Mahagonny: Tamthilia ya Bertolt Brecht

Mwishoni mwa mwaka jana, mwanafunzi wangu mmoja hapa chuoni St. Olaf aliniomba afanye kozi ya kujitegemea chini ya usimamizi wangu. Tuna utaratibu wa kuwapa wanafunzi wanaohitaji fursa ya kufanya kozi za aina hiyo. Mwanafunzi anajitungia mada kwa kushauriana na profesa, na anaifanya kozi kwa kusoma vitabu na maandishi husika, kukutana na profesa mara kwa mara kujadiliana, anaandika makala na kufanya mitihani kadiri profesa anavyopanga. Baada ya mazungumzo ya awali na mimi kuelewa alichotaka mwanafunzi huyu, kwamba alitaka kujielimisha kuhusu Marxism, na kwa kuzingatia masomo mengine anayosoma, katika sayansi ya jamii, nilimshauri kuwa mada ya kozi yake iwe "Marxism, Alienation and Culture." Ingekuwa rahisi kwangu kuandika makala hii kwa ki-Ingereza, kwani sina hakika nitafsiri vipi dhana ya "alienation" kwa ki-Swahili. Ili kuitafakari mada hii kinadharia, nilipendekeza mwanafunzi asome na tujadili ufafanuzi wa Marx na Istvan Meszaros kuhusu "alienation.&q