Posts

Showing posts from November, 2016

Kitabu cha Historia ya Chai

Image
Leo nimenunua kitabu, A Brief History of Tea , cha Roy Moxham, nilichokiona jana katika duka la vitabu la hapa chuoni St. Olaf. Nilivutiwa na taarifa kwenye jalada la nyuma: Behind the wholesale image of the world's most popular drink lies a strangely murky and often violent past. When tea began to be imported into the West from China in the seventeenth century, its high price and heavy taxes made it an immediate target for smuggling and dispute at every level, culminating in international incidents like the notorious Boston Tea Party. In China itself the British financed their tea dealings by the ruthless imposition of the opium trade. Intrepid British tea planters soon began flocking to Africa, India and Ceylon, setting up huge plantations. Workers could be bought and sold like slaves. Maelezo haya yalinisisimua nikaona sherti nikinunue kitabu hiki. Niliona wazi kuwa kitanielimisha kuhusu mengi tusiyoyajua juu ya chai, kinywaji ambacho wengi tunakitumia. Mambo hayo ni pa

"A Far Cry From Africa," Shairi la Derek Walcott

Image
Tangu nilipoanza kufundisha katika chuo cha St. Olaf, mwaka 1991, nimepata fursa ya kusoma na kufundisha fasihi iliyoandikwa kwa ki-Ingereza kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyowezekana nilipokuwa ninafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwandishi mmojawapo ambaye kazi zake nimezishughulikia sana ni Derek Walcott wa St. Lucia, pande za Caribbean, maarufu kwa utunzi wa mashairi na tamthilia, ambaye alipata tuzo ya Nobel mwaka 1992. Nimesoma na kufundisha mashairi yake mengi na tamthilia zake kadhaa. Moja ya mashairi hayo ni "A Far Cry From Africa," ambalo lilichapishwa mwaka 1962. Linaelezea mahuzuniko juu ya vita ya Mau Mau nchini Kenya iliyodumu kuanzia mwaka 1952 hadi 1960. Masetla wazungu walipigana na wa-Afrika waliotaka kuchukua ardhi yao iliyoporwa. Kwa kuwa Derek Walcott ni chotara, damu ya kizungu na ki-Afrika, alihisi vita hiyo ikitokea ndani ya nafsi yake. Uhasama na ukatili wa pande hizo mbili aliuhisi mithili ya su

Ninaendelea Kusoma "Hamlet"

Image
Miaka miwili iliyopita, niliandika katika blogu hii kuwa nina tabia ya kusoma vitabu kiholela. Wakati wowote nina vitabu kadhaa ninavyovisoma, bila mpangilio maalum, na pengine bila nia ya kufikia mwisho wa kitabu chochote. Kusoma kwa namna hii hakuna ubaya wowote, bali kuna manufaa. Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, katika seminari ya Likonde, mwalimu wetu, Padri Lambert OSB alituhimiza tuwe na mazoea ya kusoma sana vitabu, na pia mazoea ya kuvipitia vitabu kijuu juu, ambayo kwa ki-Ingereza huitwa "browsing." Nikiachilia mbali vitabu ninavyofundisha, wakati huu nimezama zaidi katika kusoma Hamlet , kama nilivyoandika katika blogu hii.  Ninasoma Hamlet pole pole, ili kuyanasa vizuri akilini yaliyomo, hasa maudhui kuhusu maisha, maadili, na tabia za binadamu. Kusoma pole pole kunaniwezesha kukifurahia ki-Ingereza cha Shakespeare, ingawa si rahisi kama ki-Ingereza tunachotumia leo. Tofauti kati ya ki-Ingereza cha leo na kile cha Shakespeare ninaifananisha na tofauti

"Ozymandias:" Shairi la Shelley na Tafsiri Yangu

Percy Bysshe Shelley ni mmoja kati ya washairi maarufu kabisa katika ki-Ingereza, ambaye nilimtaja jana katika blogu hii. Alizaliwa mwaka 1792 akafariki mwaka 1822. Ni mmoja wa washairi wanaojumlishwa katika mkondo uitwao "Romanticism," ambamo wanaorodheshwa pia washairi wa ki-Ingereza kama William Blake, William Wordsworth, Samuel Taylor Coleridge, na Lord Byron. "Romanticism" ni mkondo uliojitokeza katika mataifa na lugha zingine pia, kama vile Ujerumani na Ufaransa. Kwa waandishi wa Afrika au wenye asili ya Afrika waliotumia ki-Faransa, "Romanticism" ilijitokeza kama "Negritude," jambo ambalo nimeelezea katika mwongozo wa Song of Lawino . "Ozymandias" ni shairi mojawapo maarufu la Shelley. Ninakumbuka kuwa nililisoma kwa mara ya kwanza nilipokuwa sekondari, miaka ya kuanzia 1967. Kitu kimoja kinacholitambulisha shairi hili kuwa ni la mkondo wa "Romanticism" ni ule mtazamo wake ambao Edward Said aliuita "Orientalism

Mashairi Mazuri ya Ki-Ingereza

Tangu ujana wangu, nimebahatika kusoma na kuyafurahia mashairi mazuri ya ki-Ingereza. Ninakumbuka nilivyoingia kidato cha tano, Mkwawa High School, mwaka 1971, nikakutana na Mugyabuso Mulokozi na Kulikoyela Kahigi ambao nao walikuwa wanafunzi. Walikuwa na kitabu cha mashairi ya ki-Ingereza, tukawa tunayasoma na kuyafurahia. Mifano ni shairi la Thomas Hardy, "An Ancient to Ancients." Mashairi ya Shakespeare yaitwayo "sonnets" yalituvutia. Mfano ni "Sonnet 18" ambayo mstari wake wa kwanza ni "Shall I compare thee to a summer's day?" Shairi la Samuel Taylor Coleridge, "The Rime of the Ancient Mariner," lilikuwa daima mawazoni mwetu. Shairi la W.B. Yeats, "The Second Coming," ni moja ya mashairi yaliyonigusa sana, kama nilivyoandika katika blogu hii. Shairi la Walter de la Mare, "The Listeners," limeng'ang'ania akili mwangu tangu enzi zile. Mashairi mengine tulisoma darasani, kama vile yale ya Percy Bys

Ninajikumbusha "Hamlet"

Image
Wiki hii, pamoja na majukumu ya kawaida ya kufundisha, nimeamua kujikumbusha enzi za ujana wangu kwa kusoma Hamlet , tamthilia mojawapo maarufu kabisa ya Shakespeare. Kila ninapokumbuka tamthilia hii, ninakumbuka nilivyoangalia filamu yake yapata mwaka 1971, Mkwawa High School, Iringa.  Sir Laurence Olivier aliigiza nafasi ya Hamlet, kama nilivyogusia katika blogu hii. Miaka ile ya ujana, tulifahamu ki-Ingereza vizuri hadi kusoma maandishi ya Shakespeare na kuyafurahia. Shakespeare ni kipimo kizuri cha ufahamu wa ki-Ingereza. Umahiri wake katika kutumia maneno na kutunga sentensi unadhihirika katika tungo zake zote. Ninanukuu hapa hotuba ya Claudius, mfalme wa Denmark, kwa Hamlet, ambayo ni kielelezo cha umahiri huo: Tis sweet and commendable in your nature, Hamlet, To give these mourning duties to your father; But you must know, your father lost a father; That father lost, lost his, and the survivor bound In filial obligation for some term To do obsequious sorrow. But to

Nimeteuliwa Kwenye Bodi ya Rochester International Association

Image
Mwezi huu nimeteuliwa kujiunga na bodi ya Rochester International Association, ambayo makao yake ni mjini Rochester, Minnesota. Rochester International Association inashughulika na program mbali mbali za kujenga mahusiano mema miongoni mwa watu wa mataifa na tamaduni mbali mbali. Moja ya programu hizo ni tamasha liitwalo World Festival, linalofanyika kila mwaka. Nimewahi kushiriki tamasha hili mara mbili, nikaelezea habari zake katika blogu yangu ya ki-Ingereza, na blogu hii ya hapakwetu. Shughuli za bodi ni za kujitolea. Kwa miaka yote niliyoishi hapa Marekani, nimejionea jinsi wa-Marekani wanavyozijali shughuli za kujitolea, nami nimekuwa nikishiriki shughuli za aina hiyo, kama vile katika programu zinazowapeleka wanafunzi Afrika. Kujitolea kwa manufaa ya jamii kunaleta faraja na furaha moyoni. Kushiriki kwangu katika Rochester International Association kutaniwezesha kuchangia mawazo katika masuala ya tamaduni kama nilivyoyaelezea katika kitabu changu, Africans and Ameri

Buriani Mwandishi John Calvin Rezmerski

Image
Leo hapa Minnesota zimeenea taarifa za kufariki kwa mwandishi John Calvin Rezmerski. Taarifa moja imechapishwa katika Minneapolis Star Tribune . Nilipata bahati ya kuonana naye miaka michache iliyopita mjini Mankato, Minnesota, kwenye tamasha la vitabu, Deep Valley Book Festival. Tuliongea, nikanunua kitabu chake cha mashairi kiitwacho What Do I Know?: New & Selected Poems , ambacho alikisaini hivi: for Joseph Mbele-- Wonderful to talk with you at Deep Valley Book Festival, John Calvin Rezmerski Taarifa tulizopata leo zinaelezea mambo mema mengi ya bwana Rezmerski: alikuwa mwandishi makini wa mashairi, msimuliaji hadithi, mwalimu aliyependwa, mkarimu kwa watu. Kuhusu falsafa ya ushairi ya Rezmerski, Bill Holm, ambaye ni mwandishi maarufu hapa Minnesota, aliwahi kuandika: "John Rezmerski believes that poetry lives inside the daily speech of ordinary people, that the ear and the mouth are connected to the imagination and the heart." Dhana hiyo ya ushairi inanikum

Mteja wa Uingereza Kanunua Kitabu

Image
Leo kwenye tovuti ninapochapisha vitabu vyangu nimeona kuwa mteja aliyeko Uingereza amenunua nakala ya Notes on Achebe's Things Fall Apart . Uzuri wa uchapishaji wa namna hii ninayotumia ni kuwa mwandishi unaweza kufuatilia taarifa kama hizi za mauzo, ukajua kitabu kimenunuliwa sehemu gani ya dunia, nakala ngapi, na malipo yako ni kiasi gani. Kwa miaka yote tangu nilipoanza kuchapisha vitabu kwenye tovuti ya lulu.com maelfu ya wateja walionunua vitabu vyangu wamefanya hivyo kutokea hapa Marekani. Nilikuwa na hisia kuwa hii ni kwa kuwa utamaduni wa kununua vitu mtandaoni ulikuwa bado kujengeka sehemu zingine za dunia. Ninahisi kuwa huyu mteja aliyenunua Notes on Achebe's Things Fall Apart ni mwalimu wa fasihi. Kama ni hivyo, ninafurahi kuwa atapata mawazo mapya juu ya Things Fall Apart . Ingawa kuna miongozo mingi ya Things Fall Apart , mwongozo wangu umepata umaarufu hata ukateuliwa kama mwongozo kwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Cornell, ambacho kina jina kubwa

Nimenunua Webster's Concise Dictionary and Thesaurus

Image
Jana nilinunua nakala ya Webster's New World Concise Dictionary and Thesaurus , iliyochapishwa mwaka 2014. Hili ni toleo jipya la kitabu hiki ambacho kimekuwa kikichapishwa kwa miaka mingi. Kitabu hiki ni hazina ya pekee kwa kuwa kinajumlisha kamusi na "thesaurus." Kwa wale wasiofahamu tofauti za vitu hivi viwili, napenda kusema kwa kifupi kwamba kamusi hutoa tafsiri za maneno. "Thesaurus," badala ya kutoa tafsiri ya neno, huorodhesha maneno ambayo maana zake zinafanana au kukaribiana na neno hilo. Kwa mfano, katika kitabu nilichonunua leo, sehemu ya thesaurus, neno "docile" limewekewa maneno yafuatayo: "meek, mild, tractable, pliant, submissive, accommodating, adaptable, resigned, agreeable, willing, obliging, well-behaved, manageable, tame, yielding, teachable, easily influenced, easygoing, usable, soft, childlike." Mfano huu unaonyesha wazi ubora na upekee wa "thesaurus." Kwa kuyaorodhesha maneno yenye maana zinazofanan