Saturday, December 3, 2016

Msikilize Rais Yahya Jammeh Anavyokubali Ushindi wa Mpinzani

Msikilize Rais Yahya Jammeh wa Gambia anavyokubali matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo mpinzani ameshinda. Rais Jammey, bila kusita, anasema kuwa kwa kura zao, wananchi wa Gambia wamenena, naye anayapokea matokeo. Anampongeza mpinzani kwa ushindi wake, na anaahidi kumpa ushirikiano kuanzia kipindi hiki cha mpito. Anamwombea baraka za Allah katika kuiongoza nchi ya Gambia, na anawashukuru watu wa Gambia.

2 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Huyu jamaa, kama Gadaffi, ni kigeugeu hakuna mfano. Umesikia alivyogeuka na kudai uchaguzi mpya? Sikutaka kujiridhisha kuwa huyu jamaa angeondoka kirahisi tokana na uovu aliowafanyia wa-Gambia. Hata hivyo, siku zake zinahesabika. Mie sikushabikia namna alivyoidanganya dunia. Kwa wanaomjua, huyu jamaa ni mwendawazimu anayetumia Uislam na ukandamizaji kuendelea kukaa madarakani. Naweza kusema kwa ufupi tu kuwa sasa Afrika itashuhudia Burundi nyingine. Ni bahati mbaya kuwa mataifa kama Senegal yanayozunguka kiinchi kidogo kama hiki hayaingilii na kumfurusha huyu imla uchwara.

Mbele said...

Ni kweli, inaonekana ametupiga changa la macho sisi tuliomwamini.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...