Nimekuwa mwanablogu tangu mwaka 2008. Ninaendesha blogu hii ya Hapa Kwetu na nyingine ya ki-Ingereza. Kublogu kuna mambo mengi. Kublogu kunanipa fursa ya kujieleza kwa uhuru. Hili ni jambo la msingi, kama alivyoelezea mwanablogu Christian Bwaya.
Lakini kublogu kuna matokeo yenye manufaa. Kumeniwezesha kuwafikia watu mbali mbali ambao wanatembelea blogu zangu. Siwezi kujua wanapata ujumbe gani katika maandishi yangu. Kama taaluma inayotufundisha, hili ni suala tata.
Ujumbe wa andiko ni zao la kazi anayofanya msomaji juu ya andiko. Na kwa kuwa wasomaji wana akili zinazotofautiana, na wana nidhamu na uzoefu tofauti wa kusoma, kila mmoja anaibuka na ujumbe tofauti, kwa kiwango kidogo au kikubwa.
Niliwahi kuelezea kwa nini ninablogu, lakini sidhani kama nilikuwa na majibu ya uhakika. Baadaye, katika kutafakari suala hili, nilifikia hatua ya kutamka kwamba ninablogu kwa ajili yangu mwenyewe. Labda huu ndio ukweli wa mambo.
Imani iliyojengeka katika jamii ni kuwa mwandishi anawaandikia wasomaji. Tumezoea kuona waandishi wakiulizwa wanamwandikia nani, nao wanaelezea walengwa wao. Jadi hii na imani hii imekosolewa kwa uhodari na Roland Barthes katika makala yake, "The Death of the Author."
Makala hii ya Barthes naona inaipa uzito hoja yangu kuwa ninapoblogu ninajiandikia mwenyewe. Sijui ni nani atasoma au anasoma ninachoandika. Kusema kwamba ninawaandikia wasomaji ni kama kuota ndoto. Ni kujiridhisha kwa jambo ambalo halina uhakika bali ni bahati nasibu. Nikisema ninajiandikia mwenyewe ninasema jambo la uhakika.
Showing posts with label Jielewe blog. Show all posts
Showing posts with label Jielewe blog. Show all posts
Thursday, December 3, 2015
Thursday, August 14, 2014
Nimezawadiwa Kitabu: "Picturing Hemingway's Michigan"
Leo nimepata zawadi ya kitabu, Picturing Hemingway's Michigan kilichotungwa na Michael R. Federspiel. Kinahusu sehemu ya kaskazini ya jimbo la Michigan, ambapo familia ya Ernest Hemingway ilikuwa inakwenda kwa mapumziko. Kitabu kina picha na maelezo kuhusu sehemu hiyo, ambapo Hemingway alitembelea tena na tena wakati wa utoto na ujana wake. Hapa ni chimbuko la matukio ya riwaya ya mwanzo ya Hemingway, The Torrents of Spring na hadithi zake ziitwazo Nick Adams Stories.
Nimeletewa kitabu hiki na Bwana David Cooper wa Ohio na mwanae Clay ambaye ni mwanafunzi wangu aliyekuja Tanzania mwezi Januari, 2013 katika kozi yangu ya "Hemingway in East Africa."
Baba huyu ndiye aliyetupeleka Montana kwa ndege yake mwaka jana, kuonana na Mzee Patrick Hemingway. Hapa kushoto ni picha tuliyopiga mjini Lakeville, Minnesota, kabla ya kuruka kwenda Montana. Bwana Cooper anaonekana kulia kabisa, halafu anafuata mwanae, halafu mwanafunzi wangu mwingine aliyekuwemo katika kozi ya "Hemingway in East Africa," na mimi naonekana kushoto kabisa.
Mwanafunzi aliyeniletea kitabu anaonekana nami pichani hapa kushoto, tukiwa kwenye mpaka baina ya hifadhi za Ngorongoro na Serengeti.
Nilipokipata kitabu hiki, yapata saa saba mchana, nilijawa na furaha, nikaanza kukisoma mara, lakini nikaona nipige kwanza simu kwa walioniletea. Nilimpata Bwana Cooper, nikamshukuru sana. Ameniambia kuwa yeye na mwanae walikiona kitabu hiki katika duka kule sehemu ya Michigan Kaskazini, wakaniwazia. Baada ya maongezi nimeendelea kukisoma, nikamaliza baada ya masaa mawili hivi..
Wameninunulia nakala yenye sahihi ya mwandishi, kama inavyoonekana hapa kushoto. (Ninaposema hivi, mawazo yangu yameshakwenda kwenye mazungumzo baina yangu na Ndugu Christian Bwaya kuhusu suala hili la kusainiwa vitabu).
Nilifahamu kuwa sehemu hii ya Michigan Kaskazini ni muhimu katika utoto na ujana wa Hemingway, lakini kitabu hiki kimenifungua macho zaidi kwa kuonyesha sehemu mbali kwa picha na maelezo. Picha nyingi ni za mtoto Hemingway na watoto wengine katika familia yao, picha za wanaukoo, na sehemu mbali mbali. Nyingi katika ya picha hizo sikuwa nimeziona kabla. Kwa yote hayo, nimefurahi sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Jina la Shaaban Robert ni maarufu miongoni mwa wa-Tanzania na wengine wa nchi zingine wanaokijua ki-Swahili. Lakini, tujiulize ni wa-Tanza...