Kwa siku kadhaa sasa, nimekuwa nikisoma Kimbunga, kitabu cha mashairi ya Haji Gora Haji wa Zanzibar. Sambamba na kusoma, nimevutiwa na wazo la kujaribu kuyatafsiri baadhi. Nimeshatafsiri shairi la "Kimbunga." Leo nimeona nitafsiri "Nyang'au." Ni shairi linalohusiana na fasihi simulizi, kama yalivyo mashairi na maandishi mengine kadhaa ya Haji Gora Haji. Kwa kuwawezesha wasomaji wa ki-Ingereza kuonja utunzi wa Haji Gora Haji, ninategemea kuchangia kumtangaza ulimwenguni mshairi huyu mahiri. Anastahili kuenziwa kwa kila namna.
Yeyote anayekijua ki-Swahili vizuri, na pia ki-Ingereza, atajionea ugumu wa mtihani niliojipa wa kutafsiri shairi hili. Ingawa nimejitahidi sana, siwezi kusema ninaridhika na tafsiri yangu. Jaribu nawe kulitafsiri shairi hili, upate maumivu ya kichwa, na pia raha ukifanikiwa.
Nyang'au
1. Fisi alikichakani, mtu kapita haraka
Kwa vile yuko mbiyoni, mkono unakwepuka
Ndipo akatumaini, karibu ya kuanguka
Mate yakimdondoka, kwa tamaa ya mkono
2. Kayanowa yake meno, tayari na kujiweka
Ukidondoka mkono, afike na kuudaka
Ajipatie vinono, ale na kufaidika
Mate yakimdondoka, kwa tamaa ya mkono
3. Kafata huku na kule, hakuwa mwenye kuchoka
Fisi nyuma mtu mbele, endako ajipeleka
Kungoja mkono ule, apate kunufaika
Mate yakimdondoka, kwa tamaa ya mkono
4. Hakujuwa kama vile, mkono kupeperuka
Ndiyo yake maumbile, si kwa kuwa wakwanyuka
Kafatia vile vile, kwa tamaa kumshika
Mate yakimdondoka, kwa tamaa ya mkono
5. Yule anayemfata, anakokwenda kafika
Ndoto aliyoiota, ikakosa uhakika
Mkono hakuupata, bure alihangaika
Majuto yakamfika, hakuupata mkono
The Hyena
1. The hyena was in the bush, when a man hurried past
Speeding as he was, his arm flagged about
Raising the hyena's hopes that soon it would fall off
He kept salivating, hungering for the arm
2. He sharpened his teeth, positioning himself properly
So that when the arm fell off, he should promptly catch it
And enjoy a tasty treat, eating to satisfaction
He kept salivating, hungering for the arm
3. He followed hither and thither, not one to tire of striving
Coming behind with the man ahead, the hyena trailed the man
Waiting for that arm, hoping to feast on it
He kept salivating, hungering for the arm
4. Little did he know, that for the arm to flap about
Was its natural wont, no harbinger of dismemberment
He nevertheless kept following, choking with desire
He kept salivating, hungering for the arm
5. The one he was following, reached his destination
The dream he had been dreaming, ended in uncertainty
The arm he failed to get, in vain had he striven
Deep regrets assailed him, for failing to get the arm.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment