Hapo ni mahala muhimu kwa kwenda kujifunza historia sio tu ya wa-Hehe bali ya Tanzania. Kwa mfano, katika makumbusho haya kuna kuna zana za mawe za kale zilizopatikana Isimila.
Idara inayohusika na hifadhi ya makumbusho hayo inafanya kazi nzuri katika mazingira magumu. Hata hivi, hakuna sababu yoyote kwa nini Tanzania isiweke kipaumbele katika kuipa idara hii kila msaada unaohitajika. Umma wa wa-Tanzania unapaswa pia kuamka ili utambue umuhimu wa makumbusho kama haya. Haipendezi, kwa mfano, kuona watu wanajichukulia viwanja na kujenga nyumba katika maeneo ambayo ni ya kihistoria. Wa-Tanzania tujiulize: je, iwapo ukuta mkuu wa China ungekuwa katika nchi yetu, tungekuwa tumeutunza kama wanavyofanya wa-China? Naogopa kuwa kutokana na elimu duni, watu wangeng'oa mawe ya ukuta huo na kujengea nyumba.
3 comments:
Hongera Prof. Ninapakumbuka sana hapo maana wakati nasoma Tosa ilikuwa karibu sana. Umeitembelea hapo mahali wakati nchi yetu inakosa viongozi wajasiri kama Mkwawa! Natumaini utawapelekea wengi maana ya hayo makumbusho
Kila la kheri katika safari zako
Emmanuel
kila la heri katika safari zako za mafunzo. hatutaonana ukifika mbeya kwani sasa niko nje ya mji huo kwa shuguli zingine.
Shukrani Ndugu Emmanuel. Nitajitahidi kuwajibika ipasavyo, kuhusu hao vijana.
Ndugu Mwaipopo, shukrani kwa ujumbe. Jioni hii ndio nimeingia Mbeya. Insh'Allah tutaonana wakati mwingine. Nitakuwepo hapa hadi tarehe 21.
Post a Comment