Wednesday, August 10, 2011

Msosi Iringa

Leo nimeshinda Iringa, pamoja na wanafunzi wangu. Safari yetu ni ya masomo, kama nilivyoelezea hapa. Sehemu moja tuliyotembelea ni Chuo Kikuu Kishiriki Iringa tukaonana na kiongozi mmojawapo wa chuo, Mchungaji Dr. Richard Lubawa, mtunzi wa kitabu cha Shoulder to Shoulder.

Pichani naonekana na mwanafunzi Ryan Campbell tukiwa tunaudhibiti ugali na maini katika hoteli ya Wilolesi Hilltop, karibu na Kihesa. Ryan hakuushangaa ugali, kwani alishapambana nao Zambia alipokuwa na miaka 17.
(Picha imepigwa na Bailey Putney)

4 comments:

Simon Kitururu said...

Udenda unanitoka! Nilijaribu kukupigia simu wakati umesema uko Songea kwa kuwa kulikuwa na Rafiki yangu Mfaransa fulani ambaye nilimfanya anunue kitabu chako pia ambaye alikuwa maeneo ila hukujibu!:-(Nilitumia zile namba ulizoweka kumjulisha YAsinta Ngonyani uko maeneo!

Tukiachana na hilo nahisi ntakufuata ulipo ukiwa MAREKANI kwakuwa ntapita karibu na maeneo uishiyo Marekani baada ya kamuda fulani ambako nahisi utakuwa umerudi!

MICHUZI BLOG said...

Safi sana Prof. Usiache kuwaonjesha bada na utumbo wa mbuzi. Usitusahau kututembelea nasi wa Dar pia

Mjengwa said...

Mwalimu Mbele,
Usikose kunipigia. Unakaribishwa na wote nyumbani uje tufuturu kikwetu!
Simu yangu ile ile 0754 678 252 au ukifika Akiba House uliza ofisi za Karibu Tanzania Association. Tuko ghorofa ya tatu chumba namba 324. Na leo nitakuwa ofisini siku nzima.
Maggid

Mbele said...

Jana nilishinda katika mizunguko hadi Kalenga na sikupata fursa ya kuingia mtandaoni, hadi leo.

Ndugu Kitururu, nafurahi kusikia utakuwa na kasafari ka pande zetu. Karibu sana. Samahani kama mawasiliano ya simu nilipokuwa Songea hayakufanikiwa.

Nitazingatia ushauri wako Ankal, wa kuwasogeza maeneo ya utumbo wa mbuzi. Itabidi nimtafute Mwenyekiti Mjengwa atupeleke maeneo hayo kwa hapa Iringa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...