Kesho Naenda Faribault, Kwenye Tamasha la Tamaduni

Kesho asubuhi naenda mjini Faribault, kushiriki katika tamasha la tamaduni za kimataifa. Nimeshajiandaa. Vitabu vyangu na machapisho mengine nimeshafungasha. Meza nimeshatayarishiwa. Nitailipia kesho hiyo hiyo.

Kitakachokosekana in bendera ya Tanzania, kama nilivyosema katika ujumbe wangu wa tarehe 19 Agosti. Wakati wengine watakapokuwa wanapeperusha bendera za nchi zao na kusema machache kuhusu bendera na nchi hizo, mimi nitabaki naangalia tu.

Wakati wa tamasha, nitakuwa napeperusha picha na taarifa kwenye mtandao wa "twitter," Insh' Allah.

Comments

Nakutakieni safari njema kaka. Nenda na urudi salama utujuze yatakayojiri huko insh'Allah.
Mbele said…
Shukrani kwa ujumbe wako. Niilikwenda kuhudhuria tamasha. Ninaandika taarifa katika blogu hii na nimeanza kuandika pia katika blogu ya ki-ingereza

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini