Wednesday, August 17, 2011

Leo Ninatimiza Miaka 60

Leo natimiza miaka sitini tangu kuzaliwa. Huu si umri mdogo, nami namshukuru Muumba kwa kunipa fursa ya kuwepo ulimwenguni kiasi hiki. Ninavyokumbuka maisha yangu, ninatamani kama ningekuwa nimefanya mengi na makubwa zaidi kuliko niliyofanya kwa manufaa ya wanadamu. Ninatamani kama ningekuwa nimejiepusha na mabaya, nikawa mtu bora wa kupigiwa mfano. Lakini haiwezekani tena kuirudisha miaka iliyopita. Bora niangalie mbele, nijaribu kufanya bidii zaidi, ingawa sijui nimebakiza miaka mingapi hapa duniani.

8 comments:

Subi Nukta said...

Heko kwa kuadhimisha kumbukumbu ya sikukuu yako ya kuzaliwa.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akujaalie afya njema na fanaka tele!
Happy Birthday Prof. Mbele!

Mbele said...

Asante sana Da Subi, kwa ujumbe wako. Nimeingia Mbeya jioni hii, na ndipo nilipoandika ujumbe wangu. Ninategemea kuwepo hapa hadi tarehe 21. Ubarikiwe sana.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hongera kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwako. Ni kweli. Ni bahati kufikia umri huo. Pia nitumie fursa hii kukupa hongera kwa kuwa muwazi maana watu wetu wengi siku hizi wanakwambia natimiza miaka kadhaa-ulimbukeni bila shaka.Nakuombea Mungu akuongezee 60 uwe mmojawapo wa maajabu ya dunia.
Kila la heri na ujaliwe afya tele.

John Mwaipopo said...

hongera profesa joseph mbele kwa kutimiza miaka 60 tangu ulipozaliwa. uwe na wakati murua katika kusherehekea umri huo, na katika kutafakuri yale yaliyo mbeleni.

Yasinta Ngonyani said...

Jamani sijui nilikuwa nimelala sana...Ila najua sijachelewa HONGERA SANA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 60 ya kuzaliwa kwako. Nakuombea kwa Mungu akupe baraka tele na afya njema na uwe mwenye furaha ili uongeza miaka 60 tena. HONGERA SANA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA.

MICHUZI BLOG said...

HEPI BESDEI YA KUZALIWA KWAKO PROF. MOLA AKUONGEZEE MIAKA KAMA HIYO MINGINE NA MINGINE BAADA YAKE.

sikapundwa christian said...

Hongera Profesa kwa kutimiaza umri huo ,ni jambo la kumshukuru Mungu,Nijamboa la kufurahisha kuona unavyo na ulivyo mwenye afya njema kabisa,utadhani mwenye umri wa miaka 50.Hongera sana Bwana ana asifiwe,ni muda kidogo sijawahi kusoma blog yako hivyo leo nimefungua na kukuta habari njema. Na kumbe upo katika Jiji la Mbeya ambako ni kwa wakwe zangu Mbalizi Mbeya.Karibu sana Jijini humo.
Nakutakia shughuli njema.Wana - Press club Songea wanashukuru sana kuwa nawe katika ukumbi wa Serengeti.
Aidha Bwana Juma Nyumayo amekupongeza sana kwa kujumuika na baadhi ya waandishi wa habari wa Ruvuma.

Unknown said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa Profesa. Mungu akujalie na kukuzidishia miaka tele. Tayari wewe ni mfano wa kuigwa kwetu na nadhani hiyo inatosha katika jamii hii yetu. Tunamshukuru Mungu kwa wewe na tunakuombea ulinzi wake zaidi.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...