Tuesday, October 16, 2012

Wa-Kristu Tunamwabudu Allah!

Najua kuwa kichwa cha habari hii kitawashtua wengi. Huenda watu watasema nimechanganyikiwa au nimekufuru.  Huenda wako watakaouliza, "Iweje wa-Kristu wawe wanamwabudu Allah?"

Kwa siku kadhaa, nimekuwa nikijuliza suali: Je, wa-Arabu ambao ni wa-Kristu wanatumia jina gani kumtaja Mungu? Ninafahamu kuwa kuna mamilioni ya wa-Arabu ambao ni wa-Kristu, huko Mashariki ya Kati na sehemu zingine za dunia. Sasa je, Mungu wanamwitaje kwa ki-Arabu?

Nimefanya uchunguzi kidogo nikagundua kuwa jina wanalotumia, ni hilo hilo wanalotumia wa-Islam, yaani Allah. Hili ndilo neno lililopo katika ki-Arabu. Katika Biblia ya ki-Arabu, ambayo huitwa "al-Kitab al- Muqadis" yaani Kitabu Kitakatifu, Mungu anaitwa Allah muda wote.

Nilivyogundua hivyo nimetambua jinsi wengi wetu tulivyopotea, kwani tunaamini kuwa Allah ni tofauti na Mungu. Tunalumbana hadi tunatokwa jasho, na povu mdomoni, kwa umbumbumbu wa kutojua lugha. Taarifa iliyonifungua macho ni hii hapa.


5 comments:

Anonymous said...

asante Profesa Mbele basi hiyo ndio tabu ya watu hapo mkristo(tu)hatakuelewa kama ulivyosema,pofulitamtoka mdomoni mpaka anajiapiza,lakini ndio hapo watu hawataki kuelewa wala kusikia,lakini ndiotabu ya kutawaliwa maana watu wamelishwa upumbavu na wameukubali,nikweli kwa kiarabu mungu anaitwa hivyo,kiswahili mungu,kihaya NYAMUHANGA,RUHANGA,KICHAGA RUWA,KINYAKYUSA KYARA nk lakini wengine ukiwambia KYARA eti huyo nishetani ila kusoma nikuzuri pamoja na kutembea kama wewe ulivyotembea na kuona mengi asantesana ndio maana sikosi kupita hapa kupata busara zako ulivyosema unafikiria kustaafu ukirudi nitakutafuta walau tuongee

Mbele said...

Shukrani mdau, kwa ujumbe wako. Nami nimeshangaa kuona kuwa jina "Allah" haliwahusu wa-Islam tu.

Tukianza kuwaelezea wa-Tanzania ukweli huo, panaweza kutokea uvunjifu wa amani, kwa jinsi umbumbumbu ulivyokithiri.

Shukrani kwa kuleta majina ya Mungu katika hizo lugha mbali mbali za kwetu. Mimi kama mtafiti huwa nafuatilia masuala haya ya mambo ya jadi. Itabidi siku ije ambapo watu watambue na kukiri kuwa majina yote haya yanamtaja Mungu, ambaye wa-Arabu wanamwita Allah. Ruwa ni Allah, Nyamuhanga ni Allah, na kadhalika.

Lakini ndio hivyo, watu wamejichimbia katika ufinyu wa mawazo yao kiasi kwamba ukiwaambia hayo, panaweza kutokea vurumai ya kutisha.

Anonymous said...

Ni kweli kwamba mtu asiejua anakuwa na tatizo kubwa katika kulitumia neno "Allah"na vile vile ukisema neno "Allah"kiufanisi zaidi lina maana kubwa kuliko jina yaani"mwenyezi mungu"ili kumtukuza zaidi.Kwasababu ni mfalme wa wafalme na ndie muumba wa kila kitu.

Ukija katika neno "salam alaikum" lina maana "amani iwe juu yenu/yako" wakati pia mkristo ukimwambia hivo kwa wengine sio wote huwa hawapendi.Ila kwa waisilamu ni moja ya ibada kumjulia mwenzako hali hata kama humjui.

Neno lingine ambalo wengi hawalijui au kulitumia vibaya ni "jihad".Hili neno vile vile ni la kiarabu ambalo lina maanisha kupigania au jitihada kama inavyosemeka kwa english "strive".Lakini limekuwa ni neno moja linatumika kwa propaganda zaidi.







Anonymous said...

Kila mwenye dini anamuabudu mungu wake. Hata kwa Kiswahili, neno ni hilohilo, MUNGU. Ukisema Mkristo Mwarabu anamuabudu Allah, sawa, lakini Mungu anaeabudiwa na Muislam siye anaeabudiwa na Mkristo, labda kama wanaoabudu ndiyo wanafanya makosa. Lakini ukienda kanisani, mtu anaombewa kwa mamlaka ya Mungu, anapona, sivyo ilivyo katika msikiti. Wahindi pia wanasifika kwa kuwa na miungu kibao, hao nao kwa kiarabu ni Allah, maana hiyo ni tafsiri tu.

tz biashara said...

October 23,2012,5:47 AM

Nadhani unajichanganya au huelewi maana ya kuabudu.

Neno la kiarabu "Allah" kwa kiswahili ni mungu au mwenyezi mungu.Ni sawa na kusema kizungu "God"ni masuala ya lugha zaidi na sio imani.

Nadhani Profesa Mbele alimaanisha kwamba kutokana na wengi wasio waisilamu wanaufahamu tofauti kuhusiana na neno Allah ambalo bado linakutatiza.

Haina maana ya kuwa mungu tofauti isipokuwa imani ndio zinatofautiana.Nisawa na tofauti tuliyonayo katika kumtambua "Yesu"(amani iwe juu yake).Waisilamu wanatumia "Issa"(amani iwe juu yake)

Tofauti baina ya wakristo na waisilamu kwa yesu (amani iwe juu yake) ni;
-Wakristo..wanamtambua kama ni mungu (allah)ama mwana wa mungu kwa wengine.
-Waisilamu ..wanamtambua mtume au mjumbe wa mwenyezimungu.
-Na kwa wenzetu mayahudi ambao pia hulingana nasi baadhi ya mitume ni kwamba wao walimkataa yesu (amani iwe juu yake.

Kiukweli tu ni kwamba wahindi unavowazungumzia wewe nadhani inabidi utofautishe ni wahindi gani.Kwani sio wote wenye kuabudu masanamu kwasababu wengine ni wakristo na wengine ni waisilamu.Na hawa wenye kuabudu masanamu wanaitwa hindu's au dini yao inaitwa "buddist"

Niliwahi kusikia muhindi mmoja muisilamu akitfsiri neno hindu,linamaana muhindi kiswahili au hindi ama India.Ni neno la kijografia zaidi na sio nembo ya dini yao ingawaje wao hutumia kama dini.Kwasababu wengi wao wanasema hujifanya kama ile nchi ni ya hao hindu's na ndio maana wanavikundi ambavo huvamia wanavijiji na kuwaua ikiwa kama sio mabuddist.

Kwa hivo tofauti zetu na imani zetu hutofautiana katika ibada zetu na muelekeo wetu ulivo katika nyumba za ibada,lakini neno mungu (allah) tunalitaja midomoni kwetu hata kama imani ni tofauti.

Mwisho kabisa ni kudumisha amani kwani tunaweza tukawa ndugu siku moja ama tukakubaliana katika imani.Na kingine ni kwamba tuvumiliane kutokana na tofauti zetu vinginevo tutamuudhi mwenyezi mungu (Allah)ambae ametuleta duniani kujenga amani miongoni mwetu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...