Ziara Namanga, Januari 26

Katika mizunguko yangu na wanafunzi nchini Tanzania mwezi Januari tukisoma na kujadili maandishi ya Ernest Hemingway, tulifanya ziara ya mji wa Namanga tarehe 26. Mji huo uko mpakani baina ya Kenya na Tanzania.

Hemingway na msafara wake walipita hapa, tarehe 20 Desemba, 1933, wakitokea Kenya, wakaingia Tanganyika. Katika vitabu vya watu kama Carlos Baker na Michael Reynolds kuna masimulizi ya jinsi wasafiri hao walivyopita hapa. Hemingway na wenzake hawakukaa Namanga. Walikamilisha tu taratibu za uhamiaji na forodha, wakaelekea Arusha.

Katika kuandaa kozi yangu, niliona ni muhimu nikawafikishe wanafunzi Namanga. Ingekuwa tuna muda, tungeenda hadi Kenya na kuzunguka sehemu ambamo Hemingway alipita, kabla ya kuja Tanganyika.

Kwangu kama mtafiti, nina masuala ya kuyafanyia kazi. Kwa mfano, je, kuna picha za Namanga za wakati ule Hemingway alipopita hapa? Je, ofisi ya forodha na uhamiaji ilikuwaje siku zile? Kuna hifadhi yoyote ambayo ina taarifa za kupita kwa msafara wa Hemingway hapa mpakani?

Pamoja na maandishi ya hao akina Baker, Reynolds, na wengine, labda Hemingway mwenyewe aliandika kuhusu tukio la kuingia Tanganyika. Hatujui. Labda uchapishaji wa barua zote za Hemingway unaoendelea utasaidia, endapo itapatikana barua ya aina hiyo. Kwa sasa hatuwezi kujua, isipokuwa ni faraja kujua kuwa Hemingway alikuwa mwandishi wa barua wa aina yake, aliyeandika maelfu ya barua.


Comments

Kitoto said…
Pro Mbele, hii mada muhimu sana sana. Juu ya sababu ulizoziandika za utafiti pia tuchangie suala zima la elimu, fasihi na uandishi. Ingekuwa vyema labda utuandikie makala fupi kidogo kusaidia kuwajulisha wasiomfahamu mwandishi Ernest Hemingway vizuri. Maana alifariki zamani na sijui kama vitabu vyake vyapatikana Tanzania siku hizi; sisi tulibahatika kusoma "For Whom The Bell Tolls" katika fasihi tukiwa sekondari. Leo je?
Kitabu chake kingine maarufu "Snows of Mount Kilimanjaro" kilizungumzia chui aliyefariki juu ya ule mlima. Kilisaidia kujenga jina la mlima, Tanzania na Afrika Mashariki kwa wasomaji wake duniani. Huo ni mfano mmoja.
Wa pili ni mada nzima ya kusoma na kuandika leo Bongo.
Waandishi wengi chipukizi (hawa walioshakua na uzoefu katika mablog na magazetini) wanaweza faidika na ufundi wake wa kuandika lugha nyepesi, jambo alilofaidisha waandishi wengi sana sana ulimwenguni.
Nakumbuka tukiwa vijana, miye na marehemu Adam Lusekelo tulizungumzia sana hilo- suala la lugha nyepesi na kueleweka. Aghalabu ukichunguza maandishi ya Lusekelo (hata kiasi fulani yangu) au marehem Mike Sikawa yamefaidika na hilo. Utumiaji wa lugha nyepesi isiyobabaisha, inayoeleweka bila kujaribu kumtisha msomaji kuwa analosoma ni gumu.
Wewe Mbele huandika pia vile; rahisi kusomeka na kueleweka. Waandishi wakongwe wa habari, Ndimara Tegambwage, Jenerali Ulimwengu hali kadhalika. Na vijana wanaofahamika leo: Maggid Mjengwa, Jeff Msangi, Issa Michuzi, lugha zao nyepesi...bila kutisha. Hemwingway alianzia kazi kama mwanahabari ndiyo maana alijifunza mapema kueleweka haraka unapoandika.
Ndiyo kati ya mawazo yanayokuja kichwani jina la Ernest Hemingway (aliyeshinda tuzo la Nobel mwaka 1954) linapotajwa.
Kati ya mambo ninayohusudu kwake pia ni kule kuchukulia kazi ya uandishi kama kazi, mathalan alikua akiandika huku amesimama. Hiyo ni bab kubwa.
Sipendi kwamba alikua mlevi, jambo ambalo linasemekana lilichangia kwake kujiua. Lakini hayo si muhim kama yake bora.
Ahsante sana kwa habari hii - inachangamsha, inaelemisha na ni tofauti na nyingine za kawaida tulizozoea.
Wanataaluma andikeni blogu kama za Mbele!!!
Mbele said…
Ndugu Macha, shukrani kwa ujumbe wako murua. Yote uliyoyasema ni muhimu. Napenda tu nilete hapa muhtasari wa mawazo yaliyonifanya nitunge kozi juu ya Hemingway na uhusiano wake na Afrika. Katika kupendekeza kozi hii kwa chuo cha St. Olaf, niliandika hivi:

Ernest Hemingway, arguably the most famous twentieth century writer in English, was a man of many dimensions. Famous as a great writer of novels and short stories, he also wrote non-fiction and poems. People know him as a big game hunter, deep-sea fisherman, world traveler, and hard drinker. His detractors lament his attitude towards, and relationships with, women. During his lifetime, he married four women in succession and had mistresses along the way.

When people talk about Hemingway, they focus on his life and adventures in the USA, Cuba, Europe, and perhaps Asia. They focus on his writings about those places. They know, for example, about his time in Paris, among exiled American writers like Gertrude Stein and Ezra Pound. They know about his experiences as an ambulance driver in Italy, during the First World War, and his experiences in the Spanish Civil War. Above all, they know about his fascination with bullfighting in Spain.

What is not so well known is Hemingway’s relationship with Africa. Yet, Africa was a key driving force in Hemingway’s life and consciousness, from the time he was a boy, in Oak Park, Illinois, to the time of his death. This course, “Hemingway in East Africa,” explores this aspect of Hemingway: his life-long fascination with Africa, a continent he visited in 1933-34 and 1953-54 and wrote about passionately. As a young boy in Chicago, Hemingway began learning about Africa from visiting the Field Museum of Natural History, where he saw African stuffed lions and elephants, and reading about Teddy Roosevelt’s African safari of 1909. This was a major story that occupied the American public for almost a year, during which Roosevelt traveled and hunted in East Africa. For boys of Hemingway’s time, Roosevelt represented a hero and role model. As a school boy, Hemingway wrote that he wanted to be an adventurer and explorer in unknown places.

The young Hemingway also read other writers, such as Rudyard Kipling and Carl Akeley, who wrote about big game hunting in East Africa. In 1922, while in Paris, he read and reviewed the novel "Batouala," by Rene Maran, a Black Martinican. He greatly admired Maran’s depiction of Africa society. Hemingway finally made his first trip to Africa, in late 1933, traveling and hunting in some of the places his heroes, especially Roosevelt, traveled and hunted in. Hemingway wrote about this trip and after making the second trip, 1953-54, he also wrote about it.

This course will explore Hemingway’s African writings in conjunction with his travels, which inspired them. We will travel in places where Hemingway traveled and hunted, such as the world famous Serengeti National Park. We will see Mount Kilimanjaro, immortalized by Hemingway in his short story, “The Snows of Kilimanjaro.” Through four weeks of travel, reading and cultural engagement, students will learn about the cultures Hemingway encountered and wrote about. Starting with western writers who wrote before Hemingway and inspired him, this course will explore how Hemingway appropriated and transformed that tradition and how he utilized his own individual skills as a writer, which he had learned as a journalist and avid reader. We will read other writers—western and African, such as Joseph Conrad, Maria Thomas, and Ngugi wa Thiong’o—who help illuminate the themes and situations Hemingway dealt with. All instruction will take place in Tanzania, following the route of Hemingway’s first safari. Students will read Hemingway’s "Green Hills of Africa," “The Snows of Kilimanjaro,” “The Short Happy Life of Francis Macomber,” and Under Kilimanjaro. They will also read his letters and journalistic pieces about Africa, as well as a selection of folklore, a tradition that Hemingway also appropriated.
Kitoto said…
Shukrani ...ama kweli Pro Mbele unautumia usomi wako na maisha ya ughaibuni kufunua watu wa pande zote mbili mawazo

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini