Posts

Showing posts from May, 2013

Kinana, CCM Wanapanga Njama za Kumvua Lissu Ubunge

Image
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TAARIFA KWA UMMA KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI!!! Dar es Salaam, 31 Mei 2013... Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali njama za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amedai kwamba CHADEMA imekamata nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliowakuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Mh. Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu. Kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27

Siku ya Vijana Kuhitimu

Image
 Leo hapa chuoni St. Olaf tulikuwa na sherehe ya wanafunzi kuhitimu shahada ya kwanza. Kama kawaida kulikuwa na umati mkubwa wa watu, kuanzia wahitimu na ndugu na marafiki zao, wanafunzi wengine, na sisi walimu. Ni siku ya furaha kwa wanafunzi wanaohitimu, lakini pia siku ya masononeko, kwani wanaondoka mahali ambapo walipazoea na wanaachana na watu ambao waliwazoea, kwa miaka minne. Hapa kushoto niko na mwanafunzi mojawapo ambaye nilikuwa naye Tanzania mwezi Januari, katika kozi niliyofundisha juu ya mwandishi Ernest Hemingway. Hapa kushoto niko na mwanafunzi ambaye alikuwa mmoja wa wale niliowaleta Tanzania mwaka 2011, kwa masomo katika mpango wa LCCT . Kwa mujibu wa mpango huo, mwanafunzi huyu alisoma chuo kikuu Dar es Salaam kwa muhula moja. Hilo vazi nililovaa ndilo wanalopata wahitimu wa shahada ya uzamifu (PhD) katika chuo kikuu cha Wisconsin, Marekani, ambapo nilisoma 1980-86, nikahitimisha na tasnifu juu ya "The Hero in the African Epic." Rangi za mavazi

Mkutano wa Watu Wenye Asili ya Afrika, Minnesota

Image
Leo nilienda St. Paul, kushiriki katika mahojiano kuhusu watu wenye asili ya Afrika wanaoishi Minnesota. Watu kadhaa walihojiwa, kila mtu peke yake, na mahojiano yamerikodiwa ili hatimaye itangenezwe video ambayo itaonyeshwa kwenye mkutano utakaofanyika tarehe 28, 29, 30 Juni. Mkutano huo, ambao unaratibiwa na Minnesota Humanities Center na Council on Black Minnesotans, utakuwa na mijadala na maonesho kuhusu watu wenye asili ya Afrika, kama vile historia, siasa, utamaduni. Aliyeandaa mahojiano ya leo ni Tene Wells, ambaye amefanya kazi kubwa. Katika picha inayoonekana hapa, tuko baadhi ya watu tulioshiriki shughuli ya leo. Kutoka kushoto ni Adebayo, Joseph Mbele, Tene Wells, Profesa Mahmoud el-Kati, na Adrian Mack.

Hotuba ya "Sugu" Bungeni

MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)  1. UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’ Mheshimiwa Spika, Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuha

Ziara Namanga, Januari 26

Image
Katika mizunguko yangu na wanafunzi nchini Tanzania mwezi Januari tukisoma na kujadili maandishi ya Ernest Hemingway, tulifanya ziara ya mji wa Namanga tarehe 26. Mji huo uko mpakani baina ya Kenya na Tanzania. Hemingway na msafara wake walipita hapa, tarehe 20 Desemba, 1933, wakitokea Kenya, wakaingia Tanganyika. Katika vitabu vya watu kama Carlos Baker na Michael Reynolds kuna masimulizi ya jinsi wasafiri hao walivyopita hapa. Hemingway na wenzake hawakukaa Namanga. Walikamilisha tu taratibu za uhamiaji na forodha, wakaelekea Arusha. Katika kuandaa kozi yangu, niliona ni muhimu nikawafikishe wanafunzi Namanga. Ingekuwa tuna muda, tungeenda hadi Kenya na kuzunguka sehemu ambamo Hemingway alipita, kabla ya kuja Tanganyika. Kwangu kama mtafiti, nina masuala ya kuyafanyia kazi. Kwa mfano, je, kuna picha za Namanga za wakati ule Hemingway alipopita hapa? Je, ofisi ya forodha na uhamiaji ilikuwaje siku zile? Kuna hifadhi yoyote ambayo ina taarifa za kupita kwa msafara wa Hemingwa

Mdahalo wa Dr. Slaa, ITV, Utumike Mashuleni

  (CHANZO: Makala hii niliichapisha wakati wa kampeni za mwaka 2010. Inapatikana hapa) ------------------------------------------------------------------------------------------------------ Mimi ni mwalimu, mwenye uzoefu wa kufundisha tangu mwaka 1976, nilipoanza kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na hatimaye kutoa mihadhara katika vyuo vikuu sehemu mbali mbali duniani. Kutokana na wadhifa wangu, napenda kusema kuwa ingekuwa bora iwapo mdahalo wa Dr. Slaa ITV ungesambazwa mashuleni, kwani una mambo muhimu ya kuwafundisha vijana wetu. Jambo la kwanza ni kuwa mdahalo ule unatoa changamoto kuhusu masuala ya nchi yetu, ni kichocheo cha fikra. Jambo la pili ni kuwa vijana wetu wakiona jinsi Dr. Slaa anavyoyakabili masuali, kwa ufasaha, ufahamu, na kujiamini, wataona mfano wa kuiga na kigezo cha kujipima. Wataelewa kuwa wana wajibu wa kujielimisha sana. Wengi tunafahamu jinsi kiwango cha elimu kilivyoporomoka nchini, kiasi kwamba hata kwenye mahojiano ya kutafuta a
Image
Walimu Tunduru walia na mazingira duni ya kazi    CHANZO: Blogu ya Maendeleo ni Vita Na Albano Midelo Baadhi ya walimu katika sekondari ya Frankweston Tun duru MAZINGIRA duni ya kufanyia kazi yaliyopo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma yanatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha wilaya hiyo kuwa duni katika elimu ya msingi na sekondari. Hayo yamesemwa na baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo katika mahojiano maalum ya kutambua kwanini wilaya hiyo inakuwa ya mwisho kitaaluma katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea vijijini,Songea manispaa,Nyasa,Mbinga,Namtumbo na Tunduru. Teresphol Ngonyani ni mwalimu wa sekondari ya Frankweston anazitaja sababu za wilaya hiyo kuwa ya mwisho kuwa ni pamoja na maslahi duni ya walimu wanaoishi na kufanya kazi katika mazingira magumu kama ya wilaya ya Tunduru hivyo walimu wamepoteza moyo wa kufanyakazi. “Kama moyo wa mwalimu umekufa kufanyakazi hata serikali ingelet