Tuesday, November 3, 2015

"Equal Rights:" Wimbo wa Peter Tosh

Mimi ni shabiki mkubwa wa miziki ya aina mbali mbali, ikiwemo "reggae." Kati ya wana "reggae ninaowapenda sana ni Peter Tosh wa Jamaica, ambaye ni marehemu sasa. Wimbo wake mojawapo niupendao sana ni "Equal Rights." Nilianza kuusikia wimbo huu miaka zaidi ya 30 iliyopita. Ujumbe wake ni chemsha bongo ya aina fulani. Anasema "I don't want no peace; I need equal rights and justice," yaani "Sitaki amani; nahitaji usawa kwa wote na haki."
1 comment:

NN Mhango said...

Ndugu Mbele umenikumbusha mbali. Ni kweli heri kuwa na haki kwanza. Ukiwa na haki, itakuja amani ya kweli. Unaweza kuwa na amani feki kama ya Tanzania lakini ukadhulumiwa na kupumbazwa na upuuzi huu unaoitwa amani nchini kwetu. Sijui kama wanaopanga nyumba za kimaskini wakasumbuliwa na wenye nyumba, wamachinga wanaofukuzwa na migambo ya City, wanafunzi wanaokaa sakafuni, wagonjwa wanaolala wanne kitanda kimoja na wengine kama hao wanajua maana ya amani. Ukiwa na haki sawa hakuna atakayemnyonya mwenzake. Kimsingi Tosh aliimba kama vile alikuwa anaiona Tanzania na Afrika kwa ujumla ambapo amani ya nchi ni kwa watawala kuwala watawaliwa. Nimecheka nilipoona madikteta kama Mugabe, Museveni, Kagame na Kabila eti wanahudhuria kuapishwa kwa Makufuli. Baadaye nilijikuta nikijisuta baada ya kugundua kuwa CCM ni dikteta kuliko hata hao niliowashangaa.