubies sound;
If pearles, hir teeth be pearls, both pure and round;
If yvorie, her forhead yvorie weene;
If gold, her locks are finest gold on ground;
If silver, her faire hands are silver sheene:
But that which fairest is but few behold,
Her mind, adornd with vertues manifold.
ENYI WAFANYA BIASHARA MAKINI
Enyi wafanya biashara makini, mnaomenyeka na kazi,
Mkitafuta vitu ghali kujipatia faida,
Na India zote mbili mwazipora utajiri wao,
Nini mnajisumbua kutafuta mbali kote huko?
Kwani, hakika, mpenzi wangu anao nafsini mwake,
Utajiri wote wa dunia upatikanao mbali huko:
Kama ni yakuti, lo! macho yake ni yakuti bayana;
Kama ni akiki, lo! midomo yake ni akiki murua;
Kama ni lulu, meno yake ni lulu, safi za mviringo;
Kama ni nakshi ya pembe ndovu, panda la uso wake linayo;
Kama ni dhahabu, nywele zake ni dhahabu bora ya ardhini;
Kama ni uzuri wa fedha, mikono yake ni mizuri hivyo:
Lakini kilicho kizuri kabisa na wachache wanakiona,
Ni akili yake, iliyojaa mema maridhawa.
Wednesday, December 9, 2015
Mtunzi Haji Gora Haji
Leo nimeamua kuongelea kifupi utunzi wa Haji Gora Haji wa Zanzibar, mmoja wa waandishi maarufu wa ki-Swahili wa zama zetu hizi. Nafurahi kuwa niliwahi kuonana naye mjini Zanzibar na kuzungumza naye. Panapo majaliwa, nitaandika taarifa ya mazungumzo yetu, ambayo yalihusu maisha yake katika sanaa. Ni muhimu kuutangazia ulimwengu kazi murua inayofanywa na watu wetu wenye vipaji kama Haji Gora Haji.
Nina vitabu vyake vinne: Kimbunga (Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press, 1994), Utenzi wa Visa vya Nabii Suleiman Bi Daudi (A.S.) (Zanzibar: Al-Khayria Press Ltd, 1999), Kamusi ya Kitumbatu (Zanzibar: Express Printing Services, 2006), na Siri ya Ging'ingi (Dar es Salaam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam, 2009).
Kadiri siku zinavyopita, wasomaji na wahakiki wanajitokeza na kuongelea uandishi wa Haji Gora Haji. Mifano ya kutambuliwa huko ni taarifa ya Amanda Leigh Lichtenstein, ya Ridder Samson, na ya Pascal Bacuez. Nami nimetafsiri mashairi yake mawili nikayachapisha hapa, hapa, na hapa.
Haji Gora Haji, kama walivyo watunzi wengi, wa zamani hadi leo, wamejengeka katika jadi ya fasihi simulizi. Wanaitumia jadi hii katika utunzi wao, iwe ni mashairi kama walivyofanya W.B. Yeats na Derek Walcott, au riwaya, kama walivyofanya Charles Dickens na Chinua Achebe, au tamthilia, kama walivyofanya William Shakespeare, Wole Soyinka na Ebrahim Hussein, au hadithi fupi, kama walivyofanya Lu Hsun na Ama Ata Aidoo.
Ni hivyo hivyo kwa Haji Gora Haji, kama nilivyowahi kutamka. Utumiaji wa mbinu, miundo, na hata dhamira zitokanazo na fasihi simulizi kunachangia uwezo wa tungo kugusa fikra na hisia za hadhira kwa namna ya pekee kutokana na kwamba fasihi simulizi ni urithi wa wanadamu wote. Maudhui yatokanayo na fasihi simulizi ni ya thamani kwa wanadamu wote.
Kuthibitisha zaidi namna Haji Gora Haji alivyojengeka katika fasihi simulizi, sikiliza anavyosimulia hadithi ya Paa na Pweza.

Thursday, October 29, 2015
Shairi la "Kimbunga" (Haji Gora Haji)
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasihi. Tofauti na inavyoeleweka katika jamii, kutafsiri ni suala pana kuliko kuwasilisha ujumbe kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine, bali ni kutunga upya kazi ya fasihi inayotafsiriwa. Hili suala linajadiliwa sana na wataalam wa lugha, fasihi, na falsafa. Pamoja na matatizo yote, ninapenda kuchemsha akili yangu kwa kutafsiri kazi za fasihi. Kwa mfano, nimetafsiri hadithi za ki-Matengo, na shairi la Mama Mkatoliki.
Hapa naleta shairi la Haji Gora Haji, mshairi maarufu wa Zanzibar, ambaye niliwahi kukutana naye. Shairi hilo ni "Kimbunga" ambalo limo katika kitabu chake kiitwacho Kimbunga. Jisomee shairi hilo na ujionee nilivyopambana na lugha katika kutafsiri. Ni mapambano, na kuna wakati unajikuta umepigwa butwaa au mwereka.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kimbunga
1. Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika
Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika
Kimeing'owa mibuyu, minazi kunusurika
Nyoyo zilifadhaika.
2. Yalizuka majabali, yakabirukabiruka
Zikadidimia meli, ngarawa zikaokoka
Kimbunga hicho kikali, mavumbi hayakuruka
Nyoyo zilifadhaika.
3. Nyumba kubwa za ghorofa, siku hiyo zimeruka
Zikenenda kwa masafa, kufikia kwa kufika
Vibanda vyao malofa, vyote vikasalimika
Nyoyo zikafadhaika.
4. Chura kakausha mto, maji yakamalizika
Pwani kulikuwa moto, mawimbi yaliyowaka
Usufi nusu kipeto, rikwama limevunjika
Nyoyo zikafadhaika.
5. Kuna kikongwe ajuza, viumbe kimewateka
Hicho kinamiujiza, kila rangi hugeuka
Wataokiendekeza, hilaki zitawafika
Nyoyo zikafadhaika.
A Hurricane
1. A hurricane once arrived in Siyu town
Sparing neither that one nor this one, it was sheer mayhem
It uprooted babobab trees, the coconut trees surviving
Hearts went panicking.
2. Big rocks turned up, tumbling over and over
Ships were sinking, while mere boats survived
Fearsome as the hurricane was, it raised no dust
Hearts went panicking
3. Great storied houses were blown away that day
They flew quite a distance, landing wherever they landed
The huts of the lowly, all survived intact
And hearts went panicking
4. The frog drained the river, the water all dried up
On the shore was conflagration, of the waves flaming
Half a container of kapok, broke the coolie's cart
And hearts went panicking
5. A wizened hag there was, who held beings captive
She is given to magical powers, changing hues at will
Those who let her be, perdition will be their lot
And hearts will go panicking.
Friday, May 20, 2011
"Mama m-Katoliki" (shairi kutoka India)
Uandishi wa ki-Ingereza wa India unafahamika zaidi katika tanzu ya riwaya na hadithi fupi, ingawa waandishi wa mashairi pia wapo, kama vile Kamala Das, Nissim Ezekiel na Jayanta Mahapatra. Leo wanafunzi wangu wa somo la fasihi ya Asia Kusini walifanya mtihani wa mwisho, na suali moja nililowapa lilihusu shairi la "Catholic Mother," lililotungwa na Eunice de Souza.
Suali nililowapa ni hili: "Discuss the poem, "Catholic Mother," by Eunice de Souza. Say what you want about it. In addition, compare the woman in this poem with Anil, a key character in Michael Ondaatje's Anil's Ghost."
Sijui kwa nini, baada ya mtihani kumalizika, nimepata wazo la kulitafsiri shairi hili na kuliweka hapa kwenye blogu yangu. Ingawa lugha aliyotumia mtunzi inaonekana ni ya kawaida tu, ameingiza tamathali za usemi kiurahisi, lakini kwa uhodari na kufikirisha. Amepenyeza na kuchochea uchambuzi wa masuala muhimu ya jamii, kama vile dini, udini na jinsia.
Vile vile, nimekuwa nikiangalia jinsi anavyotumia herufi kubwa na wakati mwingine herufi ndogo. Hili nalo ni suala la kufikiriwa. Kuna kejeli nzuri na ucheshi fulani ndani yake.
Kutafsiri kazi ya fasihi--iwe ni hadithi, riwaya, au shairi--ni suala tata na mtihani mkubwa. Ninajua ninalosema, kutokana na kusoma mawazo ya watalaam na pia kutokana na uzoefu wangu. Kwa kweli, dhana yenyewe ya tafsiri ni ndoto, kwani lugha zinatofautiana, na tafsiri yoyote ni lazima itofautiane kwa namna mbali mbali na utungo unaotafsiriwa. Hali hiyo inajitokeza katika tafsiri yangu ya shairi la "Catholic Mother."
Msomaji ambaye anafahamu vizuri ki-Ingereza na ki-Swahili ataweza kutambua namna ambayo yeye angetafsiri shairi hili. Ingekuwa vizuri kuona wengine wangetafsiri vipi shairi hili, nami nakaribisha michango hiyo.
Mimi kama m-Mkatoliki nimevutiwa na shairi hili. Nimejikuta nikitabasamu kwa jinsi mshairi anavyotusanifu sisi wa-Katoliki. Mshairi Eunice de Souza ni mwanamke, na ni m-Katoliki kutoka jamii ya wa-Goa. Alizaliwa Pune, India, mwaka 1940. Amestaafu kazi ya ualimu wa ki-Ingereza katika chuo cha Mtakatifu Xavier, mjini Mumbai. Soma hilo shairi lake, na tafsiri yangu:
Catholic Mother
Francis X. D’Souza
father of the year.
Here he is top left
the one smiling.
By the Grace of God he says
we’ve had seven children
(in seven years)
We’re One Big Happy Family
God Always Provides
India will Suffer for
her Wicked Ways
(these Hindu buggers got no ethics)
Pillar of the Church
says the parish priest
Lovely Catholic Family
says Mother Superior
the pillar's wife
says nothing.
---------------------------
Mama m-Katoliki
Francis X. D’Souza
baba wa mwaka.
Yuko hapa juu kushoto
anayetabasamu.
Kwa Neema ya Mungu anasema
tumejaaliwa watoto saba
(katika miaka saba)
Sisi ni Familia Moja Kubwa Yenye Furaha
Mungu Daima Anaruzuku
India Itateseka
kwa Mwenendo Wake Mbaya
(hao wa-Hindu mabwege hawana maadili)
Ni Nguzo ya Kanisa
asema baba paroko
Familia Murua ya ki-Katoliki
asema Mkuu wa Masista
mkewe nguzo
hasemi lolote.

Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Jina la Shaaban Robert ni maarufu miongoni mwa wa-Tanzania na wengine wa nchi zingine wanaokijua ki-Swahili. Lakini, tujiulize ni wa-Tanza...