Tutasoma Visa vya Iceland

Muhula ujao, katika kozi yangu ya Folklore, nitafundisha fasihi simulizi kutoka nchi mbali mbali, kama kawaida. Lakini kwa mara ya kwanza, nitafundisha fasihi simulizi kutoka Urusi na Iceland. Hapo pichani ninaonekana nikiwa nimeshika kitabu kiitwacho Hrafnkel's Saga and Other Icelandic Stories. Wanataaluma wa fasihi simulizi wanaelewa kuwa haya masimulizi yaitwayo saga ni ya nchi za ulaya Kaskazini, kama Iceland na Ireland. Ni sawa na tendi za kale katika utamaduni wa wa-Swahili. Nilivutiwa na wazo la kuhusisha fasihi simulizi ya Iceland katika kozi yangu ya Folklore, kutokana na kufundisha utungo wa Kalevala kutoka Finland. Utungo huu , ambao umetafsiriwa katika lugha nyingi, ikiwemo ki-Swahili, iulinifungua macho kuhusu fasihi simulizi ya Ulaya ya kaskazini. Mvuto wa usimuliaji wa hadithi, mila na imani zilizomo zilinigusa kwa namna ya pekee. Kuhusu hizi saga, kwa miaka mingi nilikuwa ninafahamu uwepo wake, na nilifahamu majina ya baadhi ya hizi saga. Wakati ninasoma k