
Jana jioni nilihudhuria shughuli ya
Cheetah Development mjini St. Paul.
Cheetah Development ni mtandao wa watu wanaojishughulisha na miradi ya maendeleo Afrika Mashariki, hasa Tanzania. Nilijulishwa kuhusu mtandao huu na rafiki yangu Mzee Paul Bolstad, ambaye anaonekana kushoto kabisa hapa pichani.
Yeye na huyu mwingine ni marafiki wa tangu zamani. Wote ni wapenzi wakubwa wa Tanzania. Mzee Bolstad alizaliwa na kukulia Tanzania, na huyu mwenzake walikuwa wote katika programu ya Peace Corps Tanzania walipokuwa vijana.

Walihudhuria watu wengi Kulikuwa na hotuba na maonesho ya shughuli mbali mbali za Cheetah Development.
Kikundi cha kwaya kiitwacho
imuka,
kutoka Bukoba, ambacho kiko katika ziara hapa Marekani, kilitoa burudani.
No comments:
Post a Comment