Posts

Showing posts from August, 2014

Marekani Hata Wazee Wananunua na Wanasoma Vitabu

Image
Kama nilivyoandika katika blogu hii , nilishiriki tamasha la tamaduni za kimataifa lililofanyika mjini Faribault tarehe 23 mwezi huu. Kati ya mambo niliyoelezea ni shughuli niliyofanya ya kusaini vitabu, na kati ya picha nilizoweka, ni hiyo inayoonekana hapa kushoto, ambayo inamwonesha mama mmoja mzee niliyekuwa namsainia nakala ya Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , aliyokuwa ameinunua hapo hapo. Sijui kama jambo hili linaweza kutokea mahali kama Tanzania. Kule watu wanachojua ni kuwa vitabu ni kitu kinachowahusu wanafunzi, labda kiwe kitabu cha hadithi, hasa hadithi za kusisimua na za mapenzi. Vitabu vya maarifa ya aina yoyote vinachukuliwa kuwa ni kwa ajili ya wanafunzi, na hao wanafunzi wanatafuta vitabu vinavyotumika mashuleni. Hapa Marekani, hali ni tofauti. Hata wazee hununua na husoma vitabu. Ukienda kwenye maduka ya vitabu, utawaona. Kwenye matamasha ya vitabu, utawaona. Nenda maktabani, utawaona. Nasema hayo kutokana na uzoefu wangu. Nisiende mbal

Tamasha la Tamaduni Faribault, Minnesota, Agosti 23

Image
Tamasha la tamaduni za kimataifa lilifanyika mjini Faribault tarehe 23 mwezi huu, kama ilivyopangwa. Nilihudhuria. Kati ya mambo yaliyonivutia ni bendera za nchi mbali mbali. Mwanzoni bendera hizi zilikuwa kwenye jukwaa kuu. Washiriki wa tamasha ambao nchi zao ziliwakilishwa na bendera hizi walikuja kwenye jukwaa kuu, wakasema machache kuhusu bendera hizi na nchi zao. Baada ya hapo, waliandamana katika mstari mmoja wakiwa na bendera zao, kisha bendera zilisimikwa uwanjani, ambapo zilipepea muda wote wa tamasha. Kama nilivyosema katika blog hii , kabla ya siku ya tamasha, sikuwa na bendera ya Tanzania. Kwa hivi, sikushiriki shughuli hii ya bendera. Yalikuwepo mabanda mengi ambamo vitu mbali mbali vilikuwa vinauzwa, kama vile vyakula, maji ya kunywa, soda, nguo, vipodozi na vitu kadha wa kadha vya urembo. Vilikuwepo pia vikundi vya burudani, vikiwakilisha tamaduni mbali mbali. Nilipata fursa ya kukutana na kuon

Kesho Naenda Faribault, Kwenye Tamasha la Tamaduni

Kesho asubuhi naenda mjini Faribault, kushiriki katika tamasha la tamaduni za kimataifa. Nimeshajiandaa. Vitabu vyangu na machapisho mengine nimeshafungasha. Meza nimeshatayarishiwa. Nitailipia kesho hiyo hiyo. Kitakachokosekana in bendera ya Tanzania, kama nilivyosema katika ujumbe wangu wa tarehe 19 Agosti . Wakati wengine watakapokuwa wanapeperusha bendera za nchi zao na kusema machache kuhusu bendera na nchi hizo, mimi nitabaki naangalia tu. Wakati wa tamasha, nitakuwa napeperusha picha na taarifa kwenye mtandao wa "twitter," Insh' Allah.

Laiti Ningekuwa na Bendera ya Tanzania

Image
Jana nimeona taarifa mtandaoni kuwa Jumamosi hii, tarehe 23, mjini Faribault, Minnesota, kutakuwepo na tamasha la kimataifa la tamaduni . Hapo hapo nilipiga simu kwa waandaaji, ili kuona kama bado kuna nafasi ya mimi kushiriki. Leo mratibu mkuu wa tamasha, amenipigia simu. Tumeongea kwa muda, nami nikamwulizia kama bado kuna nafasi ya kushiriki katika tamasha. Hapo hapo aliniambia kuwa nafasi bado iko, na kwamba tukimaliza maongezi atanitumia fomu ya kujisajili. Tuliongelea shughuli nifanyazo katika jamii, ikiwemo kushiriki matamasha ya aina hii kama mwandishi na mwelimishaji, hasa kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni na athari zake. Tuligusia pia ushiriki wangu katika masuala ya Faribault, kama ilivyotamkwa katika taarifa hii hapa . Wakati tunaendelea na mazungumzo, aliniuliza kama nina bendera ya nchi yangu, yaani Tanzania. Alifafanua kwamba kwenye jukwaa kuu, zitakuwepo bendera za nchi wanakotoka washiriki wa tamasha, na kuna kipindi ambapo wawakilishi wa nchi hizo watakuwepo

Tenzi Tatu za Kale

Image
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katika duka la vitabu la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo , uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi , uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; na Mwanakupona , uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999. Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa "classics." Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anaye

Nimezawadiwa Kitabu: "Picturing Hemingway's Michigan"

Image
Leo nimepata zawadi ya kitabu, Picturing Hemingway's Michigan kilichotungwa na Michael R. Federspiel. Kinahusu sehemu ya kaskazini ya jimbo la Michigan, ambapo familia ya Ernest Hemingway ilikuwa inakwenda kwa mapumziko. Kitabu kina picha na maelezo kuhusu sehemu hiyo, ambapo Hemingway alitembelea tena na tena wakati wa utoto na ujana wake. Hapa ni chimbuko la matukio ya riwaya ya mwanzo ya Hemingway, The Torrents of Spring na hadithi zake ziitwazo  Nick Adams Stories . Nimeletewa kitabu hiki na Bwana David Cooper wa Ohio na mwanae Clay ambaye ni mwanafunzi wangu aliyekuja Tanzania mwezi Januari, 2013 katika kozi yangu ya "Hemingway in East Africa." Baba huyu ndiye aliyetupeleka Montana kwa ndege yake mwaka jana, kuonana na Mzee Patrick Hemingway . Hapa kushoto ni picha tuliyopiga mjini Lakeville, Minnesota, kabla ya kuruka kwenda Montana. Bwana Cooper anaonekana kulia kabisa, halafu anafuata mwanae, halafu mwanafunzi wangu mwingine aliyekuwemo katika kozi y

Nimemaliza Kusoma "The Pearl," Kitabu cha John Steinbeck

Image
Leo asubuhi, nimemaliza kusoma The Pearl , kitabu cha John Steinbeck. Kitabu hiki kimeyagubika mawazo yangu siku nzima. Nilipomaliza kukisoma, nilibaki nimeduwaa, wala sikuweza kuandika ujumbe katika blogu yangu, ingawa nilitamani kufanya hivyo. Ni jioni hii, saa moja na kitu, ndipo nimeweza kuanza kuandika ujumbe huu. Nirudi nyuma kidogo. Wiki kadhaa zilizopita, kitabu hiki nilikitaja katika blogu hii kuwa kimoja kati ya vitabu nilivyokuwa navisoma kwa mpigo. Sikuwa na haraka, bali niliamua mwenyewe muda gani nisome, na katika kusoma, niliamua mwenyewe niishie wapi, siku hadi siku. Mtindo huu naendelea nao kwa vitabu vingine. Haiwezekani kuelezea nilivyojisikia wakati nasoma The Pearl . Ni kama kumwelezea mtu ambaye hajawahi kuumwa na jino au kula embe, jinsi jino linavyouma, au utamu wa embe. Hata hivi, naona nigusie tu kuhusu kitabu hiki, Ni hadithi yenye mvuto wa pekee. Inasisimua, inasikitisha, na inatisha pia. Ni hadithi iliyoniteka, kama vile ndoto ya ajabu au jinamizi. K

Furaha ya Kusainiwa Kitabu

Image
Wapenzi wa vitabu wakishajipatia nakala ya kitabu cha mwandishi fulani, huguswa pale mwandishi anaposaini kitabu hicho. Aghalabu mwandishi huandika ujumbe mfupi kwa mteja huyu na kasha kuweka sahihi. Ni jambo linalowagusa sana wasomaji. Mimi mwenyewe, kama mwandishi, nimeshasaini vitabu vyangu vingi. Ninazo baadhi ya picha za matukio haya kutoka miaka iliyopita. Msomaji makini na mwanablogu Christian Bwaya hivi karibuni ameelezea vizuri katika blogu yake , hisia zake baada ya kujipatia kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences ambacho nilikuwa nimekisaini : Namshukuru kwa dhati mwandishi wa kitabu hiki, Prof. Mbele kwa kunitumia kitabu hiki bila malipo, tena kwa gharama zake. Si jambo linalowatokea wengi. Ni furaha iliyoje hatimaye nimekipokea leo asubuhi. Naanza kukisoma kitabu hiki kwa mara nyingine, safari hii kikiwa na saini ya mwandishi. Ni upendeleo na muujiza wa pekee kunitokea katika siku za hivi karibuni. Ni lazima nimshukuru kwa dhati. Asan

Watoto Katika Tamasha la Afrifest 2014

Image
Kati ya watu waliotembelea meza yangu jana kwenye tamasha la Afrifest, alikuwepo mto anayeonaka katika picha hapa kushoto. Ninawapenda watoto, Kila nikipata fursa ya kutembelea darasa la watoto, napenda kuwasimulia hadithi na mambo mengine. Nimefanya hivyo sehemu mbali mbali hapa Marekani, kama vile Colorado, Minnesota, na Pennsylvania. Mtoto huyu alifika hapa mezani pangu ghafla, wakati namalizia kutafuna vipande vya kuku, Nilikuwa nimesalimiana na wazazi wake, kama nakumbuka sawa sawa, nao walikuwa pemdeni wakiangalia vitabu. Binti yangu Zawadi alipoona naongea na mtoto, alifanya uamuzi wa haraka wa kupiga hii picha, hata kabla sijasafisha meza, kwani mtu huwezi kujua mtoto atakuwepo hapo dakika au sekunde ngapi. Unapoongea na motto, unakuwa katika mtihani mzito, wa kujua sio tu mambo ya kumwambia, bali namna ya kuongea naye ili avutiwe na aendelee kukusikiliza. Unapaswa kumweleza mambo yanayomgusa. Binafsi, nikishauliza jina na mtoto, napenda kujua kama yuko shuleni. Na ka

Tamasha la Afrifest Limefana

Image
Tamasha la Afrifest 2014 lilifanyika jana na leo hapa Minnesota. Jana jioni, shughuli ikuwa ni maonesho ya mavazi na muziki, kama inavyoonekana katika tangazo hapa kushoto. Sikuweza kuhudhuria shughuli za jana, kutokana na masuala ya matibabu, lakini leo nimejikongoja hadi Brooklyn Park, ambako shughuli ya leo ilifanyika. Kule nilipata taarifa za mambo ya jana, kwamba yalifanikiwa vizuri kabisa. Leo niliweza kwenda kuhudhuria Brooklyn Park ambako shughuli ziliendelea, kama ilivyopangwa. Nilikuwa pamoja na binti zangu, Assumpta na Zawadi. Kama kawaida, watu kutoka nchi mbali mbali za Afrrika, Marekani, na kwingineko walihudhuria. Kulikuwa na maonesho ya vitu  mbali mbali, kuanzia mavazi, vitu vya urembo, vitabu na machapisho mengine. Vile vile vile walikuwepo wauza vyakula. Benki ya Wells Fargo. ambayo sasa huhudhuria Afrifest kila mwaka, ilikuwa na banda lake, ambapo paliwekwa taarifa za huduma za benki hiyo, na watu walikuwa na fursa ya kujiunga kama wateja. Ilipokaribia j