Wednesday, August 31, 2011

Wadau Wawili Wamenitembelea

Leo hapa Sinza nimepata bahati ya kutembelewa na wadau wawili wa maandishi yangu.

Kwanza alifika ndugu Renatus Mgusii kutoka Segerea. Huyu tumefahamiana mtandaoni na ni msomaji wa maandishi yangu, kuanzia blogu hadi vitabu. Tuliongea mengi kuhusu masuala ya elimu, tofauti za tamaduni na athari zake katika dunia ya leo na mengine kadha wa kadha. Nimefurahi kukutana na mdau huyu, msomaji makini na mwenye uchungu na elimu.Mdau wa pili alifika majira ya jioni. Huyu ni Gilbert Mahenge wa Msoga. Huyu niliwahi kuandika habari zake katika blogu hii, kwamba alikuwa mdau wa kwanza hapa Tanzania kununua na kusoma kitabu changu cha CHANGAMOTO. Niliguswa kumwona amefika na nakala yake. Tumeongea mengi kuhusu siasa, maendeleo na elimu. Alipiga simu Msoga nikapata fursa ya kumsalimia mkuu wa kijiji.

1 comment:

Mbele said...

Nimepitapita kwenye blogu hii na nimeona jinsi tulivyoanza mawasiliano na mdau Mgusii. Angalia kwenye sehemu ya maoni katika makala hii hapa.