Wajinga Hunena, CCM Ilileta Uhuru Tanganyika

Kiwango cha ujinga Tanzania kinatisha. Utawasikia wengi wakisema kuwa CCM ilileta Uhuru Tanganyika mwaka 1961. Wajinga wengine, kuanzia wanasiasa hadi watu wa mitaani, husema kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 52.

Utamsikia mwanasiasa anaiponda CCM kwa kuuliza, "Miaka yote 52 ya utawala wa CCM, wananchi mmenufaika vipi?" Na utammsikia kada wa CCM akitamba, "CCM ni chama chenye uzoefu wa miaka 52.

Hapakuwa na CCM mwaka 1961. Chama kilicholeta Uhuru Tanganyika ni TANU. Wala CCM haijawa madarakani miaka 52. Kuna mengi katika historia ya Tanganyika na Tanzania ambayo yanasahaulika au kupotoshwa kwa sababu ya uzembe wa wa-Tanzania.

Wajinga wengine wanasema kuwa leo tunasherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania au Tanzania Bara. Mwaka 1961 hapakuwa na nchi iliyoitwa Tanzania wala Tanzania Bara. Nchi iliyopata Uhuru mwaka ule ni Tanganyika. Inasikitisha.

Comments


Nashukuru Profesa kwa Kuliona hilo. Kwa maana hiyo kuna kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wasomi, wanasiana na ambao hawakupata fursa ya kukaa darasani ili waelewe historia sawasawa. Hiyo itasaidia kizazi hiki na kijacho.

Popular posts from this blog

Tenzi Tatu za Kale

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Filamu ya "Papa's Shadow:" Fursa ya Kuitangaza Tanzania