Sunday, August 7, 2011
Mdau Kanitembelea
Leo nimepata bahati ya kutembelewa na mdau Emmanuel Sulle ambaye yuko masomoni Chuo Kikuu cha Maryland, College Park. Imetokea kuwa sote tuko Dar es Salaam kwa wakati huu.
Aliniletea ujumbe kuwa anayapenda maandishi yangu akataka kuniona, kwani hatujapata kuonana. Alikodi teksi akanifuata. Yeye ni mtafiti makini mwenye nia thabiti ya kuchangia taaluma kwa maandishi. Tumeongea mengi, kuhusu utafiti na uandishi, pia umuhimu wa kuwahamasisha vijana kujiendeleza kielimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
1 comment:
Aksante sana Profesa kwa fursa ile tuliyopata kubadilishana mawazo mawili matatu. Ninaamini tutaendelea kuwasiliana na kushirikiana zaidi juu ya masuala mazima ya kijamii na kitaaluma. Mungu atupe nguvu na upeo zaidi katika harakati zetu!
Post a Comment